Dalili za ufisadi kwenye posho za wasimamizi wa mtihani wa Kidato cha nne

Hapana mwalimu. Ufisadi unahusu kiwango kikubwa cha fedha sio vijisenti hivi vya walimu wenye njaa.
Tafsiri ya neno fisadi haikusafishi hata kwa senti moja unayo iiba, pia kuchangia uzi huu hamjawekewa walimu pekee ndio mchangie, usinipe cheo cha wanyonge mnaoibiana hadi vijihela vya kujikimu.
 
Kwani wao walimu anasemaje?
Miongozo ya malipo inatakiwa iwe wazi
Hapa ndio baraza wanapokwama
 
Kama hii post ina ukweli basi kilichofanyika ni uhuni, unapaswa kuchukuliwa hatua. Naamini halitachukua mda mrefu kabla ya wahusika hawajawajibishwa.
 
Baadhi ya Halmashauri zimedaiwa 'kuwapiga' cha juu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa...
Mfumo wa Elimu bado hauendani na wakati na ndio huko tunakotoka na kuvujisha mtihani!

Wanafunzi waanze kutahiniwa kila mhula kuona maendeleo yake na anapokuwa hakufanya vizuri alama za chini atiliwe mkazo kupandisha alama zake na mwisho wa mwaka mtihani kidogo ujumuishe alama zote za awali kupata asilimianitakiwayo kufuzu.

Hakuna sababu ya kusubiria mtihani wa mwisho na kusema amefeli wakati amekalia dawati/jiwe au sakafu miaka 7 au 4!

Hatuhitaji Taifa la failure!
 
Tafsiri ya neno fisadi haikusafishi hata kwa senti moja unayo iiba, pia kuchangia uzi huu hamjawekewa walimu pekee ndio mchangie, usinipe cheo cha wanyonge mnaoibiana hadi vijihela vya kujikimu.
Mkuu I don't support kitendo hicho sema umetumia neno Nene mno. So wahusika watatolea ufafanuzi.
 
Hili Jambo lipo miaka yote . Sijui baraza kwanini huwa hawafatilii? Msonde halmashauri zinakupiga Sana kupitia bajeti wanayokutumia ukituma hela wao nikuidukua kwa kuwaounja wasimamizi idadi ya siku za kusimamia.
 
Mfumo wa Elimu bado hauendani na wakati na ndio huko tunakotoka na kuvujisha mtihani...
Bright idea...

Ni kweli kabisa. Inawezekanaje mtu aliyekaa shule miaka minne uje umpime kwa mtihani wa masaa 2 au 3 kisha useme huyu hawezi, hana akili au hana uwezo..?

Wengine anaweza awe totally mjinga huko nyuma. Lakini mtihani Wa mwisho kwa kutumia wizi Wa mtihani anatengenezewa alama bandia kuonesha ana ufaulu Wa juu kumbe ni bomu tupu...!

Kwa hiyo, ni hakika kabisa mtihani wa masaa 2 au 3 hauwezi kuwa kipimo sahihi na halisi cha uwezo wa mtu....

Kuwe na utaratibu wa kuwapima kila baada ya muda fulani na mwisho wa kozi/mafunzo wakawa na mtihani mmoja wenye alama 25 tu na 75 zingine zitokane na Continued Assessments...

Utaratibu huo utazuia ama kuepusha hata malalamiko kama haya na pia kupunguza gharama za uendeshaji....!
 
Kwwl
Kweli, lazima wabadili mtaala
 
Baraza wanatakiwa waweke wazi miongozo yote ikiwemo ya posho za wanaoshughulikia mitihani
Hili Jambo lipo miaka yote . Sijui baraza kwanini huwa hawafatilii? Msonde halmashauri zinakupiga Sana kupitia bajeti wanayokutumia ukituma hela wao nikuidukua kwa kuwaounja wasimamizi idadi ya siku za kusimamia.
 
Sasa unataka ulipwe Allowance hata kwa cku ambazo hajafanya hiyo kazi???? Serikalini kuna mambo ya ajabu sana ! Hapa hoja yako ni ipi haswa!???
 
Mkuu Sasa mbona umesanua dili letu , usiaribu Mambo kaa kimia, tumeisha lamba
 
Pole teacher vumilia
 
Mi sijaelewa hapa, yani kazi ya siku tano malipo yawe sawa na siku 19?

Na kama hii ilikuwa inafanyika huko nyuma huo ni wizi wa wazi kabisaaa.

Shule zote zinajulikana, pesa itengwe kulingana na mahitaji ya shule sio shule zote zipate mgao sawa wakati kuna baadhi zinahitaji pesa kidogo Au zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…