BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Hawa wanaweza kuwa ndio wale wafadhili wa Royol tour ambao tulifichwa , sasa wanapewa mapande ya aridhi, na wana binasifisha, fikiria Mzungu ana binasifisha Aridhi ya Umma.
======
Tanzania ni nyumbani kwa moja ya hifadhi bora za wanyama barani Afrika, ambayo inafanya iwe sehemu ambayo inapenda kutembelewa sana na watu wengi ulimwenguni, lakini kisichojulikana ni kuwa kuna hifadhi ya wanyama ya Mwiba ambayo inamilikiwa kibinafsi na bilionea Mmarekani.
Mmiliki wa hifadhi hiyo anajulikana kama Bilionea Dan Friedkin, ambaye makao yake makuu yako Texas, ni Mwenyekiti wa Gulf States Toyota.
Bilionea Dan Friedkin
Kulingana na makala ya Forbes, mfuko wa familia yake, Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org), unashiriki kikamilifu katika uhifadhi wa Afrika Mashariki na umekodisha ekari milioni 6 za eneo la pori la Tanzania kwa lengo la kulilinda.
Haijulikani bilionea alilipa kiasi gani kuipata hazina hii, lakini inasemekana kuwa hifadhi hiyo ilifanywa kuwa ya binafsi mwaka 2009.
Mwiba, ambayo inaenea zaidi ya ekari 125,000, inapakana na mpaka wa Magharibi wa eneo la uhifadhi la Ngorongoro na sehemu ya Kusini ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Uhamaji wa nyumbu wa Serengeti hupita kupitia Mwiba kati ya Desemba na Aprili. Ikiwa na vilima virefu, msitu mnene, mashimo ya maji na mito (iliyokauka) ambapo mabwawa hutokea, maji yake ya kudumu huvutia wanyama pori mwaka mzima
Wageni ambao wamewahi kufika Mwiba wanasema ni kama sumaku ya wanyama wakati sehemu ya Kusini ya Serengeti na maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro yanakauka kati ya Julai na Novemba kila mwaka.
Kulingana na Friedkin, Logde ya Mwiba, ambayo gharama yake ni dola za Kimarekani 1,800 (Milioni nne na ushee za Kitanzania) kwa mtu, ilijengwa ili kuwa na uwepo unaofanana na mandhari ya sehemu hiyo.
"Utekelezaji wa muundo ulikuwa jitihada ya pamoja, lakini mke wangu, Debra, ndiye anayepewa sifa zote kwa wazo kumbukumbu tuliotaka kuwapa wageni wetu," anasema.
The Citizen