Hili jambo naliongelea mimi kama mimi na kwa uelewa wangu.
Ni kweli, Makenga aliwahi kuwa mwanajeshi wa RDF. Kama kina Kagame walikuwa wanajeshi Uganda.
Mpaka hapa, kila mkimbizi anaweza kulihudumia jeshi la nchi furani,hasa hizi zetu, lakini uhalisia akiwa si raia.
Kwa M23, hao unaowasema, historia yao, wengi wao wakiwa wakimbizi Rwanda, waliweza kuingia jeshini.
Penda usipende, watutsi wa DRC na Rwanda ni wamoja.
Jeshi la Rwanda, unalijua uwezo wake. Huo huo, ndo wa M23. Na nahisi pengine, ndo maana sasa hivi kutofautisha hizi pande mbili ni ngumu.
Jambo usilotaka kuongelea, ni uwepo wa mataifa makubwa yanayotumia mgongo wa watu kupata yanachokipata. Kwa taarifa za wanaojua, inasemekana hakuna nchi yenye utajili wa madini duniani kama DRC.
Nadhani ulisikia kesi ya Apple, kuzuiliwa kununua madini ya DRC. Sasa, itafunga kiwanda? Wengine, watafunga viwanda?