Damu inanitoka kwenye dhakari

Damu inanitoka kwenye dhakari

Metallic

Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
57
Reaction score
6
Wakuu,

Ni mara ya kwanza kunitokea hali hii after kufanya mapenzi na my fiance this weekend, niligundua natoka damu ktk mboo after kwenda kukojoa yani niliumia sana as if kuna viwembe vinakata ktk njia ya mkojo, kujiangalia baada ya kukojoa nikakuta damu inatoka kwenye mboo.na kuanzia hapo damu imekua inatoka kila nikikojoa.
Jamani wataalamu naombeni msaada hii ni kitu gani?? na nini kisababishi??na dawa yake nini??
Natanguliza shukrani zangu...
 
Mkuu pole sana hapo unaweza kuwa umepata magonjwa ya zinaa(kisonono au kaswende) au utakuwa na ugonjwa wa kichocho,kimbia haraka hospitali kabla hiyo hari haijakuletea madhara makubwa zaidi hasa kuharibu uzazi.
 
hiyo gono, wahi hospitali, .....what a fiance!!
 
Muende hospitali haraka - wewe pamoja na mchumba wako. Usimwache nyuma.
 
Ushalikanyaga kudadadeki, wahi hosp, na hiyo ni taa ya tahadhari kwako kuhusu huyo fiance
 
sababu hizo zilizo tajwa zaweza kuwa sahii. Dalili hizo pia zaweza kuwa ugonjwa wa prostate glands ambao mara nyingi huwapata watu wenye umri mkubwa. dalili nyingine ni kukojoa mara kwa mara. usahauri: kachukue vipimo hospitali kwa uhakika zaidi.
 
Huo uchumba unawalakini based kwenye uaminifu,
POLE NA WAHI HOSP MKUU.
 
Sukrani sana wakuu kwa ushauri,
but how long does it take kwa dalili za gono ama ugonjwa wa zinaa kuanza kujitokeza???
 
Sukrani sana wakuu kwa ushauri,
but how long does it take kwa dalili za gono ama ugonjwa wa zinaa kuanza kujitokeza???

yani uctafute mchawi we wahi kwanza hospitali kabla ya yote ucjekupotza uzazi
 
Sukrani sana wakuu kwa ushauri,
but how long does it take kwa dalili za gono ama ugonjwa wa zinaa kuanza kujitokeza???

Dalili za Gono hujitokeza haraka sana kwa mwanaume - nasikia hata siku ya pili/tatu
 
Du pole sana! Lakini kwa jinsi ulivyoelezea inaonekana kama ni tatizo ambalo ulikuwa nalo muda sema baada ya kufanya mapenzi ndio likajitokeza kitu cha msingi muone daktari mapema kwani inawezekana ikawa kweli ni magonjwa ya zinaa, lakini kama itakuwa ni ugonjwa wa zinaa kama ukiwahi huwa yanatibika kiurahisi sana hauna haja ya kuchanganyikiwa, labda kitu cha msingi mueleze mwenzangu juu ya hilo na vile vile jaribu upate tiba ya pamoja, kwani ukipata wewe pekee inaweza isisaidie sana. Ni kweli magonjwa ya zinaa kwa akina dada dalili huwa zinahelewa kujitokeza sana wanaweza kukaaa na huu ugonjwa hata miezi minne lakini tofauti na kwa mwanaume huwa mara nyingi ndani ya masaa 24 dalili zinaanza kujitokeza, je hizo damu haziambatana na usaha au harufu mbaya? vipi kwenye kichwa cha uume wako hakuna vipele vyovyote?
 
uyo fiancee kakufiancee vizuri kweli..dah...kakuletea gono, tena linalotoka kwenye mb.ooo ya mtu mwingine...hahahahaha. uzinzi kazi kwelikweli..
 
Ndugu yangu Metallic usije kurupuka mlaumu au gombana na mchumba wako sababu ya ushauri wa baadhi ya watu humu ndani ukidhani umeambukizwa ugonjwa wa zinaa...mara nyingi kama sio zote ugonjwa wa zinaa (Gonorrhoea au Syphilis (Kaswende)) huwa na dalili za kutoa usaa, si damu mbichi.

Timing ya hiyo damu kwenye mkojo ni muhimu kujua...inatoka unapoanza kukojoa halafu baadae unatoka mkojo wa kawaida (mara nyingi ni kichocho)? unatoka mkojo wa kawaida halafu inatoka damu (Injury)? au ionatoka damu mwanzo mpaka mwisho (inawezekana ikawa uvimbe au kansa ya kibofu kama umri wako umeenda ie. zaidi ya miaka 50 hivi)...nenda hospitali, tyoa historia ya ugonjwa bila kificho na utafanyiwa vipimo na kupata tiba.

NB: Sahau kuhusu kulaumiana na mwenzi wako kuwa umetendwa kama walivyoshauri wengine.
 
Back
Top Bottom