Tetesi: Daladala route ya K.koo na Posta toka Mbezi na Kimara imezuiliwa

Mwendokasi wanalipa road licence bila usumbufu kwa hiyo lazima wapewe kipaumbele
 
Inaweza kuwa kweli ndiyo maana gari barabarani zilikuwa chache leo,maana hata gari za Simu2000 hazikuonekana,mie naishi Magomeni leo nimetoka home mapema sikutaka kupanda mwendokasi kufika stand gari hamna kabisa,gari zilizokuwa zinakuja ni za Mabibo na Makumbusho kupitia Shekilango.
 
Waongeze tu magari, loooh, tunaminyana hadi matumbo yanakaribia kupasuka;
ila ni kweli mizigo hairuhusiwi, watu wa feri sijui samaki wanabeba kwenye usafiri upi.
 
Waongeze tu magari, loooh, tunaminyana hadi matumbo yanakaribia kupasuka;
ila ni kweli mizigo hairuhusiwi, watu wa feri sijui samaki wanabeba kwenye usafiri upi.
mbona wanabeba kwenye mwendokasi...........utakutana na ndoo kibao .
 
Acha tuisome namba,haya ya mwendokasi yenyewe hayapo ya kutosha.
Mtu unakaa kituoni lisaa lizima amna daladala.
Na ukifanikiwa kulipanda hilo nyomi lake nilichogundua kumbe likijaza hewa yake ndani ni ndogo sana kweli mwendo kasi
 
Huo mzigo utaubeba kichwani ama
 
Waruhusu haya ya mwendo kasi yapakie mizigo tu aiseee.

Watatesa sana watu wanaochukua mizigo kariakoo na mnazi mmoja.
 
Yaani tunakaa sana stand likija Lipo nyomi hata kwa kusimama akuna
 
Sijui wanafikiri kwa kutumia nini hawa wakuu magari yenyewe machache hayo mnalazimisha vitu ambavyo havipo monopoly hadi kwenye usafiri mbona huku tuliko kuna mabasi ya mwendokasi,treni ya mwendo kasi,daladala,taxi meter,treni ya speed ya kawaida hakuna ataezuiliwa ni kukua kwa maendeleo na si kurudi nyuma...
 
Wakifanya hivo watakuwa hawajatundea haki walipa kodi wayaacha yote iwe chagua lako unataka upande lipi,au ya mwendo kasi wayafunge matela ya kuvutia mizigo sababu sio wote twaenda ofisini.
 
Nchi hii kila nikiitafakari nashindwa kuielewa. Hivi haya magari ya mwendo kasi yanatosha kubeba abairia wote wa ruti hiyo?

Watu wanakaa kituoni zaidi ya dk 40 na gari zenyewe zinakuwa zimejaa kupita maelezo hata nafasi ya kuweka miguu yote miwili wakati mwingine hakuna,halafu mzuie daladala,kweli????
 
Hiyo ruti ya kimara/Mbezi sasa itakuwa noma.
Kama hivi daladala za kawaida zipo bado hayo mabasi yanajaa itakuwaje zikizuiliwa?
 
source ya habar konda
Ambaye ni mdau katika sekta ya usafiri wa daladala, hao madereva na makondakta wao hupata habari kwanza kabla ya kukufikia wewe msafiri.
Si vizuri kudharau ni vyema kama una shaka uangalie comment za uthibitisho.
 
kama ni ukweli basi tuhamie kwenye treni ya mwakyembe tu hamna namna maana mwendokasi siku hizi ni mwendokero.
 
Hatunywi sumu hatujingiiii......mbele kwa mbele. Daaah! wakati wa kuimba waliimbia upande mmoja ila wakati wa kuyatumia kwa vitendo hayachagui upande wa kuuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…