Dangote Cement penetrates giant Kenyan Cement Market

Hapo point moja ya ku note ni kuwa Kenya wanaagiza coal yote kutoka South Afrika. Kwa nini wasiagize Tanzania. Kwanza ni partner EA member na zipo tax benefits na pili Freight charges ni ndogo kutokana na distance?
Jee mkaa wetu uko bei juu?
Jee mkaa wetu unazalishwa kwa kiwango cha chini ?
Jee kuna ulazima kumlazimisha Dangote kununua coal Tanzania?
Nadhani Tuna matatizo lakini badala ya kuyaangalia kwa solution ya kitaalam na kibiashara tuna yaamua ki mwondo kasi
Hatufiki Ngooo
 
Serikali hipo nyuma ya msauzi afrika kuujumu dangote kwa sababu msauzi ndiyo anamiliki viwanda vya saruji nchini hivyo ujio wa dangote ulikuwa tatizo kwao
 
Kiwanda ni kiwanda tu,Hata cha gongo ni kiwanda kinachoajiri watu. Kwanza maviwanda makubwa makubwa ya nini, hata ndege mbona tumeanza na ndogondogo.
 
Hivi course za political science na public administration ziliwekwa kwa lengo gani... Hv kw nn tunawapa uongozi watu ambao hawana ideas about governance?? Mi naona madudu mengi ya viongozi Africa ni juu ya kuwa mbumbu wa elimu tajwa
Kama Dangotte atafunga kiwanda neno nchi ya viwanda lije lipigwe marufuku bora tuseme nchi ya jembe la mkono hyo ndy itakua saizi yetu..
Mana hata Sasa wasomi wengi ndiko wanaelekezwa na wenye kushka makali kwamba wakajiajili. Inaumaaa Sana. !!!!
 
Tanzania si sehemu salama/uhakika kwa uwekezaji.
Anytime watawala wanabadilika kutokana na mlichokubaliana officially.

Watu wataleta siasa, upambe, ujingaujinga tu at last kila kitu kinaharibika
 
Kuna tabia ya waTanzania kupenda kuiponda serekali yao bila hata kuujua ukweli,ilimradi tu awe ametoa kashifa kwa nchi yake na kuisifia ya pembeni,ni kawaida kabisa kwa waTanzania,kila ukifika vijiweni,kwenye mkusanyiko wa watu kidogo utakuta raia wanasema vibaya tu kwa kila kitu hata kama kuna jema hawalioni,hapa wewe ndugu hata unaweza usijue undani wa huyo Dangote alitaka yamkini kutubadilikiaje,ogopa sana ukiwa na watoto wa kike nyumbani kwako afu anaibuka tu jamaa anasema ataweka ofc ili watoto wako wapate ajira pia,kuna siku utajuta na utatamani kumfukuza lakini atakua keshazalisha watoto wako wote na hauwezi mfukuza kwa kua wajukuu zako watalelewa na nani.
 
Mimi yangu macho na masikio.Lakini Nina imani kuna jambo kubwa kuliko anayosema waziri na Dangote hadharani .Hapo lazima mikono ya mafisadi Wa bongo IPO tu.
 
Lakini habari yote hakuna sehemu inasema anafunga Tz akafungue Ke. Umeona anafungua kwenye nchi nyingine 9 zaidi ya tz. Na ana ubia na wahandisi wa kichina kujenga hivyo viwanda.

So anafungua Kenya kwa soko la huko labda na sudan kusini na uganda. Hiki cha kwetu ili pia auzie malawi zambia congo n.k.

Nipe ushahidi wowotw kuwa kufungua Kenya ndo anafunga huku.
 
Washauri wa serikali ili jambo linapaswa kuliangalia kwa umakini mkubwa isije ikawa majuto ni mjukuu. Uzalendo kwanza.
 
Acha ahamie kenya.
Huyu mfalme wetu sijui anawaza nini.
Mimi sijauona mkataba wa Dangote na serikali hii. Hata hivyo, kwa kadri ninavyofahamu mambo haya, asingeweza kujenga the biggest cement plant in Africa bila kuwa na Certificate of Incentives ya TIC. Ceritificate hiyo ina-summarize haki za mwekezaji kama zilivyo kwenye sheria. Kama hiyo Hati inampa haki ya kupata gesi bure basi atapata gesi bure. Vinginevyo mtamlipa fidia sawa na gharama ya gesi mliyomnyima. Huyu sio mchuuzi wa Kariakoo anayeweza kutishwa na akatishika. Yeye na kabila yake huwa wanatembea na majeshi ya wanasheria na tax planners na all sorts of professional advisors. Wanafanya maamuzi only upon professional advice, sio kama huyu mfalme wetu anayefikiri kila kitokacho kwenye kinywa chake ndio sheria ya nchi. Unasema angeenda mahakamani. Kwani nani kakuambia hataenda??? Au unafikiri kwenda kwenye international arbitration ni sawa na kwenda Kisutu???
 
Hivi Ninyi Mambulula mnajua kiingereza kweli?

Ni wapi Dangote kasema Anafunga Kiwanda Tanzania na kukihamishia Kenya?

Mbona mnaruka - ruka kama kuku anayetaka kutaga? wewe umeona hapo juu kuwa anafunga hiki cha Tanzania?

Dangote ana akili zaidi yenu, unadhani yeye hajui mchezo ulivyo? kwa Taarifa yenu Dangote anajua namna washindani wake wanavyohangaika usiku na mchana ili awe frustrated na kuondoka nchini ili awaachie soko la saruji maana wanamuona kama kawazibia zibia hivi, hivo msidhani kuwa huyo Dangote ni mtoto mdogo anajua kila kitu na hawezi kufanya kosa hilo kamwe la kuondoka nchini.
 
Haya mambo yaweza kuwa tunayaongea tu kijuu juu lakini nadhani kuna makubwa zaidi ya haya tunayoyaongea.
Ngoja tuone mwisho wake. Sijui ndo litaisha kimya kimya kama la sukari.
 
Viongozi wa nchi hii wanachoka 100%,wanadhoofisha maendeleo ya nchi kila kukisha.bored.
 
Hili sakata la Dangote ni kielelezo tu kuwa kama taifa hatujajipanga kwa kwa ajili ya kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hakuna nchi iliyopata maendeleo endelevu ya kiuchumi bila kuwa na taasisi huru na imara za kiuchumi na za kisiasa.

Tanzania haitaweza kwenda kokote kiuchuni chini ya katiba iliyopo. Badala ya kuweka taasisi huru na zenye nguvu za kiutawala, katiba yetu inamfanya rais kuwa kila kitu; halazimiki kukubali ushauri wowote kutoka kwa mtu yeyote na kwa hivyo inampa "leeway" ya kuendesha nchi kwa utashi wake tu! Nilishawahi kusema tena hapa JF kuwa kinyume na watu wengi wanavyoamini, urais wa JMT siyo taasisi bali ni utashi wa anayekalia kiti cha urais.

Katika mazingira haya, nchi ikiwa na rais mwenye weledi mdogo wa mambo ya kiuchumi na kijamii au anayefanya maamuzi kwa kuzingatia hisia zake tu inakuwa ni janga. Kama kwa mfano, kama rais anahisi tu kuwa kuna "dili" za watu katika mradi wa kiwanda cha Dangote, basi hiyo pekee inatosha kusabababisha sintofahamu iliyotokea. Hii inahushisha pia matumizi ya sheria kiupendeleo kwa kulenga "maadui wa kisiasa" kama ilivyoyokea kwa Mbowe kufurumushwa Billicanas ilhali wadaiwa wengine wa NHC wanaendelea kupeta; na Sumaye kunyang'anywa shamba ilhali kuna maelfu kwa maelfu wengine wenye mashamba tena kwa muda mrefu zaidi hawajaendeleza na hawajaguswa!

Habari kama hizi zimeripotiwa sana na vyombo vya kimataifa. Je ni ujumbe gani unapelekwa kwa wawekezaji watarajiwa (potential investors)? Kwamba Tanzania ni nchi hatari kwa uwekezaji kwa sababu inaendeshwa "arbitrarily". But this is self-inflicted damage!

Katiba iliyopo haifai pia kwa sababu inazalisha watawala wasiofaa na wasio na uzalendo kwa sababu ya kukosekana kwa taasisi huru na imara za kisiasa.
 
magufuli anania nzuri na nchi ila for sure will cost us big time
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…