Dan Friedkin mmiliki wa AS Roma anamiliki ardhi kubwa Tanzania, mamlaka zimchunguze

Mambo mazito sana haya , ccm watapita kama hawaoni,

Hivi inawezekana ccm ikishaondoka madarakani kuja kuwavulumisha hawa wezi au ndo basi tena,

Yan kuna majitu yanaiba kama vile hayatakufa,
 
Mwiba Game Reserve imekuwepo muda mrefu kabla hata ya awamu ya sita ila kama mtu mmoja tena ambaye sio raia anaweza kumilikishwa ekari 25,000 basi twafa.
Tatizo la watanzania mpo very emotional hta kwenye mambo ambayo hayahitaji kuwa emotional...Nchi ni km taasisi, inafanya biashara au we unadhani hizo ekari 25000 huyo mwekezaji kapewa bure?

Mnataka nchi ipate maendeleo. Basi nakubalini michakato ya maendeleo ikiwemo kukodisha ardhi ili serikali ipate hela za kuleta hyo maendeleo.

So far nchi ya Tanzania ina ekari za mraba laki tisa ambazo zimeshatumika hazizidi laki tatu. Kwa hiyo kuna ekari zaidi ya laki sita zipo idle...sasa nini kupigia kelele ekari 25000 ambazo hta hazijauzwa moja moja zimekodishwa tu?
 
Unakua Land Grabing in Afruca? Wacha kubweka bweka humu, Wazungu hawajawahi kuwa marafiki
 
Mimi nafikiri atkuwa ni mwekezaji tu kama alivyo yule wa Grumeti game reserve. Kuwekeza kwenye tourism sector ina afya kwa nchi ili mradi asivunje sheria.
Wale wa Migodi ya North Mara na kule Kahama na Geita wanavunja sheria yoyote? Je mbona kuna Umasikini wa kule? Swala sio kuvunja sheria kwa hio unaunga mkono raia kuhamishwa na maeneo kupewa wazungu kisa hawavunji sheria? Kichwani una ubongo au Kamasi?
 
Shida sio kukodishwa ili nchi ipate pesa za kuleta maendeleo , tatizo kile nchi inapata katika ukodishaji huo ndo kinachostahili? Na je iyo mikataba ya ukodishwaji imezingatia maslahi mapana ya nchi, ukizingatia aina ya viongozi tulionao walivyojaa ubinafsi wa matumbo yao na familia zao?

Viongozi hawaaminiki na wananchi sababu kuu wizi wa mali za umma ambao wamekua wakiufanya waziwazi ndo chanzo cha makelele yote
 
Nafikiri ni wawekezaji tu sidhani kama ni wamiliki wa ardhi hiyo kwa kuwa sheria yetu ya ardhi bado hairuhusu ardhi kumilikiwa na mgeni bali mwekezaji tu kwa masharti.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kwa nchi ambayo Raia kutwa nzima maada ni yanga na Simba sishangai, nchi ina raia wasio jitambua, kutwa nzima Yanga , Simba, wanaweza kuwa na muda wa kufuatulia mambo kama haya?
Yaani Yanga na Simba ningekuwa na mamlaka ningezifutilia mbali
 
Unaongea lugha ya mwaka 1970 wakati wa Ujamaa,mabepari wameshika mpini hivi sasa hata ndani ya nyumba yako unachimba sharti mkono wa birika uwe unatoa.
 
Mapori yapo mengi tu ila baadhi ya sisi walalahoi tunakula bata tu.

Hapa napata SAFARI LAGER!
 
Never again Rais wa Jamhuri atoke Zanzibar.

Hao hawana uzalendo kabisa.

Wanagawa mali za Tanganyika kama pipi.

Hawana madini Wala wanyama.

Tuwe makini nao.
Acha kukurupuka dogo, mwiba estate amepewa na marais wa zamani huko mbali
 
Hawa wanaweza kuwa ndio wale wafadhili wa Royol tour ambao tulifichwa , sasa wanapewa mapande ya aridhi, na wana binasifisha, fikiria Mzungu ana binasifisha Aridhi ya Umma.

View attachment 2610183
Kwani shida ni nini hapo hasa?
Amedhulumu ardhi, amefisadi nchi au nini hasa.

Kwa wenye majibu au taarifa au ushahidi naomba kufahamishwa zaidi. Asanteni
 
Never again Rais wa Jamhuri atoke Zanzibar.

Hao hawana uzalendo kabisa.

Wanagawa mali za Tanganyika kama pipi.

Hawana madini Wala wanyama.

Tuwe makini nao.
Waliokuwa sio Wazanzibar walifanya nini, Waafrika wote sisi ni shida tuu wala hamna wa kumlaumu zaidi ya sisi wenyewe na akili zetu hovyo
 
Hoja yako inaweza kuwa na mashiko, hebu tujiulize lini hizo billions ziliisaidia Tz kikamilifu?
 
Hawa wanaweza kuwa ndio wale wafadhili wa Royol tour ambao tulifichwa , sasa wanapewa mapande ya aridhi, na wana binasifisha, fikiria Mzungu ana binasifisha Aridhi ya Umma.

View attachment 2610183
Haya mambo yanafanyika kimya kimya tu, na hata huko Bungeni hawajui kitu, na hata kama wangejua wasingehoji chochote.

Hivi wakati ule wa utumwa, watu walikuwa wakijua kinachoendelea katika maeneo yao? Si walistukizwa tu, vijana wenye siha kukamatwa kama mifugo na kuondoshwa?

Sasa hali ndiyo hiyo tena, mama anajua njia zake nzuri zinazofanya kazi bila ya kuleta rabsharabsha ndani ya jamii.
Tutauzwa sana safari hii kama tusipoamka na kutafuta uhuru wetu upya kabisa.
 
Nani kakwambia kwenye mradi huu Wananchi wataamishwa? kichwani una ubongo au kamasi?
 
Tanzania mapori mengi sana, hata wewe ukiwa na hela unanunua ekari utakazo.

Kama kuna maeneo ekari moja inauzwa mpaka laki moja na zipo nyingi hazina hata wanunuzi shida iko wapi, hapo tu mbwewe, msata, hiyo kiwangwa, hapo kidomole nk ambapo ni karibu na Dar ardhi ekari moja inauzwa laki tano na maeneo mpaka kesho yapo yakumwaga.

WaAfrica wengi wetu akili zetu fupi sana, leo hii ukiwaambia watu wakalima kwenye mashamba yao ya urithi wanaleta blah blah na yamebaki mapoli tu huko, akija Mzungu au Mgeni akanunua ardhi hiyo hiyo, ng'a ng'a za kumwaga.

Matajiri wetu wenyewe wenye hela wanachoweza ni kujenga bar, night clubs, mahoteli, guest house katikati ya mji na kuwa wanasiasa, wakija wenzao wanaowaza parefu hata 100yrs mbele tunaaza blah blah.

Mbona hatulalamikii Wazungu kuja kuchimba madini na kumiliki migodi, kuja kuchimba gas na mafuta pamoja na kumiliki vitalu baharini huko...

Huko baharini kuna visiwa tele havina watu vinazagaa zagaa na kuwa maficho ya pirates na wahuni wengine na wala husikii Tajiri dar es salaam hapo akitaka kununua na kufanya investment baadala yake wakija weupe tunaanza kelele nyiiingi..
Ni nani alishawahi kutoka na hela zake africa na kwenda kuwekeza kwenye ardhi ya USA au kununua kisiwa pale New Mexico au Kule Jersey akakataliwa?..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…