Du pole sana! Lakini kwa jinsi ulivyoelezea inaonekana kama ni tatizo ambalo ulikuwa nalo muda sema baada ya kufanya mapenzi ndio likajitokeza kitu cha msingi muone daktari mapema kwani inawezekana ikawa kweli ni magonjwa ya zinaa, lakini kama itakuwa ni ugonjwa wa zinaa kama ukiwahi huwa yanatibika kiurahisi sana hauna haja ya kuchanganyikiwa, labda kitu cha msingi mueleze mwenzangu juu ya hilo na vile vile jaribu upate tiba ya pamoja, kwani ukipata wewe pekee inaweza isisaidie sana. Ni kweli magonjwa ya zinaa kwa akina dada dalili huwa zinahelewa kujitokeza sana wanaweza kukaaa na huu ugonjwa hata miezi minne lakini tofauti na kwa mwanaume huwa mara nyingi ndani ya masaa 24 dalili zinaanza kujitokeza, je hizo damu haziambatana na usaha au harufu mbaya? vipi kwenye kichwa cha uume wako hakuna vipele vyovyote?