Danadana ya kupatikana Katiba mpya lengo ni kuhalalisha mikataba mibovu

Baada ya Bunge la CCM kupitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World ya Dubai hakuna tena shaka kuwa adui wa taifa hili ni CCM.

Kumbe ile dana dana iliyokuwa ikipigwa kuchelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya, ilikuwa kuwezesha Tanzania kuingia laini katiba mikataba ya aina hii.

Sote tumeshuhudia vipengele kadhaa ndani ya hii Katiba chakavu vikitumika lengo kuu likiwa ni kuhalalisha makabidhiano ya bandari zetu kwa wageni.

Baada ya bandari kipi kitafuata?

Baada ya bandari, mwarabu atapewa ngorongoro kwani Wamasai tayari wameshafurushwa.
 
Tanesco,ATCL ama SGR yenu.. kama nikiwa nimekufa mtakuja kusema hata kaburini mwangu, hivyo vitapigwa mnada wa kimagendo.
 
Kwahiyo wewe unataka Bandari ibaki kama kambi ya wavuvi mpuuuzi wewe, Kama ulikuwa unafurahia kuchelewa kwa mizigo umeumia
Sasa tulitaka uhuru wa nini, wakati kila kitu sisi wenyewe hatuwezi hadi wageni ndio wafanye? Huu ni ushahidi kuwa wakoloni wangekuwa wanatutawala hadi leo tungekuwa tumepiga hatua kubwa kuliko kuwa chini ya hawa wakoloni weusi wa CCM.
 
Tatizo la Tanzania alitengeneza mroho wa madaraka Nyerere.

Hata elimu hakutaka watu waelimike
 
Tatizo siyo katiba mpya, tatizo ni akili mbovu za watanganyika kufikiri kwa kutumia matumbo. Amini nakwambia hata katiba mpya iletwe, hakuna jambo la ajabu litakalofanyika hapa nchini. Kama wananchi hawana utamaduni wa kuwa wastaarabu, wanaojiheshimu na kujiwekea miiko binafsi hata katiba ushushwe na Mungu hawataiheshimu.

Vitabu vitakatifu kama Biblia vipo lakini watu bado wanaendelea kutenda dhambi tu. Kule Uingereza na Israeli hawajawahi kuandika katiba lakini mambo yao yanaenda vizuri kwelikweli. Sababu kubwa ni kwamba kabla ya kuundwa kwa katiba ni lazima jamii ibadilike kifikra na kimaamuzi. Tuliosoma sheria tunaamini kwamba katiba ni ushahidi tu wa makubaliano baina ya watawala na watawaliwa (A Social Contract). Sasa hayo makubaliano ndiyo huwekwa ndani ya kitabu kiitwacho katiba.

Hivyo watu hutengeneza katiba, na siyo katiba ndiyo inatengeneza watu....
 
Acha kumsingizia Nyerere aliyeondoka madarakani 1985, Kwa yote yanayotokea raia wamechukua hatua gani za kuwashinikiza watawala kwamba jambo fulani hawalitaki?
Tozo ....
Kejeli kutoka kwa viongozi....
Rushwa zawazi wazi.......
Ni uvivu, uoga na ujinga wa kifikra kumsingizia mtu aliyefariki 20 nyuma, matatizo yako.
 
Baada ya Bunge la CCM kupitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World ya Dubai hakuna tena shaka kuwa adui wa taifa hili ni CCM.

Kumbe ile dana dana iliyokuwa ikipigwa kuchelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya, ilikuwa kuwezesha Tanzania kuingia laini katiba mikataba ya aina hii.

Sote tumeshuhudia vipengele kadhaa ndani ya hii Katiba chakavu vikitumika lengo kuu likiwa ni kuhalalisha makabidhiano ya bandari zetu kwa wageni.

Baada ya bandari kipi kitafuata?
Tuungane wananchi wote wenye dhamira njema, kuidai katiba mpya kwa nguvu zetu zote.

Na kwenye katiba mpya kuwepo na kipengere kinachozuia kabisa mtu asiye raia wa Tanganyika kufanya makubaliano yoyote kuhusiana na rasilimali za Tanganyika.

Leo tumeshuhudia:
Rais kutoja Zanzibar, Waziri kutoka Zanzibar, katibu mkuu wa wizara kutoka Zanzibar wakiuza bandari za Tanganyika.
 
Hakuna bunge nimeshawahi kulidharau kwenye historia ya Taifa letu kama bunge hili.

Na hii ni regardless of the constitution that we’ve had since independence.
Bunge hili takataka la sasa ni legacy mbaya kabisa ya marehemu.
 
Nina hakika hata ile rasimu ya Warioba haingetoa mwanya kwa huu upuuzi tunaoushuhudia. Tutegemee kushuhudia mengine mengi.

Kwa kasi hii Watanganyika msipozinduka tutakula mabua. Kwa hili Bunge hatuna chetu, CCM ni ile ile, watu ni wale wale na sera ni zile zile.
Ile katiba ya haikuwa na nafasi kabisa ya mzanzibari kupiga mnada rasilimali ya Tanganyika.
 
Tatizo siyo katiba mpya, tatizo ni akili mbovu za watanganyika kufikiri kwa kutumia matumbo. Amini nakwambia hata katiba mpya iletwe, hakuna jambo la ajabu litakalofanyika hapa nchini. Kama wananchi hawana utamaduni wa kuwa wastaarabu, wanaojiheshimu na kujiwekea miiko binafsi hata katiba ushushwe na Mungu hawataiheshimu.

Vitabu vitakatifu kama Biblia vipo lakini watu bado wanaendelea kutenda dhambi tu. Kule Uingereza na Israeli hawajawahi kuandika katiba lakini mambo yao yanaenda vizuri kwelikweli. Sababu kubwa ni kwamba kabla ya kuundwa kwa katiba ni lazima jamii ibadilike kifikra na kimaamuzi. Tuliosoma sheria tunaamini kwamba katiba ni ushahidi tu wa makubaliano baina ya watawala na watawaliwa (A Social Contract). Sasa hayo makubaliano ndiyo huwekwa ndani ya kitabu kiitwacho katiba.

Hivyo watu hutengeneza katiba, na siyo katiba ndiyo inatengeneza watu....

Katiba ni msingi, huwezi kujenga nyumba juu ya Katiba mbovu, hiyo nyumba haiwezi kudumu. Kama ingekuwa kama unavyodai, CCM wala haingeogopa ujio wa Katiba.

Hiki chama cha dhulma kilichojaa wezi na wachumia tumbo kinajua fika kuwa ujio wa Katiba mpya ndio mwisho wao. Ndio maana wanathubutu kukufuru kuwa hata kwa mia hawatoki.

CCM ni nyonya damu, bila damu ya Watanzania masikini kitakufa. Nilisema hili mwaka 2008 na mpaka leo CCM bado ni ile ikiwa na fikra zile zile.

Utawasikia bila aibu wakidai eti hakuna chama mbadala. Aliyekuwa msaidizi mkuu wa JPM sasa ni Rais na anamwagiwa sifa zile zile…nachoka!
 
Miaka ya 90's Uganda iliandika katiba mpya bora kuwahi kutokea barani Afrika, lakini nini kinatokea mpaka leo. Kule bondeni, kuna demokrasia hatari sana lakini ANC bado wanafanya mambo ya ajabu mno na wala hawafanywi kitu. Wamarekani walipata uhuru mwaka 1776, lakini wakaandika katiba yao ya kwanza mwaka 1789.

Unadhani tokea mwaka 1776 waliwezaje kuishi bila katiba ? Marekani ilikuwa ni jamii ya kiungwana mno yenye watu waliosoma na kustaarabika. Bila kuwa na jamii ya watu waliostaarabika na wanaofahamu nini wanakitaka, hata uandike sheria nyingi kiasi cha kujaza maktaba ya Alexandria, utakuwa unafanya kazi bure.

Narudia kusema hivi: "A Constitution is not a document, but a condition in which the entire polity/state, political, social and economic proceedings are subjected under the authority of the law which is certain, congruent and predictable."

Kile kitabu unachokiita katiba ni ushahidi wa hali halisi ya kisiasa ambayo iko kwenye nchi husika. CCM kuogopa katiba siyo kigezo cha kusema kwamba katiba mpya ndiyo mwarobaini (A Holy Grail). Mwaka 1992 CCM na watanzania kwa ujumla tulipinga vikali mno mapendekezo ya tume ya Jaji Nyalali kuhusu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi, lakini hata baada ya kuletwa na katiba kufanyiwa marekebisho bado watu wanaendelea kufanya uovu tu.

I finish with the words of Professor Oliver Wendell Holmes "Law is a servant of man, not the opposite..."
 
Baada ya Bunge la CCM kupitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World ya Dubai hakuna tena shaka kuwa adui wa taifa hili ni CCM.

Kumbe ile dana dana iliyokuwa ikipigwa kuchelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya, ilikuwa kuwezesha Tanzania kuingia laini katiba mikataba ya aina hii.

Sote tumeshuhudia vipengele kadhaa ndani ya hii Katiba chakavu vikitumika lengo kuu likiwa ni kuhalalisha makabidhiano ya bandari zetu kwa wageni.

Baada ya bandari kipi kitafuata?
Katiba mpya bora ni muhimu !!
 
Back
Top Bottom