Dangote aongoza kwa utajiri Afrika, Mo Dewji ashika nafasi ya 16

Dangote aongoza kwa utajiri Afrika, Mo Dewji ashika nafasi ya 16

Umasikini wa akili na wivu ndio umekujaa. Fungua hata kuuza karanga tuone utawalipa sh ngapi.
Biashara yeye kakopa na kuwekeza hela anaitaka irudi na apate faida
Matajiri wa Tanzania wanafaidi sana, sijui ni wangapi wameingia katika stock market ili kuwafaidisha watu wengi zaidi na huyu Mo anapenda kujisifu kuwapa watu wengi ajira lakini sidhani kama anajali kuhusu mishahara na mazingira ya kazi. Pure capitalism and selfishness at its level best

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umasikini wa akili na wivu ndio umekujaa. Fungua hata kuuza karanga tuone utawalipa sh ngapi.
Biashara yeye kakopa na kuwekeza hela anaitaka irudi na apate faida

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijui hata kama umeelewa au unakimbilia kunijibu. No wonder tupo maskini hadi leo maana hata tu kuelewa tu faida za kampuni kubwa kama hizo kwenda public hatujui na umuhimu wa kampuni kama hiyo kutoa stahiki kwa wafanyakazi wake kulinda reputation yake. Ila ndo tupo bongo, average thinkers na tupo okey with just anything, mtu anatengeneza super normal profits out of exploitation unataka nimpigie makofi. To hell with your personal attacks to anonymous guy on Jf
 
Kuhusu mafao ni makubaliano kaka wanasema kama unaona ndogo unatafuta pazuri zaidi...ila in reality Mo ndo anaongoza kwa kuajili watu wengi zaidi afrika mashariki na kati.Nadhani kilichomahusha ni serikali kukamata soko la korosho maana ndo alikua anacontrol akmost 90%

Sijakataa na ndio maana nimesema ni pure capitalism. Naelewa anachokifanya na ninampongeza lakini anatakiwa kujali malipo na mazingira ya kazi kwa hao wafanyakazi ambao ameamua kuwa nao.
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji (Mo) ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 20 wa Afrika kwa ripoti ya mwaka 2020 licha ya utajiri wake kupungua kwa Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni).

Katika orodha hiyo ya jarida mashuhuri la Forbes kwa mwaka huu limemtaja Mo mwenye miaka 44 kama bilionea namba 16 huku mfanyabiashara wa saruji, sukari na unga (Aliko Dangote wa Nigeria) akiongoza orodha hiyo.

Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.6 (Sh3.69 trilioni) na anayeshikilia namba moja utajiri wake ni Dola bilioni 10.1 (Sh23.31trilioni) naye utajiri wake ukiwa umepungua kutoka bilioni 10.3 (Sh23.78 trilioni) mwaka jana.

Katika orodha ya jarida hilo mwaka jana Mo ambaye ni raia wa Tanzania anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 14 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.9 (Sh4.3trilioni) hivyo kwa mwaka huu ameshuka nafasi tatu.

“Imepungua Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni), lakini nina watu 32,000 na mwaka huu natarajia kuwekeza Sh500 bilioni hapa hapa nchini na uwekezaji huo utatoa ajira 100,000 kwa Watanzania,” alisema Mo baada ya ripoti hiyo akiwa ndiye Mtanzania pekee aliyeingia katika orodha hiyo.
[/
 
Back
Top Bottom