Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,328
- 11,192
Ndugu, kama humjui Chongolo ungekaa kimya.YEHODAYA said:
Vetting ya CCM iliyopo ni ya kufa mtu kwa sasa Samia ameshika system ya serikali na Chama cheap politics has no room huyo chongolo kwenye system ni nani hopeless kabisa.
——————
Tulia dawa iwaingie.
Kalelewa ndani ya CCM kuanzia akiwa UVCCM na akina Nape, Nchimbi, Bashe nk. Ndie aliekuwa master mind wa kampeni za kuhuisha chama kwenye ziara ya miaka mitatu waliyofanya kuzunguka nchi nzima kipindi kile wakiwa na katibu Mkuu Abdulrahmani Kinana na Nape Nnauye. Ana masters ya uongozi kutoka Mzumbe University na kapata mafunzo maalum ya siasa na uongozi Urusi. Amekuwa akitumwa kwenye uangalizi wa chaguzi mbalimbali nje ya nchi kama mwakilishi wa CCM, zikiwemo Zambia, Zimbabwe, Malawi nk. Usimchukulie kirahisi rahisi namna hiyo mazee.
NYONGEZA
Kabla hajateuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Longido mnamo 2016, alikuwa ndie Mkurugenzi Mkuu wa vombo vya habari vya CCM kwa maana ya Magaeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na redio Uhuru. Alipoteuliwa akaacha ukurugenzi na kwenda kutumika Longido mkoani Arusha, kisha akahamishiwa Kinondoni. Siri yake kubwa ni kwamba anapenda kufanya mambo yake KIMYA KIMYA sana, huwezi kujua kirahisi. Hata kwenye chama hana umaarufu mkubwa wa kelele kama akina Nape, Makonda, Gambo, Kheri James na wengine.
Sasa mtu aliyeaminiwa kiasi hiki hawezi kuwa mwepesi mwepesi.