Dalai Lama kiongozi wa Tibet aliyekufa na kurudi mara 14

H
Hakuna kuzaliwa tena ukifa hizo ni nadharia tu
 
 
Jambo la kwanza
Mtu huyu kama siyo mtakatifu vya kutosha, yaani kama bado anayapenda sana mambo ya ulimwengu huu basi mtu huyo atazaliwa tena duniani.

Dalai Lama anarudi sana duniani akifa.. Ina manaa hakuwa mtakatifu?

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
dalai lama anaangukia kwenye kundi la tatu, ni wale watakatifu wanaorudi makusudi ili kutusaidia sisi tuweze kuufikia utakatifu wao kibuddha tunawaita boddhisatva
 
Hiyo imani ya kibudha dhana yao ya mtu akifa kuzaliwa tena au roho take kuchanganyika na roho nyingine sikubaliani mayo.
Kama ndio hivyo, mbona duniani roho za watu zinazidi kuongezeka, kwa mantiki hiyo idadi ya watu duniani, au wabudha wenye imani hiyo duniani ingetakiwa idadi yao usiongezeke kwa vile akitoka(akifa)mtu au mbudha, nafisi yake anazaliwa mtu mwigine.
 
roho wanazaliwa nazo wanadamu zingine zinatoka kwenye viumbe wengine, sisi wabuddha tunaamini kuwa mbwa anaweza kuzaliwa kama mwanadamu na mwanadamu anaweza kuzaliwa kama paka na kadhalika, kuhusu wanadamu kuongezeka niliwahi kumuuliza Monk mmoja mkubwa akanijibu kuwa Viumbe wa baharini wanapungua kwa kasi pia
 
Dalai lama anaheshimika sana rais wa United State of america
 
Kufa na kufufuka? Utapeli wa karne ya 1 huo. Sasa mbona amekimbia Tibet anaishi uhamishoni kama ana nguvu hizo anazosema? Si angewaangushia jumba bovu wachina?
 
Umeandika mtu asiyemsafi sana akifa roho yake huenda na kuingia kwa kiumbe kingine kitachozaliwa...

Je asili ya mwanadamu wa kwanza ni ipi?
 
Uhuni uhuni,uongo uongo na propaganda tu hakuna mtu aliyekufa aka exist upande wowote ule uwe duniani,Mbinguni,motoni nk
 
Sasa mbona watu wanaongezeka duniani? Kama ndivyo basi idadi ya watu isingeongezeka.
Dini kweli ni mzigo wa misumari
Yap ni kweli kabisa inafikirisha sana kungekuwa hakuna haja ya Uzazi wa mpango,kwa hiyo billgate wa corona atazaliwa maskini,"thinking loud'
 

Papa Ni Kiongozi Wa Wakatoliki Na Sio Wakristo Ebu Lekebisha Kauli;
 
Papa Ni Kiongozi Wa Wakatoliki Na Sio Wakristo Ebu Lekebisha Kauli;
Bosi soma vizuri post yangu Papa ni kiongozi mashuhuri Zaidi wa kikristo hata huyo Dalai Lama ni kiongozi wa dhehebu tu lakini bado anabaki kuwa kiongozi mashuhuri Zaidi wa kibuddha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…