Ramea
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,146
- 4,084
Leo nililazimika kumsindikiza mke wangu hospital kupima mimba kwa ultrasound. Alipohudhuria clinic Mara ya mwisho nurse alisema mke wangu anaongezeka kilo kwa kasi sana, na Umri wa mimba hauendani na kimo/ukubwa wa tumbo. Yaani ndo kafunga mwez wa sita lakin mimba yake sawa na ya miezi 9. Tumbo kubwa kweli kweli.
Sasa Leo tukaenda kucheki kwa US majibu yakaja wife ana mapacha. Amesifia watoto wana afya nzuri na wanacheza vizuri(watundu kama Mimi baba yao) kisha akatoa hongera kwa wazazi, na kutuambia tarehe ya kujifungua. Kilichonifanya niandike Uzi huu ni kwamba, nilipomwuliza jinsia akajibu hawezi kusema hata Mungu hapendi. Ni haki kujibiwa hivi? Anakwepa nini au ni imani zake kidini au taaluma hairuhusu?