Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wao ndio wenye mamlaka ya kuamua Leo ule au ulale njaa! Jiandae 2020aisee..hivi hao wanaotoa maagizo hayo tumewakosea nini.
Habari wana board..
Leo wakati Niko kwenye daladala toka Mbezi kwenda Simu2000 nilimsikia konda akitoa hii hoja.
Kwa maelezo yake ni kuwa kwa sasa ni magari ya mwendo kasi tuu ndio yanayo ruhusiwa kuchukua abira kutoka Mbezi, Kimara kwenda k.koo na Posta.
Daladala ambazo zilikuwa zinatumika kwa njia hiyo, kwa sasa zinatakiwa kuishia Ubungo.
Lakini kubwa zaidi ni hili, magari ya mwendo kazi hayabebi mzigo wa aina yoyote, sasa kama tujuavyo k.koo ni sehemu ambayo wafanyabiashara wengi wanaenda kuchukua bidhaa zao, hii kwa upanda Fulani itaongeza ugumu wa biashara kwa wafanyabiashara Hawa.
Lakini pia hata kwa wale wanaoenda Posta, yaani feri, Hawa pia watakutana na ugumu.
Baadhi ya watu wa daladala walienda Sumatra kulalamika, lakini jibu LA Sumatra ni kuwa na wao wamepewa order ya kufanya hivyo, ingawaje wanajua kuwa italeta changamoto kwa abiri.
Wakatoa ushauri kuwa, abiria na wadau wengine waandike barua ili wao wapate nguvu ya kupata sehemu ya kusimamia na kurudisha utaratibu wa awali.
Kumbuka, hizi ni tetesi, kama kuna mtu ana maelezo kamili tafadhali tujuze ili tuweze kulipinga Kwa pamoja.
Mbona zinajaza sana abilia na joto la hapa inakuwa kero hata maana ya mwendokasi inakuwa haipo tena..kazi kupumliana na kupata hewa chafu ya vkwapa vya watu
Kwani ukiwa na mzigo kama beg,au kifurushi cchako Mwendo kas huwa hawakubari eeee au tu kwa sabab hakuna nafas mle ndan?Na hayo ni moja ya masharti yaliyofikiwa kati ya serikali na hao wanaoendesha huo mradi,kuwa pasiwepo na ruti ya daladala ktk njia hiZo kinyume na hapo ni kukiuka mkataba na kutawafanya hao waendeshaji wa huo mradi kusitisha na kuidai fidia serikali kwa kuvunja makubaliano yao,KINACHOWEZA KUFANYIKA NI KUWASHAWISHI HAO WAENDESHAJI WA HUO MRADI KUKUBALI KUBEBA MIZIGO NA SIO KURUHUSU DALADALA NJIA HIZO.
Hivi kwa mfano mtu anatoka ubungo kwenda kigambon ukodi tax? Au. Unaongea tu?Taxi,Bajaji na Bododaba wale wapi?
Mie nawapongeza kwa kuikatisha route hii ili kipato kigawanyike.
Na nyie watu wa Mbezi na Kimara mmekuwa bahili kuliko wa Mbagala?alaaa
Kama unamzigo ukishuka chukua Bodaboda au taxi au Carry kabisaa na wao wapate
Kutoka wapi?,Ubungo?tutembee kwa miguu kkoo sio mbali
kusisitiza kwangu kua chanzo cha habar konda ni dharau????Ambaye ni mdau katika sekta ya usafiri wa daladala, hao madereva na makondakta wao hupata habari kwanza kabla ya kukufikia wewe msafiri.
Si vizuri kudharau ni vyema kama una shaka uangalie comment za uthibitisho.