TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU PUANI NA TIBA YAKE (NOSEBLEED)
kutokwa na damu puani kwa lugha ya kitaalamu inafahanika kama
(epistaxis)
Ni kuvuja kwa mishipa midogo midogo ya damu iliopo puani
(blood vessels), hili nitatizo la kawida sana kwa watu wengi na sio hali hatarishi sana japo kwa wengine hujirudia mara kwa mara kwa kiwango cha juu
(chronic).
SABABU KUU ZA TATIZO
Zipo sababu nyingi kubwa ni hizi:-
->kukauka kwa kiwambo/utando wa ndani ya pua
(nasal membrane) hali inayopelekea kutungeneza nyufa na kuchanika kwa mishipa ya damu puani... "Membrane inaweza kukauka kwa sababu ya hali ya hewa, upepo, na baridi kali.
->Kufikicha ama kuingiza vidole puani (hasa kwa watoto)
->Dawa zinazozuia damu kuganda na kufanya mishipa ya damu kuwa myembamba kiasi cha kurahisisha kuchanika.
Mf warfarin, Asprin n.K
->shinikizo la juu la damu
(hypertenstion)
->Matumizi yaliyokithiri ya pombe
->uvimbe puani na matatizo ya kurithi
KUNDI LINALOKUMBWA SANA NA TAIZO HILI
1.Watoto (kwa kufikicha pua kwa vidole)
2.Wazee
3.wajawazito (kubadilika kwa homoni mwilini)
NJIA ZA KUZUIA DAMU INAYOTOKA
1.Inamisha kichwa kuelekea upande wa mbele...
EPUKA kuinamisha kichwa kwa upande wa nyuma(kulala chali) kwani kutasababisha damu kurudi ndani ya koo la hewa ama chaukula na hivyo kusababisha kichefuchefu,kutapika na tatizo ktk upumuaji
2. bana pua kwa kutumia vidole hku ukipumulia mdomo ili kusaidia damu kuganda na mishipa kuziba
3. Tumia barafu, kwa kuiweka ktk kitambaa kizito na ukande juu/nje ya pua
4.Kaa kimya utulie huku ukihakikisha kichwa kinakuwa usawa wa juu ya moyo
5.Tatizo likiendelea zaidi fika kituo cha afya kilicho karbu kwa msaada zaidi wa matibabu
ONYO
-> Usiweke pamba ama kitambaa puani
->usitumie dawa zinazosababisha kupunguza kuta za mishipq ya damu, dawa hizo nikama
Antimflamatory drugs(Ibuprofen),Asprin, warfarin n.K kwani hufanya damu iendelee kutoka ... Muone daktari kama ulikuwa kwenye dozi ya dawa hizo
KUZUIA TATIZO LISIJIRUDIE TENA
Fanya yafuatayo:-
1.Usifikiche pua ama kuweka kitu chochote puani, unapopiga chafya fungua mdomo ili hewa isipitie puani
2. Usifanye kazi ngumu zinazokulazimu kuinama kunyanyua vitu vizito
3. weka kichwa usawa wa juu wa moyo, kuzuia damu nying kusukumwa kuelekea upande wa kichwani (puani)
4. Usivute sigara
5. Kula mlo laini na vinywaji baridi(beverage), usitumie vinywaji vya moto ndan ya masaa 24 mf chai kahawa n.K
-> USITUMIE ASPRIN, IBUPROFEN, WARFARIN na dawa zingne za makundi hayo
NINI CHA KUFANYA
HATUSHAUR MTU KUNYWA DAMU HIVYO MTU UKIANZA TOKWA DAMU WEKA KICHWA CHAKO KUELEKEA CHINI UKIBANA PUA YAKO KWA DAKIKA KUMI KUNA HALI YA DAMU KUGANDA
(CLOTTING) NA KUSABABISHA DAMU KUTOTOKA UNAWEZA FANYA HIVI HUKU UKIJIKANDA NA BARAFU AMBAYO ITAKUA MSAADA WA KUPUNGUZA UPANA WA MSHIPA
NJIA RAHISI ZA KUTIBU
1. Pakaa ointment mfano vasseline.. Hapa waweza kutumia mafuta ya mgando/mazito ili kulainia ndani ya pua kuzuia mishipa kuchanika
2. Zuia mtoto asifikiche pua
3. KITUNGUU Maji
Kitunguu Maji kinasaidia sana kutibu hili tatizo,
->kata vipande vidigovidogo kisha weka chini ya tundu za pua na uvute harufu ndani ya dakika kadhaa tatizo litaisha
-> pia unaweza kukamua juice yake kisha dondoshea matone 2-3 katikai tundu zote zapua tiba itatokea ndani ya muda mfupi
NB
IKIWA UMEFANYA YOTE NA BADO HALI IMEKUA KOROFI BAS HAKIKISHA UNAPATA MWIBA WA NUNGUNUNGU UCHOME NA NUSA MOSHI WAKE UTASAHU TATIZO HILO KWA UWEZO WA MWENYEEZI MUNGU