Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Usijali! Tukitolewa kwenye hatua hii, basi dada zetu wa simba Queens watatuwakilisha vizuri tu kwenye mashindano yao ya wananwake.Mimi ni shabiki kindaki ndaki wa Simba, na nimekuwa mfuatiliaji wa timu yangu pendwa ya Simba, lakini kuna muda inakosesha amani na kunikatisha tamaa ya kuendelea kuipa imani yangu.
Najihisi kupata ugonjwa wa moyo na hii timu. Nimekuwa nikifanya kila viongozi wa timu watakalo i.e kwenda uwanjani, kununua ticket na kuwanunulia marafiki zangu, kuchangia uwanja na kila mchango ambao Wanasimba tulipaswa kushiriki.
Ninalipia kadi za uanachama kwa wakati, ninanua jezi na kila bidhaa ya Simba itokayotoka kwa Vunja Bei, hadi nimekuwa nikijihisi niyafanyayo hayatoshi kuonesha mapenzi yangu kwa Simba. Naenda mbali na kuwafanyia hayo hayo marafiki zangu, lengo ni kuongeza motisha kwa timu.
Lakini viongozi wa Simba wamekuwa wakinikatisha tamaa wakiongozwa na Afisa Habari wetu ambaye ni “Muongo muongo”, “Mjanja mjanja” na “Mnafiki mnafiki”. Tukifungwa kujifanya kaumia sana na hayupo upande wa viongozi, tukishinda kujifanya yupo upande wa viongozi!
Kilichoniuma sana ni leo baada ya taarifa rasmi kuhusu maandalizi ya timu kuelekea kuikabili De Agosto ya Angola, hizi tetesi zilipita kwenye magroup ya Simba nikahisi ni uongo ila sasa zimetoka rasmi kuwa SIMBA ITAFIKA ANGOLA TAREHE 8 na ITACHEZA MECHI TAREHE 9. Niwaulize mashabiki wenzangu wa Simba, kwa ratiba hii tunatofauti gani na IHEFU Au NAMUNGO?
Kwa timu ambazo zipo siriazi (Serious) na Kombe la CAF zinaweza kika ugenini masaa kadhaa kabla ya Mechi? Simba Tunakosa nini cha kutufanya tufike mapema Angola, tukajiandaa na kuzoea mazingira, kushusha pressure na kupata mashabiki “Wawili watatu” wakutushangilia?
Kwa ukubwa walio nao De Agosto, kwa kikosi tulichonacho ambacho mwalimu wa timu amekiri bado kina mapungufu makubwa ya kiufundi ambao unachagizwa na saikolojia ya timu, kweli tunaenda Angola masaa kadhaa kabla ya mechi?
Mbona Zanzibar tulienda siku kadhaa kabla ya michezo ya kirafiki? Simba tunakosa nini kinachotufanya tufike Angola masaa kadhaa kabla ya mechi, na tuondoke mara baada ya mechi, kama siyo kuwachosha wachezaji kisaikolojia?
Tumesahau msimu uliyopita timu ndogo toka Bostwana ilitutoa (Jwaneng Galax), leo tuenda kupambana na miamba Ya Angola tunaenda masaa kadhaa kabla ya mechi? What a joke!
Kwasasa Simba Tunajivunia Hatua Ya Makundi sijui Robo Fainali hivi Yanga Msimu huu wakifikia Hiyo Hatua Tutaficha wapi sura zetu? Tutajivunia na Nini Cha Zaidi? Angalia timu za Kiarabu ambazo huwa Serious na Kombe hili zinavyo wahi kuondoka Makwao? AL hilal Kashaondoka Anajiandaa kuingia Tanzania. Kwa hili Limeniuma Sanaaa…. Sioni Matumaini Ya Simba Kufika Hatua Ya Makundi kwa Misimi Miwili Mfululizo….. kwa kutokuwa Serious na uendeshaji wa Timu.
Hatuwezi kukaa na kocha, hatuwezi kukaa na wachezaji, hatuwezi kusajiri, hatuwezi kutetea makombe, hatuna consistency ya ubora katika pitch. Yani tupo tupo kama watoto yatima, hakika inauma sana na kufedhehesha.
Ni wapongeze De Agosto kwa kuingia hatua ya makundi. Ni hayo tuuu…. Juma Mgunda, Matola na viongozi wapuuzi wa Simba hawezi kutufikisha popote. Tusamehe Mgunda tunakulaumua bure tuu, lakini UONGOZI WETU NI WA HOVYOOO SIJAPATA KUONA.
Kwa mara nyingine tena hongereni De Agosto kwa kuingia hatua ya makundi ya Kombe la CAF. [emoji120][emoji120]
Isitoshe mwekezaji wetu kwa sasa ni promota maarufu nchini! Hivyo ataitisha mapambano mengi na mabondia kutoka pande zote za dunia, kuja kuitangaza nchi yetu.