Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Wakuu hali inazidi kuwa mbaya, kila kitu ni kilio bei juu, Gesi ya kupikia imepanda, mafuta ya kula yamepanda, mafuta yamepanda na sasa na Dangote kapandisha Sementi kisa gharama za usafiri sijui tukimbilie wapi hali inabana na vipato vipo vilevile kazi ipo kwa Watanzania.
====
Kwa Tafsi ya Barua
Kutokana na kuendelea kupanda kwa gharama za usafirishaji, malighafi, na gharama za uendeshaji kwa ujumla, Dangote Cement Limited Tanzania (DCLT) itafanya marekebisho ya bei za saruji kuanzia tarehe 12 Mei 2026 saa 00:00.
Bei ya aina zote za saruji — ikiwa ni pamoja na 32.5R, 32.5N, 42.5N, 42.5R, na 52.5N — itaongezwa kwa Shilingi 700 kwa mfuko wa kilo 50 (bila VAT) katika masoko yote.
Pamoja na mabadiliko haya, DCLT inaendelea kujizatiti kutoa saruji ya ubora wa hali ya juu na kudumisha huduma bora kwa wateja. Tunathamini kwa dhati uelewa na ushirikiano wako endelevu.