Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Hii ni kawaida kwa dunia kuhama au kupiga hatua ya kutoka kuacha hiki na kuanza kutumia kilngine ambacho ni rahisi zaidi, hatua hiyo huitwa ni maendeleo.Matumizi ya AI yameshika kasi, uwezo wa program hizi kutengeneza picha kutokana na maono au mawazo ya mtumiaji, kumeongeza wimbi kubwa la picha hizo zikitumika katika maeneo tofauti.
Wasi wasi wangu ni kwamba itafika wakati hakutokuwa na haja ya kuwa na wachoraji wa picha, kwasababu program hizi zinaweza kutafsiri mawazo ya mtu na kutengeneza kitu au picha ambayo inaendana na matakwa ya mtumiaji.
Program hizi zitaeneza uvivu wa kutumia muda mrefu kuchora au kubuni picha, picha za wachoraji zitakosa soko kwani kila mtu anaweza tengeneza picha anayo taka akiwa amekaa nyumbani kwake au katika simu yake tu.
Wengi wanadhani AI ni mkombozi lakini ni vyema kukumbuka kwamba matumizi yake huzidisha uvivu wa kufikiri na kutenda.
Hata tulivyokuwa tukitumia kulimia au kuendea makazini kwa nyakati hizo, sivyo tunavyovitumia leo. Kwa hiyo, hakuna haja ya hofu, ikiwa dunia iko katika mchakato huo.
Siku hizi hata vituo vya taksi hakuna, kila kitu kinaisha kwenya Uber, kwani imerahisisha sana kwa kunetea taxi nilipo na mwenye taksi kuletewa mteja alipo.
Na kuna App ya msaada wa kisheria inasukwa, ili asiye na uwezo wa kuajili Wakili, apate mwongozo wa kwenda na kesi kwa App tu. Au App ya Afya inayoweza kukupima afya.
Kikubwa, tunapaswa kuwa kama Mamba ili kuendana na mazingira yote kwa namna yoyote yakibadilika kwa maendeleo. Tukikaa na kulia lia, dunia itatuacha.
Ova