Dalili za ufisadi kwenye posho za wasimamizi wa mtihani wa Kidato cha nne

Dalili za ufisadi kwenye posho za wasimamizi wa mtihani wa Kidato cha nne

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Baadhi ya Halmashauri zimedaiwa 'kuwapiga' cha juu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.

Kwa utafiti wangu usio rasmi wa kuwapigia watumishi wa Halmashauri tofauti tofauti, nimegundua kwamba kuna Halmashauri zingine zimewalipa wasimamizi siku 19, zingine zikalipa siku 14 na zingine zikalipa kwa siku msimamizi atakazoingia darasani kusimamia. Kwa mfano, kama shule ina mchepuo wa sanaa pekee na ratiba ni siku tano au saba basi wamelipwa kwa siku hizo.

Swali:
Kwanini siku za malipo zitofautiane? Malipo hayo yamegharamiwa na NECTA au kila halmashauri inalipa kulingana na uwezo wake?
 
Huyo msimamizi c yuko nje ya kituo.iweje alipwe pungufu. Mbona kipindi cha uchaguzi huwa wanasambaziwa nakuku vituoni
 
Nimesikitishwa sana na hili, kila kona linasemwa jambo hili. Kuna Ufisadi mkubwa sana umefanyika katika mitihani hii, ni mradi wa wachache
 
Huyo msimamizi c yuko nje ya kituo.iweje alipwe pungufu.
Mbona kipindi cha uchaguzi huwa wanasambaziwa nakuku vituoni
Wanajisafirisha wenyewe na hakuna nauli yoyote wanayopewa.
 
Mtu alipwe kulingana na kazi yake

Yaani walimu mnatabu sana, umefanya kazi siku 5 then unataka ulipwe posho sawa mtu mwenye siku 14
Kama pesa ni ya serikali, itumike kama ilivyoelekezwa!

Kujinufaisha ndio kunapelekea uweze kujiona wewe ndie mmiliki wa rasilimali unazozisimamia kwajili ya wengine.

Makosa ya rushwa ni pamoja na kujipa uMungu mtu kupitia madaraka uliyopewa.

Lipeni wasimamizi wenu wasilalamike na muache kuchumia matumbo yenu.
 
Kama pesa ni ya serikali, itumike kama ilivyoelekezwa!
Kujinufaisha ndio kunapelekea uweze kujiona wewe ndie mmiliki wa rasilimali unazozisimamia kwajili ya wengine...
Ni serikali gani ulikwambia waliofanya kazi siku 5 walipwe sawa na hao wa siku 19?
 
Tanzania kwa sasa kauli mbiu ni kwamba kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake chief hangaya hana mda huo. Leo ametua na dege lake KIA ameenda kunuku kamisheni huko munduli.watendaji wake wameshamsoma hana makuu kwasasa yeye analetewa taarifa tu na anazikubali kwa 100%
 
Tanzania kwa sasa kauli mbiu ni kwamba kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake chief hangaya hana mda huo. Leo ametua na dege lake KIA ameenda kunuku kamisheni huko munduli.watendaji wake wameshamsoma hana makuu kwasasa yeye analetewa taarifa tu na anazikubali kwa 100%
Anahusikaje na waziri husika yupo?
 
Hii kada haina posho wala marupurupu hivyo ikitokea kajikazi kanakohusu hela hata ya buku wapo radh walogane

Kuna jamaa jiran yangu anasema yeye kamweka afisa elimu mfukon yaan kila Kaz ya kusimamia awepo

Mateso anayopata kila akienda kwenye ofs za huyo afisa lazma ambebee vijizawad kuku unga ndizi mihogo kifup jamaa n mtumwa TU
 
Back
Top Bottom