Kaudunde Kautwange
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 1,644
- 1,648
Habari wana board..
Leo wakati Niko kwenye daladala toka Mbezi kwenda Simu2000 nilimsikia konda akitoa hii hoja.
Kwa maelezo yake ni kuwa kwa sasa ni magari ya mwendo kasi tuu ndio yanayo ruhusiwa kuchukua abira kutoka Mbezi, Kimara kwenda k.koo na Posta.
Daladala ambazo zilikuwa zinatumika kwa njia hiyo, kwa sasa zinatakiwa kuishia Ubungo.
Lakini kubwa zaidi ni hili, magari ya mwendo kazi hayabebi mzigo wa aina yoyote, sasa kama tujuavyo k.koo ni sehemu ambayo wafanyabiashara wengi wanaenda kuchukua bidhaa zao, hii kwa upanda Fulani itaongeza ugumu wa biashara kwa wafanyabiashara Hawa.
Lakini pia hata kwa wale wanaoenda Posta, yaani feri, Hawa pia watakutana na ugumu.
Baadhi ya watu wa daladala walienda Sumatra kulalamika, lakini jibu LA Sumatra ni kuwa na wao wamepewa order ya kufanya hivyo, ingawaje wanajua kuwa italeta changamoto kwa abiri.
Wakatoa ushauri kuwa, abiria na wadau wengine waandike barua ili wao wapate nguvu ya kupata sehemu ya kusimamia na kurudisha utaratibu wa awali.
Kumbuka, hizi ni tetesi, kama kuna mtu ana maelezo kamili tafadhali tujuze ili tuweze kulipinga Kwa pamoja.