A
Anonymous
Guest
Mwezi Aprili, LATRA ilipotangaza nauli mpya, ilieleza kuwa safari zisizozidi kilomita 10 zitatozwa Shilingi 700, huku safari zisizozidi kilomita 20 zikitozwa Shilingi 900.
Hata hivyo, kwa takribani wiki mbili sasa, daladala za njia ya Mbezi–Goba–Kawe zimekuwa zikitoza nauli ya Shilingi 1,000 bila kuzingatia kituo cha abiria wala nauli elekezi. Kwa kawaida, kutoka Kawe hadi Goba Centre ni Shilingi 700, na kutoka Kawe hadi Mbezi ni Shilingi 900.
Unapojaribu kuwauliza makonda kuhusu ongezeko hilo, baadhi yao huwa wakali na kusisitiza kuwa nauli hiyo hairuhusiwi kujadiliwa.
Je, LATRA imetangaza nauli mpya? Ikiwa hakuna mabadiliko rasmi, tunaomba mamlaka husika zichukue hatua na kuhakikisha abiria wanatozwa nauli zinazotambuliwa kisheria.