Hiyo kuweka vikwazo ili wananchi wanao Unga mkono utawala wa kijeshi katika mgongo wa chama cha siasa Chenye jeshi lake.
Sio kuligawa jimbo bali kuwafanya wananchi waweze kukaa mbali na m23, japo inaweza kuleta hisia mchanganyiko kwa wanancchi kwa kuhisi ukandamizwaji, kutengwa nk
Mpaka sasa raia wengi wa DRC ina sadikiwa kuikimbia nchi kutoka maeneo yenye machafuko na kwenda sehemu zenye usalama ndani na nje ya DRC kama Burundi, Rwanda, Uganda nk
Napingana na kauli yako kwa namna moja.
Kwanza, hivi vita, usipolalia upande mmoja, vina vyanzo vingi mno.
Na raia kama raia, wanafuata mkumbo tu.
Mfano wa Bukavu. Kabla M23 haijaweka kambi, ilikuwa ikikebehiwa kama mbwa koko. Ilivyoingia, Ikapokelewa kifalme. Jana wazalendo walipovamia, wakapokelewa kama mashujaa. Sasa, kujua nini ni nini, si rahisi.
Kuhusu maeneo salama, Burundi isahau. Kwa sababu, Burundi imeshalalia upande wa kihutu. Ambao, japo hayasemwi, ilijua ikiipa kampani DRC, watutsi wa RED TABARA watamalizwa. Sasa hivi, ndo wanaenda kuungana na M23. Bujumbura, ipo umbali wa km kama 30 kutoka mpakani. Watutsi wa DRC waliopo Burundi, hasa wanyamulenge, wanataabika sana.
Sasa, ukisema ni kuwafanya raia wakae mbali na M23, hili kundi la M23, mifumo yake kama ya Rwanda. Jambo linalosababisha siku zote kuliona kama RDF. Kwa nchi kama Congo, ambapo watu wa kuanzia 1994, hawakuwahi kupata amani, nadhani miezi kama miwili sasa ndo wana uhakika wa kulala na kupata usingizi. Hawa watu ukiwambia waachane na M23, hutoweza. Lakini pia, raia na wao, wanaimani gani na M23? Bila raia utaongoza nini? Ndo maana unaona kuna vitu vingi M23 inafanya, vingine kama vipo nje ya uwezo wake, lakini lazima ihakikishe inaungwa mkono.
Unadhani DRC kuweza kurudisha hilo eneo mikononi mwake ni jambo jepesi? Ukizingatia nyuma ya hivi vita, kuna mataifa mazito, ambayo yanakoleza moto!!! Kauli Balkanization, iliongelewa miaka mingi siku za nyuma, watu wakapuuzia, lakini ndo hiki kinachoenda kutokea sasa.
Hakuna serikali inayoweza kuachia eneo lake kwa kigezo kama hicho. Hapo ni kwamba mifumo yote ya serikali ya awali inafumuliwa, na kuanzishwa mipya. Na huu utakuwa muda wa kujipanga sasa,kukabiliana na kila litakalotokea. Si kila mmoja ameshaona udhaifu wa mwenzake?