Dalili zinaonesha kuwa Simba hawana malengo na Kombe la CAF

Dalili zinaonesha kuwa Simba hawana malengo na Kombe la CAF

Mimi ni shabiki kindaki ndaki wa Simba, na nimekuwa mfuatiliaji wa timu yangu pendwa ya Simba, lakini kuna muda inakosesha amani na kunikatisha tamaa ya kuendelea kuipa imani yangu.

Najihisi kupata ugonjwa wa moyo na hii timu. Nimekuwa nikifanya kila viongozi wa timu watakalo i.e kwenda uwanjani, kununua ticket na kuwanunulia marafiki zangu, kuchangia uwanja na kila mchango ambao Wanasimba tulipaswa kushiriki.

Ninalipia kadi za uanachama kwa wakati, ninanua jezi na kila bidhaa ya Simba itokayotoka kwa Vunja Bei, hadi nimekuwa nikijihisi niyafanyayo hayatoshi kuonesha mapenzi yangu kwa Simba. Naenda mbali na kuwafanyia hayo hayo marafiki zangu, lengo ni kuongeza motisha kwa timu.

Lakini viongozi wa Simba wamekuwa wakinikatisha tamaa wakiongozwa na Afisa Habari wetu ambaye ni “Muongo muongo”, “Mjanja mjanja” na “Mnafiki mnafiki”. Tukifungwa kujifanya kaumia sana na hayupo upande wa viongozi, tukishinda kujifanya yupo upande wa viongozi!

Kilichoniuma sana ni leo baada ya taarifa rasmi kuhusu maandalizi ya timu kuelekea kuikabili De Agosto ya Angola, hizi tetesi zilipita kwenye magroup ya Simba nikahisi ni uongo ila sasa zimetoka rasmi kuwa SIMBA ITAFIKA ANGOLA TAREHE 8 na ITACHEZA MECHI TAREHE 9. Niwaulize mashabiki wenzangu wa Simba, kwa ratiba hii tunatofauti gani na IHEFU Au NAMUNGO?

Kwa timu ambazo zipo siriazi (Serious) na Kombe la CAF zinaweza kika ugenini masaa kadhaa kabla ya Mechi? Simba Tunakosa nini cha kutufanya tufike mapema Angola, tukajiandaa na kuzoea mazingira, kushusha pressure na kupata mashabiki “Wawili watatu” wakutushangilia?

Kwa ukubwa walio nao De Agosto, kwa kikosi tulichonacho ambacho mwalimu wa timu amekiri bado kina mapungufu makubwa ya kiufundi ambao unachagizwa na saikolojia ya timu, kweli tunaenda Angola masaa kadhaa kabla ya mechi?

Mbona Zanzibar tulienda siku kadhaa kabla ya michezo ya kirafiki? Simba tunakosa nini kinachotufanya tufike Angola masaa kadhaa kabla ya mechi, na tuondoke mara baada ya mechi, kama siyo kuwachosha wachezaji kisaikolojia?

Tumesahau msimu uliyopita timu ndogo toka Bostwana ilitutoa (Jwaneng Galax), leo tuenda kupambana na miamba Ya Angola tunaenda masaa kadhaa kabla ya mechi? What a joke!

Kwasasa Simba Tunajivunia Hatua Ya Makundi sijui Robo Fainali hivi Yanga Msimu huu wakifikia Hiyo Hatua Tutaficha wapi sura zetu? Tutajivunia na Nini Cha Zaidi? Angalia timu za Kiarabu ambazo huwa Serious na Kombe hili zinavyo wahi kuondoka Makwao? AL hilal Kashaondoka Anajiandaa kuingia Tanzania. Kwa hili Limeniuma Sanaaa…. Sioni Matumaini Ya Simba Kufika Hatua Ya Makundi kwa Misimi Miwili Mfululizo….. kwa kutokuwa Serious na uendeshaji wa Timu.

Hatuwezi kukaa na kocha, hatuwezi kukaa na wachezaji, hatuwezi kusajiri, hatuwezi kutetea makombe, hatuna consistency ya ubora katika pitch. Yani tupo tupo kama watoto yatima, hakika inauma sana na kufedhehesha.

Ni wapongeze De Agosto kwa kuingia hatua ya makundi. Ni hayo tuuu…. Juma Mgunda, Matola na viongozi wapuuzi wa Simba hawezi kutufikisha popote. Tusamehe Mgunda tunakulaumua bure tuu, lakini UONGOZI WETU NI WA HOVYOOO SIJAPATA KUONA.

Kwa mara nyingine tena hongereni De Agosto kwa kuingia hatua ya makundi ya Kombe la CAF. [emoji120][emoji120]
Usijali! Tukitolewa kwenye hatua hii, basi dada zetu wa simba Queens watatuwakilisha vizuri tu kwenye mashindano yao ya wananwake.

Isitoshe mwekezaji wetu kwa sasa ni promota maarufu nchini! Hivyo ataitisha mapambano mengi na mabondia kutoka pande zote za dunia, kuja kuitangaza nchi yetu.
 
Usijali! Tukitolewa kwenye hatua hii, basi dada zetu wa simba Queens watatuwakilisha vizuri tu kwenye mashindano yao ya wananwake.

Isitoshe mwekezaji wetu kwa sasa ni promota maarufu nchini! Hivyo ataitisha mapambano mengi na mabondia kutoka pande zote za dunia, kuja kuitangaza nchi yetu.
Mtopolo mwenzako huyu naona mnaelewana lugha.
 
hapa nakuunga mkono bwasheee kama tungepewa ile zalan ya sudan kusini sasa hivi tushatolewa siku miingiiii, nyasa bullets wepesi mnooo
Simba sio Biashara United! Kumbuka Simba kuingia makundi sio issue hawa ni wazoefu kwenye haya mashindano ondoa shaka, ndani ya kipindi cha miaka 4 robo fainali mbili! Hata hao Waangola wanajua wanakwenda kukutana na timu ngumu.
 
Kipindi Mo akilalamika kupata Hasara wa bongo wengi walikuwa waki beza na kuamini alikuwa anapata faida kubwaa .......ifike pahala mwenye pesa zake za halali aheahimiwe na sio kudhihakiwa, .... Utopolo hao hapo wame kaa kimya mdhamini kanjanja ajisombea tu
 
773339846a084ff7a1666bffac32a396_310321669_177929738148331_5220426121946754109_n.jpg
 
Mleta mada nadhani umetosheka na majibu murua kabisa kutoka kwa mashabiki wa majayanti ya soka Africa mashariki.
 
Hivi nyie mnaosema hapo Simba kuna tatizo hilo tatizo mbona hamlitaji?.naona kila mtu simba kuna tatizo....pale simba kuna tatizo si mlitaje hilo tatizo?.Kama familia tuu ya watu 4 haikosi changamoto ndo ije kuwa taasisi kubwa kama Simba?.nyie endeleeni kusubiri hilo tatizo lifumuke mlifume upya la sivyo naona mnapoteza sana muda kuijadili Simba..
 
Hivi nyie mnaosema hapo Simba kuna tatizo hilo tatizo mbona hamlitaji?.naona kila mtu simba kuna tatizo....pale simba kuna tatizo si mlitaje hilo tatizo?.Kama familia tuu ya watu 4 haikosi changamoto ndo ije kuwa taasisi kubwa kama Simba?.nyie endeleeni kusubiri hilo tatizo lifumuke mlifume upya la sivyo naona mnapoteza sana muda kuijadili Simba..
Ni wivu tu
 
Kama Simba wataondoka na ndege ya kukodi kwenda Angola nitawaelewa kuwa wanakwepa fitina za mpira na gharama za Hotel [emoji2922] maana Luanda Angola maisha ni ghali sana, Kwaiyo wanafika na kucheza na kurudi ila wakumbuke michezo ya Covid haijaisha waende na wachezaji wa kotosha.
Kama Simba wataondoka Kwa flight [emoji3575] ya connection pale Oriver Tambo wakatue Luanda Angola basi uongozi utakua na shida sana maana walitakiwa kuwahi mapema.
Simba itasafiri kwa ndege ya kukodi kwenda Angola.
 
Back
Top Bottom