Daniel Chongolo awa Katibu Mkuu CCM

Daniel Chongolo awa Katibu Mkuu CCM

YEHODAYA said:
Vetting ya CCM iliyopo ni ya kufa mtu kwa sasa Samia ameshika system ya serikali na Chama cheap politics has no room huyo chongolo kwenye system ni nani hopeless kabisa.
——————

Tulia dawa iwaingie.
Ndugu, kama humjui Chongolo ungekaa kimya.
Kalelewa ndani ya CCM kuanzia akiwa UVCCM na akina Nape, Nchimbi, Bashe nk. Ndie aliekuwa master mind wa kampeni za kuhuisha chama kwenye ziara ya miaka mitatu waliyofanya kuzunguka nchi nzima kipindi kile wakiwa na katibu Mkuu Abdulrahmani Kinana na Nape Nnauye. Ana masters ya uongozi kutoka Mzumbe University na kapata mafunzo maalum ya siasa na uongozi Urusi. Amekuwa akitumwa kwenye uangalizi wa chaguzi mbalimbali nje ya nchi kama mwakilishi wa CCM, zikiwemo Zambia, Zimbabwe, Malawi nk. Usimchukulie kirahisi rahisi namna hiyo mazee.

NYONGEZA
Kabla hajateuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Longido mnamo 2016, alikuwa ndie Mkurugenzi Mkuu wa vombo vya habari vya CCM kwa maana ya Magaeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na redio Uhuru. Alipoteuliwa akaacha ukurugenzi na kwenda kutumika Longido mkoani Arusha, kisha akahamishiwa Kinondoni. Siri yake kubwa ni kwamba anapenda kufanya mambo yake KIMYA KIMYA sana, huwezi kujua kirahisi. Hata kwenye chama hana umaarufu mkubwa wa kelele kama akina Nape, Makonda, Gambo, Kheri James na wengine.
Sasa mtu aliyeaminiwa kiasi hiki hawezi kuwa mwepesi mwepesi.
 
DANIEL CHONGOLO APENDEKEZWA KUWA KATIBU MKUU CCM

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Ndg. Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho

Kwa sasa, Chongolo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar.


CCM asilia wameamua kuwaweka "wakuja" wote pembeni ikiwemo Dr. Bashiru Ally, Humphrey Polepole
 
Tueleze sasa Mkuu wewe unayejua. Kweli sijui. Kale kakamati kadogo kanaitwaje tena? Sijui Central Commitee au nini tena? Then Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM🤣🤣🤣🤣. Mimi siyo mtaalam wa haya Mambo.
Wajumbe wa CC:-
1.Mwenyekiti
2. Makamu wenyeviti wawili
3. Wenyeviti wa Jumuiya
4. Wakuu wa idara
5. Makamu wa raisi
6. Spika wa bunge wawili
7. Waziri mkuu
.......
 
Mpogoro uliipigania kweli hii nafasi ya KM, nakusalimia popote ulipo. Tulisema hufai ukabisha! Chezea fitna wewe! Wabaya wako tunaenda kunywa mvinyo na mdudu leo. Subiri kupangiwa kazi nyingine 😂😂
 
Wajumbe wa CC:-
1.Mwenyekiti
2. Makamu wenyeviti wawili
3. Wenyeviti wa Jumuiya
4. Wakuu wa idara
5. Makamu wa raisi
6. Spika wa bunge wawili
7. Waziri mkuu
.......
Shukrani. Hao wa Idara na Jumuiya si anaweza kusema wachaguliwe upya au? Maana wengine tayari wapo.
 
Mshikaji amekulia eneo fulani linaitwa Twico kwenye kiwanda cha mbao cha Sao hill- Mafinga.

Ametoka kwenye media akiwa mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru. Amejitahidi kutatua changamoto za ardhi akiwa Longido kbl ya kuhamishiwa Dar.

Yupo humble, si mtu wa majidai, mwenye uwezo fulani wa kutatua changamoto.

Tukiondoa ujuaji uliopo CCM kwamba wapo wenye CCM yao dogo anaweza kumudu!

KILA LA KHERI
Sahihi kabisa.
 
Napinga Chongolo hafai hiyo nafasi.Take note nilipinga Bashiru kuteuliwa na napinga Chongolo kupewa hiyo nafasi
Lakini si umesema vetting iliyoko Sasa CCM ni ya kufa mtu, Sasa kama ndo kweli iko hivyo kwa nini wanateuliwa watu wasiofaa kama huyu Chongolo?! Au we muongo kuwa sio kweli kwamba vetting ya ccm Ni ya kufa mtu
 
Wacheni Mungu aitwe Mungu,Makonda aliwahi kumkoromea vibaya sana huyu jamaa, sasa leo hii Makonda alitaka kumuona lazima aombe appointment.View attachment 1769200
Nikiangakia hii clip yaani mtu mzima unadhihakiwa mbele ya camera. Mke na Watoto wanakuona na ndugu na marafiki. Achilia mbali dunia nzima. Kila kiongozi alijiona Mungu mtu katika kiti chake kuanzia wa kisiasa hata wale watendaji kwenye Taasisi. Haya yote wakichukua kwa baba yao.
Watanzania huu siyo utamaduni wetu.

Hakika Mungu alisikia masononeko yetu. Mungu akaamua iwe kweli tena kwelikweli. Au nasema uongo ndugu zanguni? Hebu piga kelele za Shangwe kwa Mungu.
 
Shukrani. Hao wa Idara na Jumuiya si anaweza kusema wachaguliwe upya au? Maana wengine tayari wapo.
Wakuu wa idara si ndio hawa wameteiliwa mzee.
1. Itikadi na uenezi
2. Uchumi na fedha
3. Organization
4. Siasa na Uhusiano wa kimataifa
5. Naibu katibu mkuu bara
6. Naibu katibu mkuu zanzibar
 
Wacheni Mungu aitwe Mungu,Makonda aliwahi kumkoromea vibaya sana huyu jamaa, sasa leo hii Makonda alitaka kumuona lazima aombe appointment.View attachment 1769200
Aisee hii dunia bana tuishi kwa amani kesho yetu hatuijui...sasa huyu jamaa kwa cheo chake anaweza akafukuza Bashite Chamani
 
Back
Top Bottom