Danadana za Tume ya Jaji Chande na matokeo yanayotarajiwa

Lexuss

Member
Joined
Mar 24, 2026
Posts
24
Reaction score
28
Tume ilipoteuliwa.jpg

Tangu Tume ya Uchunguzi wa matukiuo ya Uvunjifu wa Amani kabla na baada ya Oktoba 29, 2025 ilipoanzishwa Novemba 20, 2025, watu waliitilia shaka utendaji wake na kwamba haiwezi kuwa huru.

Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, akisaidiwa na wajumbe saba (7): Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, na Dkt. Stergomena Tax.

Walioikosoa tume hiyo walisema haiwezekani Rais Samia Suluhu Hassan anayelalamikiwa katika mambo yaliyotokea Oktoba 29, 2025 halafu aunde tume tena kujichunguza. Kutokana na hilo, kumekuwa na wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru wa matukio hayo kwa kutumia chombo huru cha kimataifa.

Pia, wajumbe wa tume hiyo walikuwa wastaafu wa Serikali na wenye viapo, huku wengine akiwamo Stergomena Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati matukio hayo yanatokea, sasa anajichunguzaje?

Akizindua tume hiyo Novemba 20, 2025, Rais Samia alisema wameanza na tume hiyo na kisha tume nyingine zitakazokuja zitaanzia kwenye tume hiyo. Hata hivyo, kauli hiyo ilionekana kama kukwepa uchunguzi huru unaodaiwa.

Danadana za Tume

Awali tume hiyo ilipewa siku 90 kuchunguza matukio hayo hivyo ilitarajiwa kukamilisha kazi yake Februari 20, 2026.

Lakini ilipofika tarehe hiyo, Jaji Chande aliomba kuongezewa muda wa siku 42, yaani ifike Aprili 3 kwa maelezo kuwa muda huo wa ziada unalenga kuipa tume fursa ya kukamilisha ukusanyaji na uchambuzi wa ushahidi, pamoja na kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali (walio ndani au nje ya nchi) kutoa taarifa au maoni yao kuhusu fujo zilizozuka.

Hata hivyo, ilipofika Aprili 3, tume hiyo iliendeleza danadana zake kwa kuomba kuongezewa siku 21 yaani ikamilishe kazi Aprili 24.Safari hii Jaji Chande akasema kuwa wanaendelea kupokea ushahidi, wanataka wapate ushauri wa kitaalamu na pia wanataka waiandike ripoti jkwa Kiswahili na Kiingereza.

Jaji Chande alisisitiza kuwa Tume hiyo inatakeleza majukumu yake kwa weledi bila kuingiliwa, huku akifafanua kuwa ombi la muda limeletwa ili kukamilisha hatua za muhimu ikiwemo taarifa hiyo kutafsiri kwa kiswahili.

Danadana hizi zinaonyesha kuwa Tume hiyo inasoma upepo wa siasa. Inawezekana kabisa taarifa walizokusanya ziko tayari ila wanaangalia watakapozitoa zitatafsiriwaje na wananchi na hata jumuiya ya kimataifa?

Ikumbukwe kwamba Rais Samia alisema ilikuwa mchakato wa maridhiano uanze baada ya uchaguzi, ambapo angeunda Tume ya usuluhishi na maridhiano, lakini akasema ni mpaka Tume ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 imalize kwanza kazi yake.

Wakati maridhiano yakisubiriwa, watu wanahoji kuhusu kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambayo nayo inapigwa danadana mahakamani. Je, hatima ya kesi hiyo ni nini? Kesi itaendelea au Lissu ataachiliwa? Kama kesi itaendelea, mbona inacheleweshwa?

Wapo wanaodai kuwa huenda kesi hiyo inapigwa danadana ili tume hiyo itakapotoa taarifa yake, imalize kwa kushauri kuwepo maridhiano na kusameheana na hapo ndipo kesi ifutwe. Je, CHADEMA waliokataa maridhiano hayo watakubali kusamehe na kuridhia kila kitu?

Waandishi wa habari wafukuzwa

Januari 24, 2026 mjumbe wa tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu, Ibrahimu Juma alitangaza kuzia waandishi wa habari kuripoti mwenendo wa uchunguzi wa tume hiyo wakati tume hiyo ikiwa Ubungo jijini Dar es Salaam kufuatilia vikao vya kusikiliza waathirika, akisema baada ya waathirika kusikilizwa, ndipo waandishi waje kuuliza maswali.

Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya tume kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya waathirika, waliodai kuwa taarifa zao binafsi zinasambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya kutoa ushuhuda wao.

Hatua hiyo ilikuwa ni piigo kwa uhuru wa habari na ilionyesha kuwa tume hiyo ilikuwa ikiendesha kazi zake kwa kificho na huo unaweza kuwa mkakati wa kupika ripoti.

Ujio wa Dk Chakwera
Tume Chakwera.png

Kuna uwezekano mkubwa kuwa Tume ya Jaji Chande ilisogeza utoaji wa ripoti mbele ili kufuatilia kwanza ujio wa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ambaye pia ni Rais mstaafu wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera, aliyetua nchini tangu Aprili 9, 2025.

Dk Chakwera amekutana na kufanya mazungumzo na vyama vya siasa vya CHADEMA, ACT Wzalendo na vingine vidogo, huku pia akikutana na ujumbe wa Serikali uliongozwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Pia, Dk Chakwera alikutana na kufanya mazungumzo na Tume ya uchunguzi wa Matukio ya vurugu za uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Ikumbukwe kwamba, Dk Chakwera alitakiwa afike Tanzania tangu Novemba 2025, lakini Serikali ilizuia hadi, baada ya Profesa Kabudi alipokutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola jijini London nchini Uingereza alipokuwa akiiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya Madola na mikutano ya kisekta. Katika ziara hiyo (Machi 2026), ambapo suala la kuzuiwa kwa mwakilishi huyo lilijadiliwa.

Kwa hiyo, ujio wa Dk Chakwera haujafurahiwa na Serikali, ni kwa vile tu hawawezi tena kumzuia.

Hivyo, huenda Tume ya Jaji Chande imewekwa pembeni kwanza ili Dk Chakwera akamilishe uchunguzi wake, halafu akimaliza watataka kujua mwelekeo wa ripoti yake utakuwaje.

Propaganda za kuitetea tume

Wakati tume hiyo ikiendeleza danadana zake, baadhi ya viongozi wameonekana wakiitetea tume ya Jaji Chande. Viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk. Maimbo Mndolwa, aliyesema Tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 ni huru na kwamba wananchi wanayo matumaini makubwa na tume hiyo.

Dk. Mndolwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari, ambapo ameeza kuwa ni busara kwa taifa kushughulikia changamoto zake kwa kutumia mifumo ya ndani kabla ya kuomba msaada kutoka nje ya nchi.

Mwingine ni Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally aliyeeleza matumaini yake kwa Tume ya uchunguzi wa vurugu za wakati na baada ya uchaguzi.

Pia kumekuwa na vipindi vinavyorushwa vikionyesha wananchi wakiipongeza tume hiyo.

Matokeo yanayotarajiwa
Hii yote ni kuonyesha matokeo ya Tume ya Jaji Chande yanatarajiwa kuegemea upande mmoja wa kuitetea Serikali na kuwakandamiza wananchi waliokuwa wakidai haki. Pia imelenga kuisiafisha Serikali na udhalimu uliofanyika Oktoba 29.
 
Kwenye hao wajumbe mwakilishi anaewakilisha wananchi ni nani? Maana wananchi walitakiwa kuchagua mjumbe wao wa kuwawakilisha katika hiyo tume kama hamna mwakilishi wa wananchi ni utoto
 
View attachment 3572467
Tangu Tume ya Uchunguzi wa matukiuo ya Uvunjifu wa Amani kabla na baada ya Oktoba 29, 2025 ilipoanzishwa Novemba 20, 2025, watu waliitilia shaka utendaji wake na kwamba haiwezi kuwa huru.

Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, akisaidiwa na wajumbe saba (7): Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, na Dkt. Stergomena Tax.

Walioikosoa tume hiyo walisema haiwezekani Rais Samia Suluhu Hassan anayelalamikiwa katika mambo yaliyotokea Oktoba 29, 2025 halafu aunde tume tena kujichunguza. Kutokana na hilo, kumekuwa na wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru wa matukio hayo kwa kutumia chombo huru cha kimataifa.

Pia, wajumbe wa tume hiyo walikuwa wastaafu wa Serikali na wenye viapo, huku wengine akiwamo Stergomena Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati matukio hayo yanatokea, sasa anajichunguzaje?

Akizindua tume hiyo Novemba 20, 2025, Rais Samia alisema wameanza na tume hiyo na kisha tume nyingine zitakazokuja zitaanzia kwenye tume hiyo. Hata hivyo, kauli hiyo ilionekana kama kukwepa uchunguzi huru unaodaiwa.

Danadana za Tume

Awali tume hiyo ilipewa siku 90 kuchunguza matukio hayo hivyo ilitarajiwa kukamilisha kazi yake Februari 20, 2026.

Lakini ilipofika tarehe hiyo, Jaji Chande aliomba kuongezewa muda wa siku 42, yaani ifike Aprili 3 kwa maelezo kuwa muda huo wa ziada unalenga kuipa tume fursa ya kukamilisha ukusanyaji na uchambuzi wa ushahidi, pamoja na kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali (walio ndani au nje ya nchi) kutoa taarifa au maoni yao kuhusu fujo zilizozuka.

View attachment 3572468

Hata hivyo, ilipofika Aprili 3, tume hiyo iliendeleza danadana zake kwa kuomba kuongezewa siku 21 yaani ikamilishe kazi Aprili 24.Safari hii Jaji Chande akasema kuwa wanaendelea kupokea ushahidi, wanataka wapate ushauri wa kitaalamu na pia wanataka waiandike ripoti jkwa Kiswahili na Kiingereza.

Jaji Chande alisisitiza kuwa Tume hiyo inatakeleza majukumu yake kwa weledi bila kuingiliwa, huku akifafanua kuwa ombi la muda limeletwa ili kukamilisha hatua za muhimu ikiwemo taarifa hiyo kutafsiri kwa kiswahili.

Danadana hizi zinaonyesha kuwa Tume hiyo inasoma upepo wa siasa. Inawezekana kabisa taarifa walizokusanya ziko tayari ila wanaangalia watakapozitoa zitatafsiriwaje na wananchi na hata jumuiya ya kimataifa?

Ikumbukwe kwamba Rais Samia alisema ilikuwa mchakato wa maridhiano uanze baada ya uchaguzi, ambapo angeunda Tume ya usuluhishi na maridhiano, lakini akasema ni mpaka Tume ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 imalize kwanza kazi yake.

Wakati maridhiano yakisubiriwa, watu wanahoji kuhusu kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambayo nayo inapigwa danadana mahakamani. Je, hatima ya kesi hiyo ni nini? Kesi itaendelea au Lissu ataachiliwa? Kama kesi itaendelea, mbona inacheleweshwa?

Wapo wanaodai kuwa huenda kesi hiyo inapigwa danadana ili tume hiyo itakapotoa taarifa yake, imalize kwa kushauri kuwepo maridhiano na kusameheana na hapo ndipo kesi ifutwe. Je, CHADEMA waliokataa maridhiano hayo watakubali kusamehe na kuridhia kila kitu?

Waandishi wa habari wafukuzwa

Januari 24, 2026 mjumbe wa tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu, Ibrahimu Juma alitangaza kuzia waandishi wa habari kuripoti mwenendo wa uchunguzi wa tume hiyo wakati tume hiyo ikiwa Ubungo jijini Dar es Salaam kufuatilia vikao vya kusikiliza waathirika, akisema baada ya waathirika kusikilizwa, ndipo waandishi waje kuuliza maswali.

Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya tume kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya waathirika, waliodai kuwa taarifa zao binafsi zinasambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya kutoa ushuhuda wao.

Hatua hiyo ilikuwa ni piigo kwa uhuru wa habari na ilionyesha kuwa tume hiyo ilikuwa ikiendesha kazi zake kwa kificho na huo unaweza kuwa mkakati wa kupika ripoti.

Ujio wa Dk Chakwera
View attachment 3572472
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Tume ya Jaji Chande ilisogeza utoaji wa ripoti mbele ili kufuatilia kwanza ujio wa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ambaye pia ni Rais mstaafu wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera, aliyetua nchini tangu Aprili 9, 2025.

Dk Chakwera amekutana na kufanya mazungumzo na vyama vya siasa vya CHADEMA, ACT Wzalendo na vingine vidogo, huku pia akikutana na ujumbe wa Serikali uliongozwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Pia, Dk Chakwera alikutana na kufanya mazungumzo na Tume ya uchunguzi wa Matukio ya vurugu za uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Ikumbukwe kwamba, Dk Chakwera alitakiwa afike Tanzania tangu Novemba 2025, lakini Serikali ilizuia hadi, baada ya Profesa Kabudi alipokutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola jijini London nchini Uingereza alipokuwa akiiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya Madola na mikutano ya kisekta. Katika ziara hiyo (Machi 2026), ambapo suala la kuzuiwa kwa mwakilishi huyo lilijadiliwa.

Kwa hiyo, ujio wa Dk Chakwera haujafurahiwa na Serikali, ni kwa vile tu hawawezi tena kumzuia.

Hivyo, huenda Tume ya Jaji Chande imewekwa pembeni kwanza ili Dk Chakwera akamilishe uchunguzi wake, halafu akimaliza watataka kujua mwelekeo wa ripoti yake utakuwaje.

Propaganda za kuitetea tume

Wakati tume hiyo ikiendeleza danadana zake, baadhi ya viongozi wameonekana wakiitetea tume ya Jaji Chande. Viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk. Maimbo Mndolwa, aliyesema Tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 ni huru na kwamba wananchi wanayo matumaini makubwa na tume hiyo.

View attachment 3572473

Dk. Mndolwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari, ambapo ameeza kuwa ni busara kwa taifa kushughulikia changamoto zake kwa kutumia mifumo ya ndani kabla ya kuomba msaada kutoka nje ya nchi.

Mwingine ni Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally aliyeeleza matumaini yake kwa Tume ya uchunguzi wa vurugu za wakati na baada ya uchaguzi.

View attachment 3572474

Pia kumekuwa na vipindi vinavyorushwa vikionyesha wananchi wakiipongeza tume hiyo.

View attachment 3572475
Matokeo yanayotarajiwa
Hii yote ni kuonyesha matokeo ya Tume ya Jaji Chande yanatarajiwa kuegemea upande mmoja wa kuitetea Serikali na kuwakandamiza wananchi waliokuwa wakidai haki. Pia imelenga kuisiafisha Serikali na udhalimu uliofanyika Oktoba 29.
Mahimbo mndolwa ni askofu wa kanisa gani masengu likubwa
 
Hii tume haina tofauti na ile kauli ya Magu kwa wakurugenzi wa halmashauri. Majibu yake yanajulikana hata kabla ya kutolewa hadharani.
 
Back
Top Bottom