BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Daktari wa Familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe, Prof.Harun Nyagori, ameongelea kifo cha Membe kilichotokea leo katika Hospitali ya Kairuki Jijini Dar es salaam ambapo amesema Membe amefariki kifo cha kawaida na kuwataka Watu wapuuze taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa ameuawa.
Dr. Haroun amesema “Dr.Membe amekuwa na afya zake njema katika miaka yote hakuwahi kuwa na ugonjwa wowote wa magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, presha hakuwahi kuwa nayo”
“Jana alipata homa ndogo ya kifua, akipata shida ya kukohoa na kubanwa kifua na ilipofika usiku wa kuamkia alfajiri ya leo alishindwa kupumua ghafla akakimbizwa Hospitali”
“Kwa kifupi maradhi haya yanatokana na virusi ambavyo vinazunguka vinaingia kwa njia ya hewa vinasababisha mgando kwenye mfumo wa mapafu, damu inakuwa nzito hiyo ndio imesababisha kifo cha Mh.Membe”
“Tuondoe mawazo potofu ambayo yamekuwa yakizungumzwa mtandaoni kwamba aidha ameuawa au amepewa sumu na vitu kama hivyo, amekufa kifo cha kawaida ambacho Mtu yoyote aidha Mimi au wewe kinaweza kumpata”