Daniel Chongolo awa Katibu Mkuu CCM

Daniel Chongolo awa Katibu Mkuu CCM

Chongolo
Suluhu.

Vowels trending inaendelea
Cc Pascal Mayalla
Mkuu The Boss , haya mambo ya numerology, watu humu hawayajui!.
P
 
Huyu Chongolo ndie katibu mkuu wa kwanza mwenye CV weak toka TANU na CCM vianzishwe.Makatibu wakuu waliomtangulia walikuwa na very strong CV
Unachokisema ni sahihi kabisa,maana hata mwenyewe namjua vizuri sana.Ila hata Mama naye CV yake sio kubwa ndio mana ametafuta anayeendana naye!. Ndege wanao fanana huruka pamoja mzee.

But ukiachana na mambo ya CV ya jamaa ni mnyenyekevu sana,na MTU poa sana.
 
Nikionaga comments za hivi nahamasika kutafuta Pesa zaidi ili nisilazimishwe kuongea hiyo lugha ya Malkia. Kiingereza kimenishinda kabisa na Shahada yangu niliyoipambania kwa jasho na kamasi.

Kwahiyo hata enterpreneurship ni changamoto 😎
 
Kwa hiyo Makonda ndiyo Basi tena?
Yaani Mama wa Watu ( Mheshimiwa Sana ) amrudishe Madarakani Mtu ambaye alimhatarishia Nafasi yake ndani ya miaka Mitano iliyopita kwa Kumfitinisha na Kumchongea kwa Bosi wake Mkuu Mtukutu, Mkurupukaji na mwenye Visasi vingi?

Nitamdharau mno Mama ( Mheshimiwa Sana ) nikisikia amemteua huyu 'Intarahamwe' wa Kanda ya Ziwa katika Nafasi yoyote ile kwani kwa zile 'dossiers' zake zilizopo Idara Nyeti ni Mtu Hatari mno kwa Ustawi mzima wa Amani ya Tanzania yetu hii.
 
Ninachojua mwaka 1999 - 2001 alisoma elimu ya kidato cha V - VI katika shule ya sekondari Mafinga sasa hivi inaitwa JJ Mungai! Kabla ya kuja kinondoni alikuwa Longido!
Aliuza mashine za magazeti ya uhuru kma skrepa na meko hakumfanya kitu
 
IMG_20210430_224641.jpg
 
Mshikaji amekulia eneo fulani linaitwa Twico kwenye kiwanda cha mbao cha Sao hill- Mafinga.

Ametoka kwenye media akiwa mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru. Amejitahidi kutatua changamoto za ardhi akiwa Longido kbl ya kuhamishiwa Dar.

Yupo humble, si mtu wa majidai, mwenye uwezo fulani wa kutatua changamoto.

Tukiondoa ujuaji uliopo CCM kwamba wapo wenye CCM yao dogo anaweza kumudu!

KILA LA KHERI
Malizia aliuza mashine za kuprint za uhuru kma vyuma chakavu,meko alipoenda alifoka bdae akamteua dc longido
 
Malizia aliuza mashine za uhuru kma vyuma chakavu ndio meko kumtoa na kumpa udc
Ndugu, kama humjui Chongolo ungekaa kimya.
Kalelewa ndani ya CCM kuanzia akiwa UVCCM na akina Nape, Nchimbi, Bashe nk. Ndie aliekuwa master mind wa kampeni za kuhuisha chama kwenye ziara ya miaka mitatu waliyofanya kuzunguka nchi nzima kipindi kile wakiwa na katibu Mkuu Abdulrahmani Kinana na Nape Nnauye. Ana masters ya uongozi kutoka Mzumbe University na kapata mafunzo maalum ya siasa na uongozi Urusi. Amekuwa akitumwa kwenye uangalizi wa chaguzi mbalimbali nje ya nchi kama mwakilishi wa CCM, zikiwemo Zambia, Zimbabwe, Malawi nk. Usimchukulie kirahisi rahisi namna hiyo mazee.

NYONGEZA
Kabla hajateuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Longido mnamo 2016, alikuwa ndie Mkurugenzi Mkuu wa vombo vya habari vya CCM kwa maana ya Magaeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na redio Uhuru. Alipoteuliwa akaacha ukurugenzi na kwenda kutumika Longido mkoani Arusha, kisha akahamishiwa Kinondoni. Siri yake kubwa ni kwamba anapenda kufanya mambo yake KIMYA KIMYA sana, huwezi kujua kirahisi. Hata kwenye chama hana umaarufu mkubwa wa kelele kama akina Nape, Makonda, Gambo, Kheri James na wengine.
Sasa mtu aliyeaminiwa kiasi hiki hawezi kuwa mwepesi mwepesi.
 
Mkuu The Boss , haya mambo ya numerology, watu humu hawayajui!.
P

P -Ea Radio 30-April 2021 Super Breakfast.

 
Mkuu maccm ni wale wale sitegemei kuona jipya lolote zaidi ya mauza mauza ya miaka nenda miaka rudi. Katiba ile ile iliyombeba yeye kuingia Ikulu kwenye COVID-19 anapiga kimya. Kuhusu kilio kikubwa cha Watanzania cha kupata katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi bado ANADEMKA.
Mnapolaumu basi angalau muonyeshe ufumbuzi ukoje. Sawa kunahitajika Katiba mpya. Mtueleze ITAPATIKANAJE? Mtaisubiri kama zawadi au mtaidai?
 
Back
Top Bottom