Dangote atangaza ongozeko la Bei ya Sementi kuanzia 12 Mei 2026 kisa gharama za usafiri, malighafi na uendeshaji

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Wakuu hali inazidi kuwa mbaya, kila kitu ni kilio bei juu, Gesi ya kupikia imepanda, mafuta ya kula yamepanda, mafuta yamepanda na sasa na Dangote kapandisha Sementi kisa gharama za usafiri sijui tukimbilie wapi hali inabana na vipato vipo vilevile kazi ipo kwa Watanzania.

====

​

Kwa Tafsi ya Barua

Kutokana na kuendelea kupanda kwa gharama za usafirishaji, malighafi, na gharama za uendeshaji kwa ujumla, Dangote Cement Limited Tanzania (DCLT) itafanya marekebisho ya bei za saruji kuanzia tarehe 12 Mei 2026 saa 00:00.

Bei ya aina zote za saruji — ikiwa ni pamoja na 32.5R, 32.5N, 42.5N, 42.5R, na 52.5N — itaongezwa kwa Shilingi 700 kwa mfuko wa kilo 50 (bila VAT) katika masoko yote.

Pamoja na mabadiliko haya, DCLT inaendelea kujizatiti kutoa saruji ya ubora wa hali ya juu na kudumisha huduma bora kwa wateja. Tunathamini kwa dhati uelewa na ushirikiano wako endelevu.
 
Hiki ndicho kipindi ambacho wananchi wanaweza kuwapima kwa urahisi watu wanao watawala kama kweli wana chochote kitu kichwani, cha kuwasaidia kuondokana na huu ugumu wa maisha! Au ni mwendo tu wa taarab na mipasho ya hapa na pale.
 
Kuhusu kukurupuka hapana
 
Alisikika chura aka kizimkazi akisema hayo sio mambo yake.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Alikuja kwa mbwembwe bongo eti mifuko wa saruji ungefika 3,000 lakini Kuna sehemu nyingi hapoa bongo hata kuona tuu saruji zake madukani hazipo zaidi ya Twiga na Simba tulizozizoea
 
Yaani niache kutoa hela kununua kuku nile bata, eti ninunue Mchanga, au simenti.. nashauri apandishe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…