Daktari: Tanzania inaongoza kwa unywaji pombe Afrika. Kwa mwaka kila Mtanzania anakunywa ndoo ndogo

Daktari: Tanzania inaongoza kwa unywaji pombe Afrika. Kwa mwaka kila Mtanzania anakunywa ndoo ndogo

Katika pombe ambazo sio Rasmi ndio pombe inayonywewa sana kuliko hii rasmi.

Pia lita moja ya Kvant huwezi fananisha na Lita moja ya serenget lite.

Ndoo moja ya Konyagi unaweza toa Pipa la lita 100 za serengeti lite. Hao jamaa wakisema pombe wanatumia rate ipi kuita hichi kiwango cha alc ndio pombe wanayokunywa watanzania?
Para yako ya kwanza makes the situation even worse kuliko hata ilivyoripotiwa.

Pombe zote rasmi alcohol contents zinajulikana. In that context, ni rahisi kujua for instance Konyagi X ni equivalent na Serengeti Lite Y. From there you feed data and come up with results; just simple Excel sheet will do the math.
 
hii tafiti nina mashaka nayo hapo alipo-generalise 'kila mtanzania kunywa ndoo ndogo kwa mwaka', maana tangu nizaliwe mpaka na uzee huu nilionao sijawahi tumia vileo!!
Unajua maana ya wastani lakini? Dah!
 
Hapo kwenye kila mtanzania tafadhali Dr mimi niondoe kwenye list yako
 
Dkt Omar Ubuguyu, Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za magonjwa yasiyo ya kuambukiza amesema kwa Wastani, kila Mtanzania anatumia lita 9.1 ya pombe kwa mwaka, sawa na ndoo ndogo ya maji, Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa unywaji wa pombe katika Bara la Afrika.

---

My Take:
Ndio maana Hii Nchi Ina Watu Wana matukio ya ajabu sana kumbe tatizo ni pombe na bangi kupanda kichwani, duu.
Namshauri atafute weekend aende Kenya halafu arudi aite waandishi wa habari atuambie kama kweli watanzania wanaongoza.
 
Kwenye Article ya WHO inasema Africa ni ya nne baada ya Europe; America na West Pacific..., sasa hapo conclusion zako zinatwambia nini on the large scale ? Kwamba Europe na America wana mambo ya ajabu ?
Niko Ujerumani huku pombe ni bei rahisi kuliko maji. Na watu wanakunywa bia asubuhi na pretzel halafu wanaingia mzigoni.
 
Ndoo ndogo mbonaa ngoja nipige mahesabu

Kwa wiki Aver 15 beers za mils 350
15x350= 5250 mls

Kwa mwezi

5250x4= 21,000 Mls

Kwa mwaka
21000x12=252,000 Mls~ sawa na Lita 252

Kama gharama ya 120,000 TSh kwa mwezi

Huyu ni mnywaji sio mlevi.
 
Dkt Omar Ubuguyu, Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za magonjwa yasiyo ya kuambukiza amesema kwa Wastani, kila Mtanzania anatumia lita 9.1 ya pombe kwa mwaka, sawa na ndoo ndogo ya maji, Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa unywaji wa pombe katika Bara la Afrika.

---

My Take:
Ndio maana Hii Nchi Ina Watu Wana matukio ya ajabu sana kumbe tatizo ni pombe na bangi kupanda kichwani, duu.
Mm binafsi nikipimwa huenda nikawa natumia ndoo ndogo 3 mpaka 4 kwa mwaka sijajua wenzangu maana ili nione nimetosheka nione wahudumu wanaanza kutoa viti
 
Unajua unapokuja na Data za Kitaalamu alafu hizo Data zinakuwa zina utata au hazina uhakika unapelekea habari yako nzima kuonekana ni ya uongo Huyo Dr. Hizo data amezitoa wapi sababu kuna hizi data za huyu Mdau allegedly zimetoka WHO zinasema vinginevyo:-

Au huyu na Data zake ndio za uongo....

View: https://twitter.com/BusInsiderSSA/status/1697592548825436655?t=GX9Td4cB57EdXXp4_D4F3A&s=19
 
amesema kwa Wastani, kila Mtanzania anatumia lita 9.1 ya pombe kwa mwaka

Huu ni wastani tu...😁

Uhalisia ni kwamba kuna watu wasiokunywa kabisaaaaa, hivyo maana yake ni kuwa wale wanaokunywa wapo wanaotumia kiasi cha SIM tanks za lita 1000 au zaidi...
 
Hapo kwenye Kila mtanzania kumefanya nione huo utafiti ni uongo kabisa, kwamba hadi tusio kunywa pombe na sisi tumejuishwa kama wanywa pombe 🤔🤔 kwamba huyo mtafiti hakujua kama kuna watanzania wengi tusio kunywa pombe 🤔🤔
 
Wachaga ndio wamesababisha tuingie kwenye kumi bora.Ila nawasifia kitu kimoja tofauti na makabila mengine.Wanakunywa pombe lakini ni wachapakazi sana.
 
Hawa watu wanaleta utani na tungi,nimeishi Irnga,huko mtu kutumbua ulanzi au komoni kindoo Cha lita 10 ni kawaida tu sana tu,na hii ni kuanzia asbuhi Hadi mchana.Na hapo jioni ataenda sukutua mdomo na safari mbili tatu Ili kumaliza siku halafu mnaleta utafiti feki humu.
 
Back
Top Bottom