Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Unashindwa kusema HAPANA kwa watu wengine kwasababu unawajali sana
Unaweza kulia ukiwa mwenyewe na hauwashiriki wengine mambo yako, kwasababu unahofu watakuonaje
Huwa unafikiri kila mtu unayekutana naye ni rafiki yako na kutaka kuwasaidia hata kama wako na wewe kwa mda mchache
Uko mkarimu sana kwa watu na unawakirimu vizuri,na unategemea kuwa watakuwa wakarimu kwako pia
Hauoni mapema pale watu wanapo kutumia kwa manufaa yao,kwasababu wewe huwezi kuwafanyia hivyo
Huwezi kuwahumiza watu wengine kwa makusudi kwasababu una moyo mzuri sana
Unajikuta kwako ni vigumu sana kuwaeleza watu wengine hisia zako bila kuguswa na hisia zako au kuumizwa na hisia hizo
Unaweza kugundua hata baadhi ya mambo madogo ambayo watu wanakufanyia lakini unashindwa kuyaongelea
Unajali sana kuhusu wengine kiasi kwamba unataka kujua au kuelewa shida zao na kutaka kuwasaidia
Unapenda kuwasaidia wengine kwa hofu ya kupoteza marafiki,lakini mwisho wa siku unaishia kuwa mpweke
Ni hayo tu!