Kama una presha usiende kupima mana waweza ukafa kabla hata majibu hayajaja.
Kweli mkuu. Mie nakumbuka kuna siku watu wa Benki ya Damu walikuja kanisani kwetu kuomba tuchangie damu, basi mie nikawa mmojawapo wa waliochangia damu. Wakatuambia kuwa kama unataka kupata majibu ya damu yako, unaruhusiwa kwenda Bugando huko kwenye benki ya damu utapewa majibu ya damu yako.
Mie nikaona isiwe tabu nikaenda.
Kilichofuatia hapo acha kabisa: Yule mtoa majibu akaniambia maneno ambayo siku sikiliza vizuri zaidi ya kusikia neno POSITIVE.
Nikajikuta makamasi yanatoka, machozi yanatoka. Basi akabaki ananishangaa. Akaniuliza kulikoni mbona unalia?
Nikamjibu "WEWE SI UMESEMA MIMI NI POSITIVE"
Hapo sasa nikaanza kulia kwa sauti kubwa, hadi wenzie wakaja pale kuuliza kuna nini?
Yule dada akawaambia wenzie kuwa "Huyu, nimemwambia kuwa DAMU YAKE NI GROUP
O POSITIVE, SASA NASHANGAA AMEPANIC"
😀😀😀😀😀😀😀 looooooh! hapo ndio nikashuka kidogo, nikamwambia mimi sikusikia kama umeongelea group la damu, nimekusikia tu ukisema mimi ni positive. hahahahahhah
Basi wakaniambia kuwa mimi niko FRESH kabisa sina ngoma, wakanipa kadi yao, wakaniomba niwe nachangia damu mara kwa mara.
KUPOKEA MAJIBU SIO MCHEZO aisee