NAKEMBETWA
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 3,517
- 3,135
Mleta mada amemaliza form four mwaka jana alikuwa anasoma shule ya boarding toka yupo chekechea ndio amepata nafasi ya kusikiliza nyimbo, so tumsamehe bure!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mleta mada amemaliza form four mwaka jana alikuwa anasoma shule ya boarding toka yupo chekechea ndio amepata nafasi ya kusikiliza nyimbo, so tumsamehe bure!
Ukweli ulio wazi ni kwamba .......
Kizazi cha mistari nondo uzao wa Fid Q kikiandika mtari mmoja Mtu kama Mwana FA ili alete maana ile ile anaandika Nyimbo nzima,
Angalia mfano:
"Pole pole... ndio mwendo kila akikumbuka inamuuma, kwanza viliumbwa vidole binadamu ndio akaunda uma" By Fid Q
"Naona mlango wa pepo ila sioni pakutokea, hii pesa imetoka jando inataka kuni babu sea" By Stamina
"Usimpige mkeo mpige shangwe, maana Young killer sio ngazi kwahiyo mwambieni shetani asinipande " By Msodoki BestMan
Huyo mwana FA wenu akitaka kuimba alete maana ya mstari wowote kati ya mistari hiyo basi ataandika nyimbo nzima,
Mfano mdogo, nyimbo nzima ya usije mjini Killer anaweza kuiandika kwa mstari mmoja ukasimama kuliko nyimbo nzima ya mwana FA,
Sasa msiwe mnafloo bila fact write down, mkishupalia mwana FA mkali bila vigezo na sababu mnakuwa na mapenzi tu hamna sababu.
CC: kende youngd diCaprio Honey Faith Viol Farha
Ni upumba.vu kumcompare FA na stamina period
"Nina Mistari mikali HADI Luanda ananionea gere", "Nina mistari mikali HADI George anarudi Bush", "Bongo Jua la utosi HADI Juma anakosa Nature"-Stamina
#USITAKE NCHEKE
Huu wimbo aisee..
amelala na bibi harusi na wala''Mara nyingi alikuwa mpole, Mara chache alizoongea wote tulimgeuza shule, Nasaha za bure kama tupo class vile..
Alituasa kuhusu kuhusiana, akatuonya kutokuaminiana, Mtazamo wake na wa mama Terry daima ulifanana'' - MwanaFA
VS
'' Ulikuja kwa Wema kumbe moyoni Sepetu'' ''Mlevi unayekunywa Gongo ukifa utazikwa La Mboto''- Stamina
Naendelea kuonesha utofauti tu wa uandishi... You do the judging!
fa MKALI jamaniMungu hakupi kama hataki,hata ukipora itapotea mradi yatimie maandiko....
dont hate the prayer,hate the game dont bi mad...
kuna vingi vya kumuomba mungu kabla hujamuomba utajir.....
Hakuitwa mwanafalsafa kwa kubahatisha,na kama nakosea niko tayar kukosolewa,biNAMU ndo msanii pekee anayetamka kiswahil fasaha ktk ukiacha mjomba
Acheni upunguwani ndugu zangu wengi mnatumia uzoefu tu sababu mwana fa ni mkongwe lakini kwa mistari ya stamina anasubir.Stamina mistar yake inapaswa kuwekwa maktaba na vyuo vikuu kufundishia.kama una uwezo wa kusoma nyuma ya ubao au uoni kwa jicho la tatu huwez kumuelewa stamina.Naunga hoja kama huna digrii mbili uwez kumuelewa stamina.
FA ni mwingi wa majigambo,stamina anacheza na maneno......tungo zenye akili mtafute songa,one, Jay mo,Salu T wale ndo waandishi, FA wa kawaida sana,anatumia ukongwe
stamina:
maisha yashakunywa super shaft yananizidi nguvu za kiume
natamani kula baga ila naishia viazi vya gairo
maisha ni kama komborela masikini ndo mlinda kopo
mi nadhani haya maisha yana ramani ila alowachorea masikini peni ilimgomea njiani
mwanafa
ingekuwa vipi duniani kusingekuwa na dini...dunia bila dhambi kipimo cha uovu nin...ingekuwa vipi kasi ya ukimwi kusingekuwa na kondom..yan ingekuwaje bila ukimwi tungetinga condom??au ingekuwa kuna ukimwi halafu hakuna condom unadhani mi ningesema mi na mabinti damdam??
kuna mabinti wapo kamili kila idara..familia bora..akili zisio lala..maumbo bomba na sura..wao ni ajira na hawahitaji zaidi ya sera...
sasa wanauliza steve b ni dj au mc...mi sijiviki uwakili na nakaa nje ya hii nategea scratch za bonny..zikitia hewan mi mzigoni...utajuta kuwa vitani au utakoma kwa shindani clap clap..
jamani wenye akili pimeni
Kwa hiyo wewe una degree tatu na macho manne basi wewe sio binaadamu wa kawaida sisi wenye macho mawili na elimu ya kawaida tunamkubali mwana FA
dddaaahhh jamani hebu kasikilizeni kwanza album ya mwanafalsafani ndo mje tubishane...daahh eti fa umliganishe na stamina??daaahh mpaka naskia hasira...fa alitoaga wimbo wa ingekuwa vip nakumbuka zilitoka nyimbo kama 3 kuujibu wimbo ule mmoja tu....sister p aliropoookaaa..mwanafa akamjibu kauli moja tu...kasolo zenye kasoro...kama hujui fasihi huwez kuelewa kauli tata za binamu...kaburi halihitaji mbwembwe ndo mana hawaweki ac.....binamu ni chombo kingine
mkuu kasolo zenye kasoro huwa ana maana gani
Okey labda nijaribu kuiweka namna nilivoelewa mimi mana tafsiri huwa zinatofatiana kutokana na uelewa..kama kuna maana nyingine naomba wadau wataongezea...maana yake ni hii katika wimbo wa hey hey dj
sista p alijaribu kumponda binamu katika mashairi ya ingekuwa vipi kwa kumwambia binamu kuwa mistari kaiba kwa mwanamziki flani(jina nimelisahau) na kuuponda kuwa una kasoro nyingi ule wimbo..lakin matamshi yake ya lafudhi akatamka kasolo badala ya kasoro....sasa katika kumjibu ..binamu akaona udhaifu ule wa matamshi ya maneno alionao sista p akaona wala asipoteze nguvu nyiiingiii kumjibu kwa kutunga wimbo mzima bali akamjibu kwa mstari mfupi tu kuwa .."wewe sista p unanikosoa wakati tayari unawasilisha ujumbe ukiwa na kasoro na umeshindwa kutamka hata neno kasoro kwa ufasaha na unatamka kasolo kweli utaweka kunikosoa mimi? Ndo akaandika maneno hayo machache ya "kasolo zenye kasoro".....hii ni kwa maoni yangu wadau kama kuna tafsiri deep zaidi tuendelee kuelimishana maana hatuna degree mbili za kumuelewa stamina mambumbumbu sisi so tunakomaa na binamu