Daniel Chongolo: Tume huru ya Uchaguzi haileti chakula

Izia

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2021
Posts
303
Reaction score
477
Katibu mkuu wa CCM hataki Tume Huru ya Uchaguzi kwa sababu haileti chakula! Hivyo anataka kuendelea na tume iliyopo ili CCM iendelee kubaki madarakani kwa sababu anadai Tume Huru ya Uchaguzi ni ya wanasiasa kuwekwa madarakani.

Kwa akili hizi za viongozi wa CCM bado tuna safari ndefu kupata viongozi watakaochaguliwa na wananchi.


Your browser is not able to display this video.
 
Kuna vyeo viwili katika taifa hili vimelaaniwa na mungu, Katibu Mkuu CCM na Katibu Mwenezi CCM. Wote waliowahi kuteuliwa nafasi hizi basi pepo ya mungu wataisikia tu walahi.

Daniel Chongolo ameanza kujisahau kama alivyokua anajisahau Profesa Polepole. Muda wake utapita na yeye, acha aendelee kujichomoa akili.
 
Kilichonichosa zaidi ni waandishi wa habari hapa Nchini.
Mtu anajibu swali linazaa maswali yakujifunga halafu hawamuulizi.Halafu aliyewaita anajiona mjanja.

Teuzi zimeathiri na kuwatia woga waandishi wa habari
 
Tume ya uchaguzi inaleta chakula kwa CCM kupitia wananchi
 
Wanasubiri tumwage damu
 
Ishiii ivi kumbe tuna viongozi wajinga kupindukia.


Yaan Kwamba Tume huru ya Uchaguzi, haiwaletei wao CHAKULA.

Kwamba hii tume iliyopo, inawajaziaa wao na familia zao vyakula.
Wajinga ni sisi mkuu unadhani tukishinikiza kwa kuchoma ofisi za kijani Kila siku hawatatusikia maana tukisema tuwasubiri waamue wao never
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…