Daktari wa ultrasound amekataa kunambia jinsia ya vitoto vyangu

Daktari wa ultrasound amekataa kunambia jinsia ya vitoto vyangu

Ramea

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
2,146
Reaction score
4,084
Leo nililazimika kumsindikiza mke wangu hospital kupima mimba kwa ultrasound. Alipohudhuria clinic Mara ya mwisho nurse alisema mke wangu anaongezeka kilo kwa kasi sana, na Umri wa mimba hauendani na kimo/ukubwa wa tumbo. Yaani ndo kafunga mwez wa sita lakin mimba yake sawa na ya miezi 9. Tumbo kubwa kweli kweli.

Sasa Leo tukaenda kucheki kwa US majibu yakaja wife ana mapacha. Amesifia watoto wana afya nzuri na wanacheza vizuri(watundu kama Mimi baba yao) kisha akatoa hongera kwa wazazi, na kutuambia tarehe ya kujifungua. Kilichonifanya niandike Uzi huu ni kwamba, nilipomwuliza jinsia akajibu hawezi kusema hata Mungu hapendi. Ni haki kujibiwa hivi? Anakwepa nini au ni imani zake kidini au taaluma hairuhusu?
 
Taaluma haizuii huyo ana lake JAMBO. Kama huwezi kusubiri hadi siku ya kujifungua nendeni mahali pengine mkaangalie ila andaa ngawira za kutosha.
 
Taaluma haizuii huyo ana lake JAMBO. Kama huwezi kusubiri hadi siku ya kujifungua nendeni mahali pengine mkaangalie ila andaa ngawira za kutosha.
Ngawira!? Umeniacha kidogo hapo.
 
Leo nililazimika kumsindikiza mke wangu hospital kupima mimba kwa ultrasound. Alipohudhuria clinic Mara ya mwisho nurse alisema mke wangu anaongezeka kilo kwa kasi sana, na Umri wa mimba hauendani na kimo/ukubwa wa tumbo. Yaani ndo kafunga mwez wa sita lakin mimba yake sawa na ya miezi 9. Tumbo kubwa kweli kweli.

Sasa Leo tukaenda kucheki kwa US majibu yakaja wife ana mapacha. Amesifia watoto wana afya nzuri na wanacheza vizuri(watundu kama Mimi baba yao) kisha akatoa hongera kwa wazazi, na kutuambia tarehe ya kujifungua. Kilichonifanya niandike Uzi huu ni kwamba, nilipomwuliza jinsia akajibu hawezi kusema hata Mungu hapendi. Ni haki kujibiwa hivi? Anakwepa nini au ni imani zake kidini au taaluma hairuhusu?
Ina week Ngapi hiyo mimba?
Kwani kipimo kinaonyesha Jinsia kuanzia wiki 27 ya mimba
 
Doctor anasoma kwanza hulka yako je unapemda watoto jinsia ipi?
akigundua unapenda wakiume alafu tumboni yupo kwa kike hawezi kukwambia kwani utaanza kumnyanyapaa mama kijacho
 
Doctor anasoma kwanza hulka yako je unapemda watoto jinsia ipi?
akigundua unapenda wakiume alafu tumboni yupo kwa kike hawezi kukwambia kwani utaanza kumnyanyapaa mama kijacho
Dr. aliyetuhudumia hatufahamiani.
 
Dr. aliyetuhudumia hatufahamiani.

Hilo analijua kwa muda mchache tu sio lazima mfahamiane,
Mama kijacho wako si huwa anaenda hapo kila siku je hawafahamiani ?
Ulivyofika kupima hiyo us uliongea nini na doctor kabla ya kupima ?

Kuna wapo wanakuangalia hadi muonekano wako anajua wewe ni mtu unapenda nini..
Kama ni uzazi wa kwanza wanaume wengi wanapenda watoto wa kiume
 
MULTIPLE PREGNANCY MEANS MORE THAN ON CHILD. dr kisheria haruhusiwi kusema jinsia ya mtoto. pamoja kama akiwa single unaweza kuona au usione inategemea na mtoto amekaaje, kama amemgeukia mama sio rahisi kuona ila kama amegeuka kukuangalia ni rahisi ila taaluma hairuhusiwi. Naweza nikakuambia kimafumbo labda finger like structure au mouth like structure. hapo unaweza chambua mwenyewe.
Tuje kwenye Multiple pregnancy yani watoto zaidi ya wawili ni kuwa mara nyingi ni ngumu kwa sababu ya space yao inakua finyu haswa kuziangalia structure zao. hvyo ngumu kuweza kujua ila wengine kama ukaaji wao upo vizuri unaweza kuona. OVa.
 
Dah jamaa huyo Warthog kwe profile nkawaza unataka zaa vinguruwe nn ah ah hongera kwa watoto si vitoto mapacha
 
Mkuu mpeleke hospital za private mfano AGA KHAN, REGENCY etc. Nakushauri hivyo kwa sababu mke wangu alikuwa anaenda clinic katika hospital fulani hapa mjini Daslam akawa anapiaga ultrasound hizo na kupewa majibu kuwa mtoto yuko vizuri yupo katika njia yake. Hivyo asiwe na wasi wasi wowote. ila siku ya kujifungua nilishangaa na kusikitika sana waliposema kuwa mtoto hajakaa sawa katika njia yake. Pia wakatoa muongozo kuwa inabidi afanyiwe upasuaji. niliwamaindi sana. Ikabidi nijikakamue kisabuni nimpeleke pale AGA KHAN kwa huduma bora Zaidi. Nilipofika walisikiitika sana kuwa angechelewa angeweza kupoteza mtoto au yeye au wote kwa pamoja.

Take care.
 
Hilo analijua kwa muda mchache tu sio lazima mfahamiane,
Mama kijacho wako si huwa anaenda hapo kila siku je hawafahamiani ?
Ulivyofika kupima hiyo us uliongea nini na doctor kabla ya kupima ?

Kuna wapo wanakuangalia hadi muonekano wako anajua wewe ni mtu unapenda nini..
Kama ni uzazi wa kwanza wanaume wengi wanapenda watoto wa kiume
Sikuongea chochote na Dr kabla ya kupima. Ni kweli wife anahudhuria clinic hapo hapo ila jengo la clinic ya wazaz ni mbali kabisa na X ray, maabara na US. Pia wahudumu wake ni tofauti.
 
Je, wewe na mkeo kuna jinsia mnayopendelea na Dr. huyo anafahamu? Madaktari wetu wengi hawana ujuzi wa kutambua jinsia na hivyo kuona ni bora kutosema kuliko lawama baadae.
Pia, naomba ubadili kichwa cha uzi huu toka " dr-wa-ultrasound-amekataa-kunambia-jinsia-ya-vitoto-vyangu" kwenda " dr-wa-ultrasound-amekataa-kunambia-jinsia-ya-watoto-wetu"
 
Back
Top Bottom