Damas Ndumbaro atupwa jela ya soka miaka 7

Sema huyu jamaa Ndumbalo aliharibu siku anamuidhinisha okwi kukipiga msimbazi,,, safi sana tff watu kama hawa wafai kushiriki katika soka manake wanapindisha sheria...

Na ndio maana wazee wa jiji wakawa wanaamuangalia tu Damas ndumbalo mbio zake kuona zitapoishia....sasa wamemdaka ukingoni hana ujanja...cheze system ya soka wewe?
 
Last edited by a moderator:
Mtoto wa darasa la kwanza leo akimaliza elimu ya msingi na huyo wakili ndo atarud tena sokani

Akirudi baada ya miaka saba na umaarufu wake kwenye soka umekwisha, tatizo watu wanaingia kwenye familia ya soka kiujanja ujanja matokeo yake ndio haya kupata watu kama kina Ndumbaro (historia yake ya soka naona imeanza hivi karibuni tu kama wakala wa wachezaji mbali ya hapo sidhani hata katika level ya chini aliwahi kuwa mdau kwenye yale machama yetu ya mtaani)
 
sasa kama vilabu vimemkana, inamaanisha vimekubali kukatwa 5%??

Mwenyewe sijaelewa ni nini hasa lengo la kumkana mtu anayetetea maslahi ya vilabu.

Kwa kuwa hii ni nchi ya wapigaji,pengine viongozi wa vilabu wameahidiwa 10% ili jamaa apotezwe mazima.

Dauda mwenyewe mhanga wa hizi hukumu za kiwendawazimu.
 
Aliongea kwa 'utashi' wake!!! ina maana hakutumwa na vilabu kuongea yale aliyoyaongea???? mmmmmmmmh! mbona hii haiji kiakil au kuna mchezo umechezwa hapa!!! soka la bongo lina mizengwe, Ngoja tutamsikia Ndumbalo atasemaje....

Atakuwa alitumwa na club yake ya Simba.
 
Sawasa TFF walichofanya sababu hawezi kujivisha mtetezi wa vilabu ila hali watu tunajua katumwa na watu ili Malinzi aonekane hafai kwa sababu Dewij kanyimwa kuuza Jezi za taifa, na hujma wanazofanya timu ya Taifa Malinzi piga lungu. Kitu kingine waandi wa michezo Tanzania ni wanafki sana, mnaju kabisa Bodi ya Rigi iko chini ya TFF sio chombo huru, Ndumbalo ni mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF atakuwaje mtetezi wa vilabu? Ongeeni vitu vya maana ili mpira wa Tanzania usonge mbele.
 
Dewji ndio alikuwa analeta jezi za taifa stars ndio maana jezi za kijinga sana zamani tulikua tunaita utumbo wa paka kwa maana hazifai jezi za hovyo sana
 
Pumbuvu huyu NDUMBALO nilianza kumchukia tangu siku anamuidhinisha emanuel okwi kuwa mchezaji halali wa simba kutoja dar young africans,,,naona hata kile kifungo alichofungiwa ni kifupi mno angepigwa ban ya maisha bila kujihusisha na masuala ya soka. Na huyu kanjibai DEWJI mbona anatuharibia mpira wetu jamani!!!!?
 
Lini ndumbalo alimuidhinisha okwi kucheza simba..haya mambo ya simba na yanga yanavuruga sana utaratibu,sasa mtu kma ww angalau unaelewa baadhi ya vitu una mawazo kma haya je uko vijijini kukoje...?
 
Hili ndo soka la bongo bana mwanasheria D. Ndumbaroo aliekua anatetea vilabu visikatwe asilimia 5 na TFF ametupwa jela ya soka na kutojihusisha na soka miaka 7, Pole sana wakili ila ujifunze kua wakubwa wakitaka kula ukae kimya
 
Lini tena hii fafanua zaidi tafali Tunzo
 
Last edited by a moderator:
Hee,sasa hilo balaaa,Dr mzima! Hapa kuna namna sio bure!
 
Dr Ndumbaro pole sana rafiki yangu mimi hili nililitegemea hasa baada ya jinsi ulivyo handle issue ya Wambura Mike na baadae issue ya Okwi. ..mtego huo huo wa press na wewe umekubana always strive to truth and transparency esp following the laws .let's wait when u come back as usual to press.
 
Ama kweli kuishi tz ni kuona mengi..sijawahi kusikia mtu anamkana wakili wake anaemtetea, au kuna kitu kimejificha nyuma ya hili?? mwenye updates atujuze...(ingawa mimi sijaumia kufungiwa kwake)
 
Lini ndumbalo alimuidhinisha okwi kucheza simba..haya mambo ya simba na yanga yanavuruga sana utaratibu,sasa mtu kma ww angalau unaelewa baadhi ya vitu una mawazo kma haya je uko vijijini kukoje...?
Wewe unauliza lini NDUMBALO alimuidhinisha okwi kucheza simba kutoka yanga!!!!!!!!!! Nadhani wewe sio mfuatiliaji wa mambo ya mpira hasa Bongo league.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…