njumu za kosovo
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 3,820
- 9,625
Yes ni Kweli, Nina jamaa yangu Bukavu ni Mcongo, ananieleza kuhusu Wazalendo.Kuna taarifa maeneo mengi ya Bukavu yameanza kurudishwa na Wazalendo toka mikonono mwa RDF ambao wanajiita M23 ukweli juu ya hili upoje?
Sasa SI uhamie Rwanda!?Sisi wakongo twapenda tuwe sehemu ya Rwanda.Rwanda ni Nchi mzuri sana kuliko zote afrika mashariki
Wazalendo Jazi waliingia waliingia mjini goma na wakashambulia na ku retreat.Kuna taarifa maeneo mengi ya Bukavu yameanza kurudishwa na Wazalendo toka mikonono mwa RDF ambao wanajiita M23 ukweli juu ya hili upoje?
Pole yako. Ila tu cha kukushauri, za kuambiwa changanya na za kwako. kwa hiyo, Wazalendo wapo bora kuliko jeshi lenyewe! Si ndio! Yaani mtu wa kufundishwa kutumia bunduki siku mbili tatu,tayari ana mbinu za kijeshi kukabiliana na M23! We usicheze kabla ya mziki. Huyo ni mmoja, tafuta na wengine, Soma taarifa magazetini, huku unasubilia walau hata wiki hivi. ndo utajua uharisia wa ulichoambiwa.Yes ni Kweli, Nina jamaa yangu Bukavu ni Mcongo, ananieleza kuhusu Wazalendo.
Wazalendo ni Vijana walioamua kujikusanya Pamoja kukamata silaha na kuamua wao kama wao kupambana na M23, hii bila ya amri ya Serikali Wala muongozo wa Jeshi la Serikali, kumbuka Vijana wengi huko Kivu wanajua kutumia Silaha, na Sasa Wana Silaha nyingi ambazo walizichukua baada ya Jeshi la Serikali hapo Bukavu kukimbia.
Na majuzi kukatokea majibizano ya Risasi baada ya Jeshi la Serikali kuingia Bukavu kutoka miji mingine na hao Wazalendo..... Naambiwa baadaye wakaelewana, na Sasa wamewapa Silaha zaidi....! Nikitizamq baadhi ya video, Yani Wazalendo wanaonekana wana hasira na machungu kuliko Askari wa Jeshi, wanapopita mtaani hivi, unaona Vijana wengine wanatoka majumbani wanawakimbilia kuwapa pesa, na wengine wanaomba kujiunga nao.
Jamii inawa support Kwa Vijana wengi kujiunga nao, kuwapa madawa na chakula......! Wamefanikiwa kuwarudisha nyuma M23 Toka maeneo ya Bukavu mjini.
We ni mmoja wao, ndio maana unapinga drc kukombolewa toka kwa waasi.Hili jambo naliongelea mimi kama mimi na kwa uelewa wangu.
Ni kweli, Makenga aliwahi kuwa mwanajeshi wa RDF. Kama kina Kagame walikuwa wanajeshi Uganda.
Mpaka hapa, kila mkimbizi anaweza kulihudumia jeshi la nchi furani,hasa hizi zetu, lakini uhalisia akiwa si raia.
Kwa M23, hao unaowasema, historia yao, wengi wao wakiwa wakimbizi Rwanda, waliweza kuingia jeshini.
Penda usipende, watutsi wa DRC na Rwanda ni wamoja.
Jeshi la Rwanda, unalijua uwezo wake. Huo huo, ndo wa M23. Na nahisi pengine, ndo maana sasa hivi kutofautisha hizi pande mbili ni ngumu.
Jambo usilotaka kuongelea, ni uwepo wa mataifa makubwa yanayotumia mgongo wa watu kupata yanachokipata. Kwa taarifa za wanaojua, inasemekana hakuna nchi yenye utajili wa madini duniani kama DRC.
Nadhani ulisikia kesi ya Apple, kuzuiliwa kununua madini ya DRC. Sasa, itafunga kiwanda? Wengine, watafunga viwanda?
Haina shida. Waasi ni kina nani?We ni mmoja wao, ndio maana unapinga drc kukombolewa toka kwa waasi.