Daladala za Masaki - Gerezani ni chafu, baadhi zina kunguni

Daladala za Masaki - Gerezani ni chafu, baadhi zina kunguni

Nina uhakika andiko langu hapa Jamii Forums linaweza kuwafikia watu wengi hasa wenye mamlaka ili ziweze kuchukua hatu.

Hapa Dar usafiri wa watu wengi ni Daladala, kina sisi ambao hatuna uwezo wa kununua magari usafiri huo ndio tunaoutegemea kwa kiasi kikubwa/

Kuna daladala zimekuwa na kawaida ya kuwa chafu kiasi kwamba inakera sana unapoingia kwa ajili ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Nakumbuka zamani trafiki wengi walikuwa wakiwakamata madereva na makonda na kuwakagua kuhusu usafi wa mavazi yao. Moja kati ya changamoto kubwa ni daladala za Masaki hadi Gerezani, zimekithiri kwa uchafu.

Nyingi kati ya zinazopiga ruti kwenye njia hizo zimechoka hatari hadi kufikia hatua hadi mnakuta kunguni kwenye daladala, hali ambayo inatia kinyaa sana.

Unaweza kukuta ipo siku kunguni anakuingia mwilini, unafika ofisini au nyumbani unamtoa mdufu huyo.
View attachment 2658333
Ngoja nije kupanda japo hata sijui nitakuwa naenda wapi ili nami nitalii na kuona wadudu hao wamba.
 
Yaani hizo biashara wacha kupiga kelele, hata upige nyuklia zitabaki hivyo hivyo kwa kuwa wenyewe ni hao hao trafik, latra na wala nchi
 
Mi naona tatizo ni RUSHWA, matraffic wamesimama balabalani kila siku!.. Na pia umoja wao (uwadar) kati ya majukumu yao ni haya na inabidi isimamiwe na mamlaka husika
 
Back
Top Bottom