Naomba wataalamu watuambie ni vyakula gani mwanamke anaweza kula akaongeza damu haraka wakati wa ujauzito au ni dawa gani zinazoweza kumfaa kuongeza kiwango cha damu naomba jibu wataalamu.
Habari,
Utaratibu wa njia ya kuongeza damu hutegemea na kiasi cha damu, umri wa ujauzito pamoja na yote mlo kamili huambatana katika njia zote.
1: Kunywa dawa ambazo zina kiasi kikubwa cha madini chuma na folic acid.
2: Kuchoma sindano au drip yenye kimiminika chenye madini chuma.
3: Kuongezewa damu
NB: Lishe au mlo kamili huusisha:
1: Tunda/matunda ya msimu kwa kila mlo.
2: Vyakula jamii ya protein: jamii ya kunde, nyama , maziwa, mayai na samaki mfano dagaa.
3: Mboga za majani zinazipatikana kwenye eneo la muhusika.
4: Vyakula vya wanga: wali, ugali, viazi nk.
Tende na maziwa zimejizolea nafasi kwenye hili poa.