Dalili saba zinazoonyesha kwamba wewe ni mtu wa maana au mwenye thamani

Dalili saba zinazoonyesha kwamba wewe ni mtu wa maana au mwenye thamani

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Mosi,unajua unaweza usikubaliane na watu baadhi ya mambo bila kuvunjiana heshima,na unaweza usikubaliane nao bila kupandisha sauti yako. Naam pamoja na kutokubaliana na watu katika baadhi ya mambo lakini haikupi sababu ya kuwavunjia watu heshima yao.

Pili,unaweza kuhudhuria sehemu kwa muda muafaka na kuondoka kwa mda muafaka mpaka watu wakujue kuwa wewe unaenda na mda,naam wengi wetu hakika hatuthamini mda kabisa yani kama tumejiwekea kautaratibu fulani hivi,shughuli saa moja jioni watu wanakuja saa saa mbili au saa tatu

Tatu,hauwajaji watu kwa muonekano wao,wala kwa kutoa maoni yao na unajua haupaswi kuwa katika mazungumzo ya kuwasema watu

Nne,unatambua kwamba unahitaji kuwapa watu moyo ili wafanye vizuri zaidi,na unajua kwa kufanya hivyo unakuwa mtu bora zaidi, naam usiwe mtu wa kukatisha tamaa watu,wape moyo hata kama machoni mwako unaona jambo hilo ni gumu,wakati mwingine tunachohitaji ni kusapotiwa kidogo tu

Tano, upo tayari kusimama imara kwa ajili ya watu wako hata kama hawapo hapo karibu,na ongea vizur kuhusu watu wako hata kama hawapo hapo.

Sita,unatambua kwamba ingawa unaona mambo mengi,lakini unaweza kuchagua kutosema au kuchangia chochote,si kila ukionacho au unachokijua lazima usema wakati mwingine piga kimya,si kila mjadala uchangie wakati mwingine unapita kimya

Saba, unaacha kuboreka au haukubali kuboreka kwasababu tu watu wengine wana kwambia hauwezi kufanya jambo fulani,kwasababu unaelewa kwamba huo ni mtizamo wao ni si wako,wakati mwingine watu wanaweza kukwambia mambo ambayo kwakuwa wao wameshindwa basi wataona nawe utashindwa,elewa kwamba hilo ni tatizo lao na si lako

Ni hayo tu!
 
Duh, tabia za malaika hizi
Wala hizi 90 % ni tabia za kurithi kutoka kwa wazazi na SIBLINGS Wanaokuzunguka
Ndo maana kuna vitu ukisikia vimetokea basi moja kwa moja utasikia ni WACHAGA hawa ndo tabia zao au WAZARAMO hao mdomo kwao ndo kwenyewe
Nature tu watu wa mara ni wajasiri
Ukipata mbena wa IRINGA umepata mke haswa
ukioa MTANGA juwa kwa mapishi ndo kwenyewe
Ukioa MNYAKYUSA utapendwa sana ila usiwe Mnyonge ni wababe
Ukitaka Uaminifu katika BIASHARA jinasibishe na wapemba au wanzanzibari

Hvyo hizo mambo zinarithiwa kutoka kiazi hadi kizazi
Jitahidi na wewe kuwarithisha watoto wako TABIA njema
 
Mie ya kwanza natofautiana kidogo ila mengine yote ndio nilivyoo
Hili kwangu limekuwa kawaida sana
Enzi za uvulana mpk ujanani wangu marafiki zangu wengi tulijuana kwenye ugomvi mkubwa baada ya hapo ni marafiki kutokana na vike nilivyoreact lkn kwa dunia ya sasa ya utafutaji haswa kma mfanyabiashara
Ukiendekeza hili litathili biashara zako mana kuna watu bila na wewe kuziregeza nati ukalichezesha DISHI kidogo hamuwezi kwenda sawa
Kuna watu wana kusudi zaidi ya kukela
 
Wala hizi 90 % ni tabia za kurithi kutoka kwa wazazi na SIBLINGS Wanaokuzunguka
Ndo maana kuna vitu ukisikia vimetokea basi moja kwa moja utasikia ni WACHAGA hawa ndo tabia zao au WAZARAMO hao mdomo kwao ndo kwenyewe
Nature tu watu wa mara no wajasiri
Ukipata mbena wa IRINGA umepata
Haswa ukioa MTANGA juwa kwa mapishi ndo kwenyewe
Ukioa MNYAKYUSA utapendwa sana ila usiwe Mnyonge no wababe
Ukitaka Uaminifu katika BIASHARA jinasibishe na wapemba aua wanzanzibari

Hvyo hizo mambo zinarithiwa kutoka kiazi hadi kizazi
Jitahidi na wewe kuwarithisha watoto wako TABIA njema
Nimeipenda hii boss,yani iko hivyo tunarithishana ama ujinga au ustaarabu itategemea na jamii uliyo nayo
 
Hili kwangu limekuwa kawaida sana
Enzi za uvulana mpk ujanani wangu marafiki zangu wengi tulijuana kwenye ugomvi mkubwa baada ya hapo ni marafiki kutokana na vike nilivyoreact lkn kwa dunia ya sasa ya utafutaji haswa kma mfanyabiashara
Ukiendekeza hili litathili biashara zako mana kuna watu bila na wewe kuziregeza nati ukalichezesha DISHI kidogo hamuwezi kwenda sawa
Kuna watu wana kusudi zaidi ya kukela
Ni sahihi kabisa wakati mwingine ni bora kujishusha ili mambo yako yanyooke na ndio kujielewa huko,malegend wanalijua hili
 
Nimeipenda hii boss,yani iko hivyo tunarithishana ama ujinga au ustaarabu itategemea na jamii uliyo nayo
Ni kawaida kukuta muhindi au mwarabu anaendesha biashara amaboyo yeye ni kizazi cha tatu au cha nne ni kawaida utakuta biashara ina hata FIVE DECADE kwann inaendelea 7bu wanarithisha maarifa sio upuuzi

Sio kama sisi wamatumbi utakuta watu wanalalama Mfanyabiashara fulani wa kanda ziwa kafa na utajiri umepotea 7bu ya ukanjanja na tunarithishana ujinga ujinga
 
Ni kweli kabisa,mfano wahindi utakuta mtoto akitoka shule lazima atapitia dukani walau hata kwa mda mchache apate uzoefu,na ndio maana wanakuwa vizur katika biashara,na kwa ujumla huwa wanasapotiana sana

Ila sisi sasa ukienda kumuomba mtu ramani anaona utafaidi sana,yani hatuko kunyanyuana wala kusaidiana,ni utaratibu wa kipuuzi sana
 
Back
Top Bottom