Daktari: Tanzania inaongoza kwa unywaji pombe Afrika. Kwa mwaka kila Mtanzania anakunywa ndoo ndogo

Hapo kwenye "kila mtanzania." Mbona tumeanza kujumuishana kwenye mambo ambayo siyo wote tunashiriki?
 
Tangu nisikie jeshi letu no.6 Kwa ubora dunian tangu cku hiyo sifatilii tena tafiti za wabongo😂
 

Sijawahi Ona Dokta muongo kama huyu, ndugu wana JF puuzeni huu uzushi.
 
Sasa ndoo ndogo nayo ya kulalamikia?

Hiyo ndoo ndogo watu wanaikata kwa siku.
... anazungumzia average; chukua kiasi cha pombe yote inayonywewa nchini kwa mwaka gawanya kwa watatnzania wote milioni 61+ (hadi vichanga) ndio unapata wastani wa ndoo ndogo kwa kila mtanzania.

Angeondoa wasiokunywa kwenye hesabu yake ikagawanywa kwa walevi peke yao, watu wangetoka na wastani wa unit ya DAWASA - 1000 ltrs kwa mwaka ==> 3 ltrs kwa siku ==> 8 bottles kwa siku.

Ingegawanywa kwa walevi sugu peke yao watu wangetoka na kreti 1.5 ==> 30 bottles daily!
 
Bado sijajua hizo hesabu za KIWASTANI wametoa wapi...? Yaani mpaka wanafikia huko kujua mimi nakunywa Ndoo ndogo kwa Mwaka hizo hesabu wamaetoa wapi.? Je Kiafya kwa Alc volume ya ndoo ndogo ukigawanya kwa siku 360 je utaniweka kundi la mnywaji hatariii?
 
... data za kiasi cha pombe rasmi (achana na za kienyeji) kinachozalishwa na kuingizwa nchini kila mwaka zipo. Ni suala la kugawanya kwa idadi ya watanzania.
 
... data za kiasi cha pombe rasmi (achana na za kienyeji) kinachozalishwa na kuingizwa nchini kila mwaka zipo. Ni suala la kugawanya kwa idadi ya watanzania.
Katika pombe ambazo sio Rasmi ndio pombe inayonywewa sana kuliko hii rasmi.

Pia lita moja ya Kvant huwezi fananisha na Lita moja ya serenget lite.

Ndoo moja ya Konyagi unaweza toa Pipa la lita 100 za serengeti lite. Hao jamaa wakisema pombe wanatumia rate ipi kuita hichi kiwango cha alc ndio pombe wanayokunywa watanzania?
 
hii tafiti nina mashaka nayo hapo alipo-generalise 'kila mtanzania kunywa ndoo ndogo kwa mwaka', maana tangu nizaliwe mpaka na uzee huu nilionao sijawahi tumia vileo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…