Dalili za ugonjwa wa UTI kwa wanaume

Dalili za ugonjwa wa UTI kwa wanaume

Hivi yaweza kutokea UTI ikaambukizwa kwa njia ya kujamiana?
 
Mi hata sijaelewa, umejikita kwenye afya au ngono hapo......Ingia internet/google ujiridhishe maana ya UTI, pia hizo STDs , kisha urudi mapema kabla watu hawajaenda Meeda Bar
 
[QUOINA "Kingcobra, post: 8034279, member: 36454"]Kinga kushuka inasababishwa na nini. Mimi nimekuwa nikitumia antibiotics mara kwa mara na nilipokwenda kupima full blood picture niliambiwa white blood cells count ipo 3.74 wakati minimum ni 4.0. Je, inaweza kuwa sababu ni hiyo ya kutumia mara kwa mara dawa? Je, ioi white blood cells ziongezeke nahitaji kufanya nini mbali ya kujiepusha na matukizi ya mara kwa mara ya dawa?[/QUOTE]
Hii ina ukweli kiasi gani
 
URINARY TRACK INFECTION (UTI)
UTI ni ugonjwa ambao unasumbua watu wengi; watoto, vijana na watu wazima.
UTI ni kifupisho cha Urinary Tract Infection.
Huu ni ugonjwa ambao hushambulia figo (kidneys); ureters; ambayo ni mirija inayounganisha figo na kibofu cha mkojo, kibofu cha mkojo (bladder) na urethra; sehemu inayotoa mkojo toka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili.
Kwa kifupu ugonjwa wa UTI hushambulia viungo vinavyohusika katika kupitisha mkojo kabla haujatoka nje ya mwili.
Hebu tuvitazame viungo hivi kabla ya kueleza chanzo cha ugonjwa na tiba ya UTI baadaye hapa chini.

Kuelewa vizuri tunachokizungumzia hapa tazama picha ya viungo hivi na kwa kifupi hapa tutatoa maelezo ya picha hiyo. Figo ni viungo viwili vilivyopo kimoja kila upande wa uti wa mgongo eneo la kiunoni. Figo hufanya shughuli nyingi katika mwili wa binadamu ikiwepo ya kutoa uchafu na maji ya ziada katika damu, na huvitoa vitu hivi kama mkojo.
Kwa sababu hii, figo ni muhimu sana katika kuweka msukumo wa damu kwenye kiwango kizuri. Figo pia husikia
mapema sana mabadiliko ya kiwango cha sukari mwilini na mabadiliko katika kiwango cha msukumo wa damu (blood pressure).
Kiwango cha sukari na msukumo wa damu vikizidi, vyote huweza kuleta madhara kwenye figo.
Ureters ni mirija miwili myembamba yenye urefu wa yapata nchi 10 hivi kila mmoja ambayo huchukua mkojo kutoka kwenye figo na kuumwaga ndani ya kibofu cha mkojo.
Kibofu cha mkojo ni kijimfuko kidogo kinachopokea mkojo kutoka kwenye mirija ya ureters na kuuhifadhi.
Mkojo ukifikia kiwango fulani ndani ya kibofu cha mkojo, tunasikia haja ya kuupunguza (kukojoa) na ndipo misuli ya nje ya kibofu cha mkojo hujibana na kuukamua mkojo nje ya kibofu.
Urethra ni mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na nje ya mwili.
Sehemu yo yote katika hizi tulizozitaja hapa juu, inaweza ikapata maambukizi ya UTI na kadri maambukizi hayo yatakavyokuwa ndani zaidi ukitokea nje, ndivyo ugonjwa huu utakavyokuwa umefikia hali mbaya zaidi.
Wasichana na akina mama hupata maambukizi haya kwa wingi zaidi kuliko wavulana au akina baba.
Asilimia kama 40 ya wanawake na asilimia 12 ya wanaume hupata maambukizi haya ya UTI katika maisha yao.

Chanzo Cha UTI ni nini?
Mkojo kwa kawaida ni kitu kisicho na wadudu wo wote wabaya.
Maambukizi yanakuja pale wadudu wanapoingia kwenye mkondo wa mkojo kupitia kitundu cha kutolea mkojo nje ya mwili na kufuata mkondo huo kuelekea kwenye figo. Wadudu hao wakisha ingia huanza kuzaliana.
Asilimai 90 ya maambukizi yasiyo mabaya sana huwa ni ya bacteria waitwao Escherichia Coli au kwa kifupi E. Coli.
Kwa kawaida bacteria hawa huishi katika utumbo au karibu na maeneo ya mkundu.
Wadudu hawa wanaweza wakatembea kutoka eneo la mkundu wakaelekea kwenye tundu la mkojo na kuingia. Lakini, kutojisafisha kwa namna nzuri (kwa mfano, kutawadha kuanzia nyuma kuja mbele) au ngono ndizo njia mbazo huambukiza bacteria hawa kirahisi zaidi.
Wanawake hupatwa zaidi na maambukizi haya kwa sababu ya ukaribu wa mkundu na kijitundu cha kutolea mkojo na kwa sababu ya ufupi wa urethra katika miili yao ukilinganisha na wanaume.
Wanawake wanaoshiriki ngono mara nyingi na watu tofauti hupatwa na maambukizi zaidi kuliko wale wanaoshiriki kwa kiwango kidogo.

Wanawake wanaotumia diaphragms kama njia ya uzazi wa mpango hupatwa zaidi na tatizo hili pia akina mama waliokoma hedhi kwa sababu ya ukosefu wa homoni ya estrogen.
Kukosekana kwa estrogen kunasababisha mabadiliko katika mkondo wa mkojo na kuufanya uweze kuambukizwa kwa urahisi zaidi.

Matatizo yo yote yanayosababisha mkojo usitoke nje kwa urahisi huongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UTI. Mifano ni; watoto kuzaliwa na matatizo katika mikondo yao ya mkojo ambayo huzuia mkojo usitoke nje kirahisi, matatizo ya kidney stones na prostate kukua kupita kiasi; na watu wanaotoa mkojo kupitia kifaa maalumu (catheter).

Tendo la kukojoa huwatoa bacteria hawa nje ya mwili lakini wakiwa wengi sana, kukojoa hakuwezi kuwatoa wakaisha. Wadudu hawa husafiri kwenye urethra hadi kwenye kibofu cha mkojo ambako watazaliana. Wanaweza kuendelea kusafiri kupitia ureters hadi kwenye figo ambako pia watazliana na kuleta matatizo makubwa endapo tiba nzuri haitatolewa kwa wakati muafaka.

Ni nini Dalili za UTI?
Dalili za ugonjwa huu huwa tofauti kulingana na hatua ambayo ugonjwa umeshafikia.
Lower UTI ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, mgonjwa atasikia dalili zifuatazo:

. Maumivu wakati wa kukojoa
. Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu
. Damu katika mkojo
. Mkojo wenye rangi ya chai
. Mkojo wenye harufu kali
. Maumivu ya kiuno kwa wanawake
. Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume

Upper UTI ni maambukizi ya ndani ya figo. Hii ni hatua mbaya sana endapo bacteria wataanza kuingia kwenye mkondo wa damu kutoka kwenye figo – SEPSIS. Sepsis huweza kusababisha msukumo wa damu kuwa mdogo sana (Low Blood Pressure), mshituko au kifo.

Dalili za upper UTI ni:

. Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo
. Homa
. Kusikia baridi
. Kusikia kichefuchefu
. Kutapika

Hatua Za Kujikinga Na UTI
Kuna hatua unazoweza kuchukua ili usipatwe na maambukizi ya ugonjwa huu kirahisi. Hii ni pamoja na kujifuta au kutawadha ukianzia mbele kwenda nyuma baada ya haja kubwa au ndogo. Kunywa maji mengi, glasi 6 hadi 8 za maji kila siku na kuhakikisha unakunywa maji baada ya kushiriki tendo la ndoa. Haifai kuubana mkojo kwa muda mrefu, timiza haja mara itokeapo. Kusafisha maeneo nyeti mara kwa mara. Kuoga kupitia bomba la mvua ni bora zaidi kuliko kutumbukia kwenye josho. Ni vema kuvaa chupi zilizotengenezwa kwa pamba.

Tiba Ya UTI
Tiba kwa ugonjwa wa UTI kwa hatua zote ni antibiotics. Daktari ataamua kukupa tiba na kukuruhusu kuendelea na tiba nyumbani kwako au kukulaza kulingana na alivyoiona hali ya ugonjwa wako. Tiba ya lower UTI ikitolewa kwa wakati mwafaka na inavyotakiwa, hakuna matatizo makubwa yanayoweza kutokea.
Lakini tiba ispotolewa kwa wakati, maambukizi haya ya mkondo wa mkojo huweza kuleta matatizo makubwa. Pamoja na mengine mgonjwa anaweza:

. Kupata maambukizi ya mara kwa mara
. Kupata uharibifu wa figo wa kudumu na kuhitaji huduma maalumu ya kutibu figo (dialysis).
. Kutokea uwezekano wa kuzaa watoto wenye uzito mdogo au wanaozaliwa kabla ya wakati. . Wanaume wanaougua UTI mara kwa mara wanakuwa kwenye hatari ya kupata madhara kwenye tezi dume (prostatitis). Uvimbe huweza kutokea kwenye tezi dume na kusababisha maumivu wakati wa haja ndogo au kutoa shahawa. . Sumu katika damu. Mara chache huweza ikatokea kuwa bakteria wakasambaa kutoka ndani ya figo na kuingia kwenye mfumo wa damu (sepsis) na baadaye kusambaa hadi kwenye viungo vingine muhimu vya mwili. Hali hii ikitokea, itabidi mgonjwa awekwe chini ya uangalizi mkali wakati akipewa tiba ya kuwaua bakteria hao.

Katika mada nyingine tutatazama tatizo la high blood pressure .
Usisite kuuliza swali au kutoa maoni yako kuhusiana na mada yetu. Tutafurahi sana kusikia kutoka kwako na kukujibu.
Habari zenu wakuu,

Naomba kupata msaada wa kujua dalili za ugonjwa wa Urinary Track Infection (UTI) kwa wanaume na nini madhara yake.

Nashukuru sana in advance
 
UTI ni nini ?

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.
Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata

tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.
Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.
Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.
Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.


Sababu za UTI


UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.

Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.
Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi (cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.
Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.
Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika

Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.

Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.@Pafyum
Safi ndugu Mzizi mkavu
 
madhara ya UTI ni yapi?
"MADHARA YA UTI KWA MAMA MJAMZITO"
U.T.I inamwadhiri mtoto haswa kwenye ukuaji wake unamdhoofisha afya yake na kuwa na uzito mdogo
Mtoto anakosa nguvu hivyo mama anashindwa kusikia mama mtoto anacheza tumboni
Kuna dalili kubwa ya mtoto kuzaliwa njiti(pre mature)
Kuharibika kwa mimba (miscarriage).
"USHAURI"
Wanawake wanatakiwa kuepuka kuweka kuweka vidole ukeni wakati wa kutawaza na kutokutoa ule ute mweupe kwani ule ndio kinga yako kubwa kuepuka mambukizi haswa kama U.T.I.
Unachotakiwa kufanya wakati wa kuoga ni kujimwagia maji kwa nje ya uke na usitumie sabuni kali au shampoo kwani zinauwa bacteria wazuri wanaokupa kinga Kwenye Uke ( PH - POTENTIAL HYDROGEN ) na Kukusababishia Kuwa Rahisi Kushambuliwa na aina Nyingine za Bakteria Wenye Madhara Kwenye Uke .
Unapotumia choo cha public kuwa makini na usafi wa mazingira ya choo na maji utakayo tumia kunawa.
Pia Inashauriwa Kutotumia Dawa za Kienyeji Zenye lengo la Kunogesha Uke na Kufanya Uwe Mnato.

Ukiipuuza U.T.I Unaweza kupata athali kubwa sana kama zifuatazo
1.Figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) hii ni hatari sana ,hutokana na bacteria kushambulia figo
2.Kupatwa magonjwa ya kibofu ,kama kibofu kuziba ,kushindwa kukojoa ,hii hupelekea MTU kukojoa kwa mirija
3 .maumivu ya mgongo, kiuno na NYONGA
4.kupoteza hamu ya tendo la ndoa.nk.
5.kuharibu homon(hormon inbalance)
6.mimba kuharibika
7.kushindwa kubeba mimba
 
Back
Top Bottom