Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Believe me, watanzania walio wengi (hasa wasio wa asili ya asia na europe) tunakabiliwa na ushamba wa kiwango cha juu katika mambo mengi duniani hususan namna ya kutumia fursa za kiuchumi zilizopo duniani na kujiletea kipato na utajiri. Matokeo yake tutaendelea kuwa chawa wa akina Mo, GSM, Bakhresa, Manji etc. Mbaya zaidi hali hii ipo pia hata kwa waliosoma hata kama kwa kiwango cha PhD.Hawa wanaweza kuwa ndio wale wafadhili wa Royol tour ambao tulifichwa , sasa wanapewa mapande ya aridhi, na wana binasifisha, fikiria Mzungu ana binasifisha Aridhi ya Umma.View attachment 2610183
Watanzania wanatoka kwenye maeneo yenye kila aina ya fursa, ila wataziacha na kwenda kuwa walinzi mjini. Akija foreigner, akiziona hizo fursa na kuzitumia huanza kulalamika wanaibiwa! Ukiuliza humu wangapi wana acre 49 zinazotolewa bure na Kijiji popote, wengi wao hata habari hawana. Akitokea investor/foreigner akitumia sheria zetu na kuchukua ardhi na kufanya uzalishaji, watakuja mitandaoni kulalamika.
Peaple, fursa za kidunia hasa rasilimali hazina mipaka kama mnavyodhani. Hata wewe ukiwa na akili na hela ukihitaji ardhi hata 50,000 acres ndani ya US unaweza kuzipata. Hakuna nchi isiyo na sheria za matumizi ya ardhi katika uwekezaji. Ndio maana unaona makampuni makubwa yanachimba madini na oil kila kona ya Dunia, yanalima, kufuga nk. Watanzania tujenge utamaduni wa kutumia fursa zinazotuzunguka kwa umakini. Sio kweli kwamba maadam rasilimali zipo Tanzania basi zitatumika na watanzania pekee.
Korea hana coltan, unataka smartphone azitengeneze vipi kama hajaenda Congo kuchukua coltan?
Rasilimali zilizopo duniani ni za wenye akili na maarifa tu regardless ziko katika nchi gani na wao wanatoka nchi gani.
Hicho kipeperushi hakina taarifa zozote za maana ku justify ulichoandika. Hao watu wanatumia sheria zenu hizo.