Dalili za kujinyonga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tambua Dalili za kujinyonga

Police Tabora yatangaza kuwasaka wanaotegemea kujinyonga. Zifuatazo ni baadhi ya viashiria vya anayetaka kujinyonga

1. Kuzungumza kuhusu kujinyonga
2. Kujitengatenga na kukaa pekeyako pekeyako
3. Kuwa na mood isiyotabirika leo uko vizuri kesho vibaya mno
4. Kuwa na mawazo yanayohusu kufa muda mwingi
5. Kujisikia huna tumaini lolote
6. Kunywa pombe kupita kawaida
7. Kuwaaga watu kama vile hamtakutana tena
8. Kuwa mkali kwa kitu kidogo tu
9. Kuongea pekeyako pekeyako
NB: Tumsaidie RPC Tabora Dalili za wanategemea kujinyonga mwaka huu ili kuokoa maisha

Jr[emoji769]
 
Dalili kuu ambazo unaweza kumgundua mtu anayetaka kujiua ni, kwanza kabisa kujitenga sana na watu, mtu kama huyu anapenda sana kukaa peke yake japo kwenye hili sio wote wanaopenda kujitenga wana hatari ya kufikia maamuzi hayo magumu.

Kiashiria kingine ni mtu kulizungumzia sana suala la kujiua, mfano mtu hutumia maneno kama ‘natamani kujiua, au mkiskia nimekufa msishangae’



Jr[emoji769]
 
Kujiua (Suicide) ni mojawapo ya vyanzo vya kifo kwa watu wenye matatizo ya kisaikolojia au matatizo ya akili. Jaribio la kujiua kwa mfano kunywa sumu au kujinyonganga ni mojawapo ya dalili inayoonyesha kua mtu huyo ana tatizo la kisaikolojia au tatizo la akili.

Watu wengi wanaojiua huonyesha dalili ambazo huashiria kutokea kwa hatua hii ya kujinyonga. Ikitokea wewe, ndugu au jamaa yako amejaribu kujiua, yawezekana ikawa ni kiashiria kua mtu huyu yupo katika hatari ya kupata ugonjwa wa akili au matatizo ya kisaikolojia.

Ni vizuri ukampeleka hospitali akapatiwa uchunguzi na msaada wa kisaikolojia kutoka kwa wataalamu wa afya na magonjwa ya akili.
Tafiti zinaonyesha kua endapo mtu ana mawazo ya kutaka kujiua, au alishawahi kujaribu kijiua, uwezekano mkubwa ni kua siku moja atafanikiwa kujiua kweli. Hivyo natibabu ni muhimu.

VICHOCHEZI (RISK FACTORS) ZA MTU KUTAKA KUJIUA

mambo yanayochangia mtu kutaka kujiua ni
• Magonjwa ya sonona (huzuni iliyopitiliza, kujiona mwenye hatia n.k)
• Magonjwa ya hofu (kuwa na hofu ilopitiliza pamoja na dalili zinazoambatana)
• Psychosis – hali ya kuona vitu ambavyo watu wengine hawavioni, kusikia sauti ambazo watu wengine hawazisikii na kua na mkanganyiko wa mawazo na hisia.
• Matumizi sugu ya madawa ya kulevya na pombe – matumizi mabaya ya pombe, bangi, cocain, heroin nk,yanahusiana sana na sonona, magonjwa ya hofu na kutaka kujiua.

UTAMJUAJE MTU ALIYEPO KATIKA HATARI YA KUJIUA?

Japo sio wote, watu wengi wanaotaka kujiua hutoa viashiria vifuatavyo
• Huonyesha hali ya husuni na kukata tama
• Hujiona mwenye hatia and aibu kwa mambo yaliyopita

• Alishawahi kujaribu kujiua siku zilizopita

• Hali ya kutawaliwa na mawazo kuhusu kifo
• Anaweza kua anatoa wosia au kuwaasa watoto au wengine kugawa vitu vyake n.k

• Mabadiliko ya ghafla katika hali ya kujijali
• Mabadiliko katika hamu ya kula na usingizi

• Kufeli shule kwa kiasi kikubwa sana na kua na dalili za kukata tamaa

• Kutoona umuhimu wa maisha ya baadae
• Kuandika au kuzungumzia kutaka kujiua..(epuka kusema anatania endapo ana dalili nyingine isiyo ya kawaida)

UFANYE NINI ENDAPO RAFIKI AU NDUGU ANA DALILI ZA KUTAKA KUJIUA AU AMEJARIBU KUJIUA

kama unadhani ndugu yako ana hatari ya kutaka kujiua, mpeleke hospitali na muelekeze daktari. Ongea nae bula kumjaji na kuonyesha lengo la kutaka kumsaidia. Ikiwa umemkuta akiwa anajaribu kujiua, hii ni emergence sawa na ajali, muwahishe hospitali, apewe huduma na kasha aonane na msaikolojia au daktari wa afya na magonjwa ya akili kwa matibabu. Unaweza pia kupiga namba 0754 8366 59 kwa msaada na maelezo ya nini cha kufanya na wapi pa kupata msaada wa haraka.

IKIWA AMESHAJARIBU KUJIUA NA MMEMUOKOA,

psychiatrist or clinical psychologist watakusaidia kumpa msaada wa kuweza kupona na kuondokana na hali hiyo. Usikae nae nyumbani, mara nyingi mtu aliyejaribu kujiua na kama ameamua kujiua hutoweza kumzuia bila msaada wa kitaalam.
Hakikisha hamumuachi peke yake hadi atakapopata msaada wa kitaalamu
Hakikisha hana access ya kitu au vitu anavyoweza kutumia kujiua
Muonyeshe upendo, kumjali na epuka kumkaripia, kumsema au kumtisha

KAMA UNA MAWAZO YA KUTAKA KUJIUA

ni muhimu sana kukumbuka kua mawazo kuhusu kutaka kujiua au kujidhuru ni mawazo tu na hayamaanishi kua kweli ujiue. Ili kupata msaada jinsi ya kuondokana na mawazo haya kabisa,
• Nenda hospitali, mweleze daktari wako au psychiatrist au Msaikolojia tiba (clinical psychologist) kama una dalili nyingine kama dalili za sonona au tatizo linguine la kisaikolojia au afya ya akili, matibabu na dawa huondoa kabisa hali hiyo
• Tafuta watu unaoweza kuongea nae. Omba msaada wa matibabu,. Ikiwa hujui pa kupata msaada, piga namba 0754836659 au tuma ujumbe.
• Kumbuka hutakiwi kufuata mawazo hayo ya kutaka kujiua, yatapita baada ya muda

WAPI PA KUPATA MSAADA

• Hospitali(hasa hasa kitengo cha afya ya akili au Psychotherapy centres kama zipo
• Kwa msaada. +255 712 748 758 /0754836659
• Hospitali iliyopo jirani nawe watakupa rufaa na maelezo
KUMBUKA
• Suicide au kutaka kujiua ni chanzo kinachoongoza kusababisha vifo kwa watu wenye matatizo ya kisaikolojia na magonjwa ya akili.
• Sonona ni chanzo kikubwa cha kusababisha mtu kutaka kujiua
• Mawazo kuhusu kutaka kujiua au kujidhuru ni mawazo tu na hayamaanishi kua kweli ujiue




Jr[emoji769]
 
wanaofikiria kujiua huwa hawataki kufikiria mambo ya mbele, hata kwa mambo ambayo tayari waliyapanga huwa wanaahirisha bila sababu ya msingi na wengine huwa wanaahirisha hata safari muhimu.

Modesta, ambaye ni mwalimu wa Chuo cha Elimu cha Patandi, tawi la Tanga anasema watu wanaofikiria kujiua pia huwa wanapenda kuahirisha mambo kwa sababu ya hasira ambazo zimetokana na uchungu uliosababishwa na watu, vitu au mazingira.

“Mtu anafikiria niwekeze kwa ajili ya nani, kinachomfanya kuahirisha mipango yake au uwezekaji si yeye ila ni uchungu kwa sababu anaamini kuwa jamii ndiyo imemjeruhi,” anasema Modesta.

Ukiwa na mtu wa aina hii hutakiwi kumuacha mwenyewe, badala yake unatakiwa kuwa naye karibu huku ukimpa maneno ya faraja.

Jr[emoji769]
 
Mkuu, huyo Bw Rpc wa Tabora amenishangaza sana baada ya kusikia kauli yake, yaani jeshi letu hili la polisi ambalo huwa linashindwa kukamilisha kesi ambazo ushahidi wake unakuwa wazi, leo hii wanataka kutuambia kwamba wanaweza eti kumkamata na kumfungulia mashtaka mtu anayetaraajia kujinyonga, maajabu ya 2020
 
Wewe unakuta mtu amekamatwa na kiganja cha mkono wa albino, halafu jeshi la polisi wanafungua mashitaka eti wanaandika Mtuhumiwa amekutwa na kitu kinachodhaniwa kuwa kiganja cha binadamu, hapa unaona kuna kesi kweli, si inakuwa imeisha kabla haijaanza.
 
Alikuwa na point ila alikosea kuiwakilisha.. Na hii ni shida ya wengi... Kukariri maarifa.. Kawaomba na watumishi wa kiroho pia wasaidie bado kayumba alikuwa hana hakika anataka ku deliver nini hasa Msikilize hapa asije kusema alinukuliwa vibaya.... [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Your browser is not able to display this video.


Jr[emoji769]
 
Lakini pia, hivi ni kwanini unataka kumshitaki mtu anaetaka kujiua mwenyewe ?, kwani anaua mtu ?, kwani mnamdai ? anawapunguzia nini nyinyi kama serikali ?, hii serikali ya awamu hii imesababisha watu wengi wanakosa matumaini na hivyo kuona bora kufa, nashauri wawaache tu watu wafanye wanalopenda kufanya, maisha hapa bongo hayafai, kama rais mwenye anawataka watu waishi kama mashetani, nani anataka kuwa shetani ?.
 
[emoji1][emoji1][emoji1]mtu kachinjwa na kisu na kipo pembeni yake.. Wanasema kakatwa na kitu chenye ncha kali
Jr[emoji769]
 
[emoji1][emoji1][emoji1]mtu kachinjwa na kisu na kipo pembeni yake.. Wanasema kakatwa na kitu chenye ncha kali

Jr[emoji769]
Mtu anauwa kwa kupigwa risasi na maganda ya risasi yakutwa eneo la tukio wanasema ameuwa ni kiti kinachodhaniwa kuwa ni bunduki,
Kule Iringa polisi hawahawa walimuua Mwangosi kwa bomu halafu wakasema ameuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa silaha !!
 
Hahahahahaha dah ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu hii ya 5 unaweza ukawa chizi usijijue kama umeshakuwa chizi mpaka hapo utakapoona watu wanakuvizia na kamba ndio utagundua hauko timamu
Nakumbuka kuna mtu aliwahi kusema wakati tunaanza 2016 kwamba kufikia 2020 kutakuwa idadi kubwa sna ya wagonjwa wa Presha, Kisukari na pia watu wanajiua, yanatimia jadidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…