Kujiua (Suicide) ni mojawapo ya vyanzo vya kifo kwa watu wenye matatizo ya kisaikolojia au matatizo ya akili. Jaribio la kujiua kwa mfano kunywa sumu au kujinyonganga ni mojawapo ya dalili inayoonyesha kua mtu huyo ana tatizo la kisaikolojia au tatizo la akili.
Watu wengi wanaojiua huonyesha dalili ambazo huashiria kutokea kwa hatua hii ya kujinyonga. Ikitokea wewe, ndugu au jamaa yako amejaribu kujiua, yawezekana ikawa ni kiashiria kua mtu huyu yupo katika hatari ya kupata ugonjwa wa akili au matatizo ya kisaikolojia.
Ni vizuri ukampeleka hospitali akapatiwa uchunguzi na msaada wa kisaikolojia kutoka kwa wataalamu wa afya na magonjwa ya akili.
Tafiti zinaonyesha kua endapo mtu ana mawazo ya kutaka kujiua, au alishawahi kujaribu kijiua, uwezekano mkubwa ni kua siku moja atafanikiwa kujiua kweli. Hivyo natibabu ni muhimu.
VICHOCHEZI (RISK FACTORS) ZA MTU KUTAKA KUJIUA
mambo yanayochangia mtu kutaka kujiua ni
• Magonjwa ya sonona (huzuni iliyopitiliza, kujiona mwenye hatia n.k)
• Magonjwa ya hofu (kuwa na hofu ilopitiliza pamoja na dalili zinazoambatana)
• Psychosis – hali ya kuona vitu ambavyo watu wengine hawavioni, kusikia sauti ambazo watu wengine hawazisikii na kua na mkanganyiko wa mawazo na hisia.
• Matumizi sugu ya madawa ya kulevya na pombe – matumizi mabaya ya pombe, bangi, cocain, heroin nk,yanahusiana sana na sonona, magonjwa ya hofu na kutaka kujiua.
UTAMJUAJE MTU ALIYEPO KATIKA HATARI YA KUJIUA?
Japo sio wote, watu wengi wanaotaka kujiua hutoa viashiria vifuatavyo
• Huonyesha hali ya husuni na kukata tama
• Hujiona mwenye hatia and aibu kwa mambo yaliyopita
•
• Alishawahi kujaribu kujiua siku zilizopita
•
• Hali ya kutawaliwa na mawazo kuhusu kifo
• Anaweza kua anatoa wosia au kuwaasa watoto au wengine kugawa vitu vyake n.k
•
• Mabadiliko ya ghafla katika hali ya kujijali
• Mabadiliko katika hamu ya kula na usingizi
•
• Kufeli shule kwa kiasi kikubwa sana na kua na dalili za kukata tamaa
•
• Kutoona umuhimu wa maisha ya baadae
• Kuandika au kuzungumzia kutaka kujiua..(epuka kusema anatania endapo ana dalili nyingine isiyo ya kawaida)
•
UFANYE NINI ENDAPO RAFIKI AU NDUGU ANA DALILI ZA KUTAKA KUJIUA AU AMEJARIBU KUJIUA
kama unadhani ndugu yako ana hatari ya kutaka kujiua, mpeleke hospitali na muelekeze daktari. Ongea nae bula kumjaji na kuonyesha lengo la kutaka kumsaidia. Ikiwa umemkuta akiwa anajaribu kujiua, hii ni emergence sawa na ajali, muwahishe hospitali, apewe huduma na kasha aonane na msaikolojia au daktari wa afya na magonjwa ya akili kwa matibabu. Unaweza pia kupiga namba 0754 8366 59 kwa msaada na maelezo ya nini cha kufanya na wapi pa kupata msaada wa haraka.
IKIWA AMESHAJARIBU KUJIUA NA MMEMUOKOA,
psychiatrist or clinical psychologist watakusaidia kumpa msaada wa kuweza kupona na kuondokana na hali hiyo. Usikae nae nyumbani, mara nyingi mtu aliyejaribu kujiua na kama ameamua kujiua hutoweza kumzuia bila msaada wa kitaalam.
Hakikisha hamumuachi peke yake hadi atakapopata msaada wa kitaalamu
Hakikisha hana access ya kitu au vitu anavyoweza kutumia kujiua
Muonyeshe upendo, kumjali na epuka kumkaripia, kumsema au kumtisha
KAMA UNA MAWAZO YA KUTAKA KUJIUA
ni muhimu sana kukumbuka kua mawazo kuhusu kutaka kujiua au kujidhuru ni mawazo tu na hayamaanishi kua kweli ujiue. Ili kupata msaada jinsi ya kuondokana na mawazo haya kabisa,
• Nenda hospitali, mweleze daktari wako au psychiatrist au Msaikolojia tiba (clinical psychologist) kama una dalili nyingine kama dalili za sonona au tatizo linguine la kisaikolojia au afya ya akili, matibabu na dawa huondoa kabisa hali hiyo
• Tafuta watu unaoweza kuongea nae. Omba msaada wa matibabu,. Ikiwa hujui pa kupata msaada, piga namba 0754836659 au tuma ujumbe.
• Kumbuka hutakiwi kufuata mawazo hayo ya kutaka kujiua, yatapita baada ya muda
WAPI PA KUPATA MSAADA
• Hospitali(hasa hasa kitengo cha afya ya akili au Psychotherapy centres kama zipo
• Kwa msaada. +255 712 748 758 /0754836659
• Hospitali iliyopo jirani nawe watakupa rufaa na maelezo
KUMBUKA
• Suicide au kutaka kujiua ni chanzo kinachoongoza kusababisha vifo kwa watu wenye matatizo ya kisaikolojia na magonjwa ya akili.
• Sonona ni chanzo kikubwa cha kusababisha mtu kutaka kujiua
• Mawazo kuhusu kutaka kujiua au kujidhuru ni mawazo tu na hayamaanishi kua kweli ujiue
Jr[emoji769]