DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Kwa wana JF,

Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

C19A7F2F-4DFE-46D3-ACF0-DB4FC32A6CB5.jpeg


Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi na kukutwa na nyara za serikali pia katika makosa hayo.

32DDCC06-482A-44AE-BC2A-4CB7BC8A8852.jpeg

14D48533-716B-43DE-81BB-BAC440EE00AA.jpeg


Kwa Taarifa za awali, Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums

===========
Mfanyabiashara Akram Azizi amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 9,018.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka 70 ya kukutwa na silaha, mawili ya kukutwa na risasi, mawili ya kukutwa na nyaraka na moja la utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali wakuu, Paul Kadushi na Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana. Mshtakiwa ameenda rumande katika gereza la Segerea.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12, 2018.
 
Back
Top Bottom