Dalili za kupotea kwa sanaa ya uchoraji kutokana na matumizi ya IA (Artificial Intelligence)

Dalili za kupotea kwa sanaa ya uchoraji kutokana na matumizi ya IA (Artificial Intelligence)

1. Leonardo da Vinci
2. Vincent van Gogh
3. Pablo Picasso
4. Michelangelo
5. Claude Monet
6. Rembrandt van Rijn
7. Salvador Dalí

Hawa jamaa sanaa zao za uchoraji zinaheshimika na kupata thamani kubwa hadi sasa .
Kweli hao ni magwiji katika sanaa hiyo na kazi zao zitabaki kuwa na thamani kubwa siku zote.
 
Matumizi ya AI yameshika kasi, uwezo wa program hizi kutengeneza picha kutokana na maono au mawazo ya mtumiaji, kumeongeza wimbi kubwa la picha hizo zikitumika katika maeneo tofauti.

Wasi wasi wangu ni kwamba itafika wakati hakutokuwa na haja ya kuwa na wachoraji wa picha, kwasababu program hizi zinaweza kutafsiri mawazo ya mtu na kutengeneza kitu au picha ambayo inaendana na matakwa ya mtumiaji.

Program hizi zitaeneza uvivu wa kutumia muda mrefu kuchora au kubuni picha, picha za wachoraji zitakosa soko kwani kila mtu anaweza tengeneza picha anayo taka akiwa amekaa nyumbani kwake au katika simu yake tu.

Wengi wanadhani AI ni mkombozi lakini ni vyema kukumbuka kwamba matumizi yake huzidisha uvivu wa kufikiri na kutenda.


#BM
Screenshot_20240830-094613_1.jpg

Mfano huo
 
Back
Top Bottom