Bwana Dangote Tajiri Mkubwa Afrika ameeleza Kwa uchungu namna Mtu mweusi ana roho mbaya ya kuthamini vitu vya mweupe lakini sio vitu vya kwao weusi.
Vikwazo alivyokutana navyo bwana Dangote ni uthibitisho wa akili za hovyo za mtu mweusi.Haya hapa Tanzania awamu Ile iliyopita kulibakia kidogo afungashe virago kwenye biashara ya saruji Mtwara Kwa sababu zile zile za kukosa akili Kwa mtu mweusi.
Just imagine huyo ni Tajiri anayumbishwa hivyo itakuwaje Kwa mfanyabiashara na mjasiliamali wa kawaida?
Tangote ni mfano wa mbali ila ukitaka kujua Hali ikoje Kwa mtu mweusi wa hapa Tanzania nenda tuu katafute passport ya kusafiria Nje Nchi na usiwe na jina Kisiasa au Cheo ndio Utajua hujui.👇👇
Takribani wiki mbili zilizopita, kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), tajiri mkubwa barani Afrika, Aliko Dangote, alikaribia kulia akizungumzia hali ngumu ya kibiashara anayopitia.
Miezi michache iliyopita, Dangote alitangaza uzinduzi wa moja ya viwanda vikubwa vya kusafisha mafuta barani Afrika kwa lengo la kuzalisha mafuta kwa gharama nafuu kwa wananchi.
Kwa bahati mbaya, tangu uzinduzi wa kiwanda chake cha kusafisha mafuta, Aliko amekumbana na vikwazo vingi vya kibiashara. Serikali ya Nigeria, ambayo ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani, ilidai kwamba haina mafuta ghafi ya kumpatia Dangote.
Dangote alikasirika sana aliposikia habari hizi na akaamua kwenda Brazil na Marekani kununua mafuta ghafi. Kwa bahati mbaya, na kwa mshangao wake mkubwa, alipotaka kuingiza mafuta haya ghafi kutoka nchi hizo kwa ajili ya kuyasafisha kwenye kiwanda chake, serikali ya Nigeria ilipinga ikisema kwamba hana leseni za uagizaji
Chanzo: Mwananchi
----
My Take
Pole sana bwana Dangote,ukitaka uwe safe na utajiri wako hapa Afrika lazima upige Magoti Kwa Wanasiasa au naweza pia uwe mwanasiasa.👇👇
View: https://twitter.com/EduTalkTz/status/1818741061625495640?t=SqzsC3V1Dz2qtxdH4o21Jw&s=19