Dalili mbili kuwa hatima yako ni kuwa Mtu Mkubwa na mkuu (Greatness)

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
10,002
Reaction score
16,240
First, You never fit in
Hujawahi kuendana na makundi au mifumo ya kawaida. Tofauti yako ndio alama ya ukuu wako.
Ukijiunga na watu kwa jambo lolote wenzio watakua hawakuelewi na wewe huwaelewi, fikra zako ziko mbele ya muda ndio sababu. wanayoyapenda wengine wewe sio habari hata kidogo,

Secondly;
You irritate people who don't love or hate to stand in front of a Great Man who is still in progress
Wasioweza kuhimili kuwa karibu na mtu mkuu wataweweseka sana,
Wasiopenda kuona wanazidiwa kwenye jambo lolote, hasa utendaji watakuchukia na kujaribu kutumia maneno ya mdomo kugeuza au kulazimisha kusema kuwa huwezi.
Lazima watataka kushindana nawe sana kujaribu kufuta nguvu yako isio onekana lakini hata hivo bila wewe kutumia nguvu nyingi unafanikisha yale ambayo kwao ni magumu au wanahitaji energy kubwa kupata.
Kwao ni ngumu lakini kwako ni rahisi, simple.
 
Ninakubaliana kwamba mtu anaweza kuwa tofauti na wengi, akawa na uwezo fulani wa kipekee, au akafikiri kwa namna ambayo si ya kawaida. Lakini ninapinga hitimisho kwamba hali hizo peke yake ni ushahidi wa “greatness.”

Kwanza, kutokufit katika kundi si ushahidi wa ukuu. Mtu anaweza kushindwa kuendana na kundi kwa sababu ya tabia, mawasiliano mabaya, ukosefu wa social skills, kiburi, kutokubali ushauri au tofauti ya personality. Kwa hiyo, kusema “huelewani na watu kwa sababu fikra zako ziko mbele ya muda” ni false cause; umeona matokeo lakini ume-assume sababu bila ushahidi.

Pili, kuwa tofauti si sawa na kuwa bora. Watu wengi hawapendi vitu vinavyopendwa na wengine, wana mitazamo tofauti au wanaishi kwa namna tofauti. Hiyo inathibitisha individuality, si greatness. Ili kudai superiority, lazima kuwe na kipimo kinachoonyesha superiority hiyo.

Tatu, hoja ya kwamba “unawakwaza watu wasioweza kusimama mbele ya Great Man” ina tatizo kubwa la kimantiki. Unachukuliwa tayari kuwa Great Man, halafu reaction ya watu inatumika kuthibitisha kwamba wewe ni Great Man. Hii ni circular reasoning. Kwa lugha rahisi: unasema wewe ni mkubwa, halafu unatumia watu kukukataa kama ushahidi kwamba wewe ni mkubwa.

Nne, kuna confirmation bias. Mtu akisoma andiko hili, karibu kila hali anayopitia anaweza kuitafsiri kama ushahidi wa greatness. Akipingwa, “wanakuogopa”; asipoeleweka, “fikra zako ziko mbele”; akichukiwa, “wanakuonea wivu”; akifanya vizuri, “unaona, nilijua mimi ni tofauti.” Mfumo huu hauachi nafasi ya kuuliza kama tatizo linaweza kuwa limetokana na yeye mwenyewe.

Tano, hoja hii ina self-serving bias. Mtu anachagua tafsiri inayoinua thamani yake binafsi na kupuuza tafsiri nyingine zinazoweza kuwa na maana zaidi. Kwa mfano, mtu akikukosoa, badala ya kujiuliza kama criticism yake ina ukweli, unahitimisha kwamba anajaribu kupunguza nguvu yako.

Sita, kusema “watu wanakuchukia kwa sababu hawapendi kuona unawazidi” ni mind reading. Huwezi kujua motivation ya mtu bila ushahidi. Mtu anaweza kukupinga kwa sababu amegundua kosa lako, hakubaliani na mtazamo wako, au kwa sababu tu ana interests tofauti. Si kila opposition ni envy.

Saba, kauli kwamba “kwako ni rahisi lakini kwao ni ngumu” nayo si ushahidi wa greatness. Inaweza kutokana na uzoefu, kipaji, maarifa, mazoezi, mazingira au specialization. Mtu kuwa bora katika jambo moja hakumfanyi moja kwa moja kuwa superior kwa ujumla.

Nane, andiko linatumia hasty generalization. Linafanya generalization kubwa kuhusu watu na greatness kutokana na experiences chache ambazo zinaweza kumpata karibu mtu yeyote. Karibu kila mtu amewahi kutokuelewana na watu, kukosolewa, kuchukiwa, kuwa tofauti au kufanya jambo ambalo wengine waliona ni gumu. Kama hayo ndiyo vigezo vya greatness, basi definition yenyewe inakuwa haina discriminatory power.

Tisa, kuna false dichotomy: ama watu wanakuelewa kwa sababu wewe ni wa kawaida, au hawakuelewi kwa sababu wewe ni mkubwa. Kuna possibilities nyingi katikati. Unaweza kuwa sahihi, unaweza kuwa umekosea, unaweza kuwa na wazo zuri lakini ukalieleza vibaya, au unaweza kuwa mbele katika jambo fulani na nyuma katika jambo jingine.

Greatness haiwezi kuthibitishwa na namna mtu anavyojisikia kuhusu yeye mwenyewe au namna anavyotafsiri reactions za watu wengine. Greatness inahitaji evidence: competence, consistency, discipline, measurable results, character na impact. Mtu anaweza kuwa tofauti bila kuwa mkubwa; anaweza kukataliwa bila kuwa genius; anaweza kukosolewa bila kuwa victim; na anaweza kuwa na uwezo bila kuhitaji kujenga narrative kwamba kila anayempinga ana wivu.

Kwa hiyo, tatizo la msingi la andiko lako si kwamba kila kitu kilichoandikwa ni uongo. Tatizo ni kwamba experiences za kawaida zimepewa interpretation ya kipekee na kuwasilishwa kama ushahidi wa greatness bila establishing the necessary evidence. Hiyo ni motivational psychology, si proof ya greatness.
 
Tuangalie mifano hai ya watu kimaisha kuthibitisha hoja Zangu,
We say, "Every champion, one day feels like quitting

Uliza wasanii wakubwa, Wacheza mpira kama Messi, watakwambia walipitia kwanza hali ya kuonekana hawajui chochote.
Kwenye vitabu vya dini sasa ndio balaa, nikiaanza kuweka shuhuda hizo hapa simalizi, Naanza na Prophet Mohamed mwenyewe mwanzo alionekana boya kumbe ni Mtu mkubwa.
 
unachanganya mambo mawili: kupitia kipindi kigumu si sawa na kuwa Great.
Messi kukataliwa au kuonekana hafai mwanzoni hakuthibitishi kwamba kila anayekataliwa ni Messi wa kesho. Mwanzo mgumu unaweza kuwa sehemu ya safari ya greatness, lakini si kila anayepitia mwanzo huo anafikia greatness.
 
Kufika au kutokufika sasa hiyo ni mada nyingine.
Ndio maana unaambiwa Makaburini ndio sehemu imejaa utajiri.
 
First, You never fit in
Hujawahi kuendana na makundi au mifumo ya kawaida. Tofauti yako ndio alama ya ukuu wako.
Ukijiunga na watu kwa jambo lolote wenzio watakua hakuelewi na wewe huwaelewi, fikra zako ziko mbele ya muda ndio sababu. wanayoyapenda wengine wewe sio habari hata kidogo,

Secondly;
You irritate people who don't love or hate to stand in front of a Great Man who is still in progress
Wasioweza kuhimili kuwa karibu na mtu mkuu wataweweseka sana,
Wasiopenda kuona wanazidiwa kwenye jambo lolote, hasa utendaji watakuchukia na kujaribu kutumia maneno ya mdomo kugeuza au kulazimisha kusema kuwa huwezi.
Lazima watataka kushinda nawe sana kujaribu kufuta nguvu yako isio onekana lakini hata hivo bila wewe kutumia nguvu nyingi unafanikisha yale ambayo kwao ni magumu au wanahitaji energy kubwa kupata.
Kwao ni ngumu lakini kwako ni rahisi, simple.
Hongera Mkuu Kwa Uzi nzuri sana, ila naona hujautendea haki, umeandika Kwa Kifupi sana, na nikisoma maelezo Yako, naona ulikua na uwezo wa kujazia Nyama Uzi wako.
 
Unapata unachoshawishi mtu mkubwa ni yule anayeweza kuishi na kila mtu awe kichaa au genius
 
Back
Top Bottom