Dalili za kupotea kwa sanaa ya uchoraji kutokana na matumizi ya IA (Artificial Intelligence)

Dalili za kupotea kwa sanaa ya uchoraji kutokana na matumizi ya IA (Artificial Intelligence)

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Matumizi ya AI yameshika kasi, uwezo wa program hizi kutengeneza picha kutokana na maono au mawazo ya mtumiaji, kumeongeza wimbi kubwa la picha hizo zikitumika katika maeneo tofauti.

Wasi wasi wangu ni kwamba itafika wakati hakutokuwa na haja ya kuwa na wachoraji wa picha, kwasababu program hizi zinaweza kutafsiri mawazo ya mtu na kutengeneza kitu au picha ambayo inaendana na matakwa ya mtumiaji.

Program hizi zitaeneza uvivu wa kutumia muda mrefu kuchora au kubuni picha, picha za wachoraji zitakosa soko kwani kila mtu anaweza tengeneza picha anayo taka akiwa amekaa nyumbani kwake au katika simu yake tu.

Wengi wanadhani AI ni mkombozi lakini ni vyema kukumbuka kwamba matumizi yake huzidisha uvivu wa kufikiri na kutenda.

#BM
 
Mkuu wanasema old is gold...
Sasa hivi michoro ya kuchora kwa mkono ina thamani sana...

Japo artificial intelligence ipo kasi ila kwa hapa kwetu bado sana ...

Maana hapo mwanzo walikuja watu wakatutisha sana ila kazi bado watu wanapiga kazi kazi
Ni kweli bado watu wanachora na michoro hiyo ina thamani kubwa, lakini huu ni mwanzo tu wa matumizi ya AI na matokeo yake yamekuwa makubwa.

Madhara yatakuwa badae ambapo program hizi zitakuwa na matumizi makubwa hasa kwa vizazi ambayo technology itakuwa sehemu kubwa ya maisha.
 
AI inasifiwa saaaanaa lakini tusichokijua ni watu kupoteza ajira.

Elimu haitakuwa na thamani tena

. Huu ni uhuni tu wa makampuni makubwa kujitengenezea pesa na kutokulipa kodi.

Watu wengi watapoteza kazi. Just saying
 
Matumizi ya AI yameshika kasi, uwezo wa program hizi kutengeneza picha kutokana na maono au mawazo ya mtumiaji, kumeongeza wimbi kubwa la picha hizo zikitumika katika maeneo tofauti...
Haiwezi maana hata camera hazikuondoa picha za kuchota
 
AI inasifiwa saaaanaa lakini tusichokijua ni watu kupoteza ajira.

Elimu haitakuwa na thamani tena

. Huu ni uhuni tu wa makampuni makubwa kujitengenezea pesa na kutokulipa kodi.

Watu wengi watapoteza kazi. Just saying
Itatengeneza ajira mpya. Mimi kitu ninachokifanya naona within 5 years to come kitakuwa kimepotea.
 
AI inasifiwa saaaanaa lakini tusichokijua ni watu kupoteza ajira.

Elimu haitakuwa na thamani tena

. Huu ni uhuni tu wa makampuni makubwa kujitengenezea pesa na kutokulipa kodi.

Watu wengi watapoteza kazi. Just saying
Hatua hiyo ya AI hatujafikia.

Tuko kwenye Hype
 
AI kuna maeneo haitaweza kuchora kama ukutani, kwenye mawe, magogo na sehemu zingine za ku paint. Natural art haitaweza kuchora, watu wataendelea kutaka michoro iliyochorwa kwa mikono, hiyo ndiyo sanaa asilia itaendelea kupendwa
 
Yah watu wanapenda picha zilizochorwa kwa mkono kwa sababu ya nguvu, muda kipaji kilicho kwenye picha yenyewe. By the way, siku hizi kuna printer za kuchora ukutani mkuu.
 
Njia ya kufikiri ni kuchora pekee ?; Mbona mambo ya kutumia fikra zako ni mengi ? AI inasaidia ku translate kilichopo kwenye akili yako kwenye kadamnasi ili wengi waone kile unachokiwaza..., Jambo ambalo hapo kale waliweza kulifanya wachache (through years of training) leo hii wanaweza kulifanya wengi....

Hivyo tunaweza kuwekeza akili zetu kwenye next best thing; after all its imagination that matters na AI imewezesha kuleta hilo kwenye mainstream....

You can not Stop the Waves, but you can Learn how to Surf....
 
AI kuna maeneo haitaweza kuchora kama ukutani, kwenye mawe, magogo na sehemu zingine za ku paint. Natural art haitaweza kuchora, watu wataendelea kutaka michoro iliyochorwa kwa mikono, hiyo ndiyo sanaa asilia itaendelea kupendwa
Lengo lao hasa ni kupunguza au kuuwa kabisa hizo natural art, na huu ni mwanzo tu.
 
Njia ya kufikiri ni kuchora pekee ?; Mbona mambo ya kutumia fikra zako ni mengi ? AI inasaidia ku translate kilichopo kwenye akili yako kwenye kadamnasi ili wengi waone kile unachokiwaza..., Jambo ambalo hapo kali waliweza kulifanya wachache (through years of training) leo hii wanaweza kulifanya wengi....
Kusaidia ku translate Mawazo yetu ni jambo jema ambalo AI imeleta, lakini tatzo ni kushindwa kubuni na kuwa na uvivu wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom