Daktari wa China akumbukwa nchini Tanzania kwa kujitoa muhanga kishujaa

Daktari wa China akumbukwa nchini Tanzania kwa kujitoa muhanga kishujaa

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
微信图片_20250625105950.png


Daktari wa ganzi wa China, Zhang Junqiao, aliwahi kusema kwamba "Bila kujali utaifa au rangi, ninachothamini zaidi ni maisha,"

Asubuhi ya siku ya Ijumaa, zaidi ya watu 300 walikusanyika huku kukiwa na kimya kizito katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, Tanzania, na kusimama bega kwa bega kumuaga Daktari Zhang, kiongozi wa timu ya 27 ya madaktari wa China nchini Tanzania, ambaye alipoteza maisha wakati akimuokoa mtu aliyezama.

Hafla ya kumuaga, iliyofanyika kwa heshima kubwa na mioyo mizito, ilimuenzi Zhang, ambaye picha yake ilizungukwa na maua meupe. Waombolezaji wengi walivaa fulana nyeupe zenye picha ya uso wake wenye tabasamu, huku wengine wakiinua fulana iliyojaa majina yaliyoandikwa kwa mkono -- ishara za shukrani na huzuni. Waombolezaji waliokuwa wakitiririkwa na machozi walinong'ona jina lake. "Alikuwa Mchina," muuguzi mmoja alisema. "Lakini kwetu sisi, alikuwa familia yetu."

Dokta Zhang alifariki Juni 15, Siku ya Baba Duniani, wakati akimwokoa mama aliyekuwa anazama huko kigamboni Dar es Salaam. Picha za walioshuhudia zilimuonesha akiwa amemshika mama huyo juu ya maji na kumpa jaketi lake la kuogelea, na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi lakini maji yalimzidi nguvu akazama na kupoteza maisha. Licha ya juhudi za wenzake kumuokoa, lakini Dokta Zhang hakuweza kufufuliwa.

Dokta Zhang, 38, anatoka Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China na alipangiwa kazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hospitali kuu ya rufaa nchini humo, tangu mwanzoni mwa mwaka 2024. Akiwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi, alizoea haraka kushughulikia mahitaji ya dharura ya hospitali hiyo, ambapo madaktari wasiopungua 20 wa dawa za Usingizi na Ganzi wanahudumia katika vyumba saba hadi vinane vya upasuaji.

Badala ya kujiwekea kikomo kwa kazi ya kimatibabu, Dokta Zhang alilenga katika kujenga uwezo. "Lazima nifundishe. Lazima niache kitu nyuma," Zhang aliwaambia madaktari wenzake.

Akitimiza ahadi yake, Dokta Zhang alianzisha programu za mafunzo ya vitendo kwa watumishi wa afya na wanafunzi wazawa. Alifundisha mbinu za hali ya juu kama vile kutafuta mishipa ya neva isiyoonekana kwa kutumia ultrasound, akitumia kielelezo cha kuiga, ambayo ni njia ya kwanza katika mafunzo ya hospitali hiyo. Akifanya kazi na Chama cha Madaktari wa Usingizi na Ganzi Tanzania, mafunzo yake yalipongezwa kwa thamani yake ya kiutendaji.

"Aliniongoza kwa utulivu nilipokuwa kwenye chumba changu cha upasuaji," alikumbuka Elick Mwakatungila, nesi kijana ambaye ni mtaalamu wa dawa za usingizi na ganzi. "Hakunifundisha tu jinsi ya kuifanya, bali alinifanya niamini kuwa naweza."

Licha ya vizuizi vya lugha, Zhang alipata njia za kuwasiliana, kwa kutumia michoro, ishara na kuonesha kwa mikono. Pia alipendekeza kielelezo cha mafunzo ya njia mbili ili kuwanoa wauguzi na mafundi wa kiwango cha juu.

"Alituletea maarifa na uchangamfu," alisema Daniel Munubi, kaimu mkuu wa dawa za usingizi na ganzi. "Alikuwa daraja kati ya madaktari wa mataifa mawili, daraja lililojengwa kwa uwajibikaji na moyo."

Kitendo cha kujitolea cha Dokta Zhang na kifo cha ghafla kiliibua majonzi makubwa kote Tanzania. Maelfu ya wanamtandao walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kutoa salamu za rambirambi.

"Tumempoteza daktari wa kweli. Alimuokoa mtu mwingine kwa mikono yake, "mmoja aliandika. "Hakuwa mtu anayetoka nchini kwetu, lakini alitoa maisha yake kwa ajili ya watu wetu."

Maoni mengine yalisomeka: "Tumempoteza daktari bingwa,".

Wakati wa hafla ya kumkumbuka Dokta Zhang iliyofanyika siku ya Ijumaa, mfanyakazi mwenzake mmoja aliorodhesha mbinu 16 za hali ya juu alizofundisha Dokta Zhang, ikiwa ni pamoja na kuweka katheta kwenye mshipa ya ndani ya shingoni kwa usaidizi wa picha ya ultrasound na mipira ya kupumulia. Dokta Zhang pia aliongoza mihadhara na ushauri wa vitendo, akijenga kile ambacho wenzake wa Tanzania sasa wanakiita "timu ya madaktari ambayo haiwezi kuondolewa."

Chapisho la mwisho la mtandao wa kijamii la Dokta Zhang lilieleza dhamira yake: "Kuhudumia watu hakuna mipaka. Kama daktari wa China, ninajivunia kuwafanya wenzangu wa Tanzania kuhisi nguvu ya nchi yetu na taaluma yetu."
 
Kifo ni kama vile wakati mwingine kinatoa onyo kali kikitaka kuchukua uhai wa mtu.. Usikiingiliee.. Hakitaki kuingiliwa... Kazi yake.. Yaani najiuliza Hili tukio Kiroho siyo Coincidence..
 
Watu kama hawa wana haki majina yao yatumike kama utambulisho wa mitaa , barabara ,au hata kitengo hapo muhimbili
 
Kazi ya Zhang ndo ikuonyeshe kuwa kuna watu wema kwente kila taifa.
Hii tabia ya kudai kuwa watu wa mataifa fulani wako hivi au wako vile haifai
 
Back
Top Bottom